JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kundi la watu wanaokadiriwa kuwa 8 usiku wa kuamkia Juni 4, 2022 wamevunja nyumba moja iliyopo Mtaa wa Bomani Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani na kufanya ukatili wa kubaka, kuiba vifaa vya ndani na kujeruhi kwa mapanga na kutokomea kusikojulikana
Wahalifu hao walifunga komeo kwa nyumba za majirani ili wasiweze kutoa msaada. Majeruhi, Estem Sevenia amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe baada ya kucharazwa mapanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema msako unaendelea kuwatafuta waliohusika na tukio hilo.
Mganga wa Zamu, Dkt. Sadi Amri amesema Estem amejeruhiwa kichwani na kwenye vidole.
Source: ITV