Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Katiba mpya? Inaondoaje vibaka. Kinachotakiwa ni kuimarisha mifuko ya ulinzi kuanzia ngazi za jamii, kipindi cha nyuma polisi jamii ilitiliwa mkazo kukawa na ulinzi shirikishi vitendo vya uhalifu vikapungua. Wakati wa mwendazake akasimamia uwajibikaji wa viongozi kila ngazi kukawa hakuna uzembe, kwa sasa hakuna uwajibikaji wala ndo sababu haya yanarudi. Mlinda nchi ni mwananchi kwa kuwa wahalifu ni ndugu zetu, watoto nk, tusimame kwa pamoja.KATIBA MPYA NDIYO SULUHISHO LA HAYO YOTE.
Huko ndio kuna DC mlamba lips kazi kuuza sura mitandaoniKundi la watu wanaokadiriwa kuwa 8 usiku wa kuamkia Juni 4, 2022 wamevunja nyumba moja iliyopo Mtaa wa Bomani Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani na kufanya ukatili wa kubaka, kuiba vifaa vya ndani na kujeruhi kwa mapanga na kutokomea kusikojulikana
Wahalifu hao walifunga komeo kwa nyumba za majirani ili wasiweze kutoa msaada. Majeruhi, Estem Sevenia amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe baada ya kucharazwa mapanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema msako unaendelea kuwatafuta waliohusika na tukio hilo.
Mganga wa Zamu, Dkt. Sadi Amri amesema Estem amejeruhiwa kichwani na kwenye vidole.
Source: ITV