SoC02 Kisasi sahihi cha kuponya jeraha lako la mapenzi kulinda afya ya akili

Stories of Change - 2022 Competition

mmmuhumba

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2017
Posts
493
Reaction score
478
KISASI SAHIHI CHA KUPONYA JERAHA LAKO LA MAPENZI KULINDA AFYA YA AKILI
Hivi karibuni mahusiano yameingia dosari kubwa ya kutisha, wapenzi/wenza wamekuwa wakifanyiana unyama wa kuchomana moto, kukatana mapanga na hata wengine kuua na kujiua nae na hili kuhusishwa na wivu wa mapenzi.

Ni kweli mapenzi ni hisia na raha zake upumbaza na kujenga ubinafsi, lakini kisasi kinapotawala huwa ni maamuzi ya hisia yanayotawala, sio mara zote umpeleka mtu katika maamuzi yalio sahihi bali yenye tu kuridhisha nafsi yake.

Kisasi huwa ni kitendo na hali ya kujichukia hadi kuzitoa hisia zako katika vitendo ambapo unaamua kurudisha ubaya au kumkomoa mtu yule aliyesababisha au unayehisi amesababisha yaliokufika.

Tuelewe kuwa sio visasi vyote wanaotenda huwa wanaujua ukweli wa jambo husika, wengine huwa wanahisi tu au wanakuwa ni maneno ya kuambiwa, hawana uhakika, wengine ni kuona tu lakini sio katika mazingira mabaya ila wanaingia hofu na kuhitimisha kile wanachokiwaza.

Maisha ya mapenzi na mahusiano hayana maana moja kwa kila mtu, kila mtu kuishi kulingana na anavyoona ni sahihi na sio makosa yote, watu huyakusudia mengine kuletwa na binadamu japo mengine huwa ni hulka zetu wanadamu, ndio maana wahenga walitufunza kuwa "janga halina mganga" yaani yanapotokea matatizo ya mapenzi na ndoa sio ya kukurupuka ni lazima utulie usiwe na papara ya maamuzi.

Kuna vitu vya kuzingatia pale unapopatwa na jambo lolote unaloliona ni zito kwako katika mapenzi na ndoa:

Zungumza, tafuta watu waliokuzidi umri waambie kinachokusumbua, unapopata tatizo na unaona linakuzidia unatakiwa uwe muwazi kama ni kwa mzazi wako, mlezi wako au mtu yeyote aliyekuzidi umri ambaye ni timamu. Kuzungumza ni kufungua vifungo au pingu inayokukabili, kuzungumza ni kuwa huru, kuzungumza ni mwanzo wa kufikiria maisha mengine mazuri yenye kukupa furaha na sio kuua mpenzi, kujiua, kujipa msongo wa mawazo. Kataa kuwa mtumwa wa ujinga wa mtu mwingine, zungumza maisha yako ni zawadi, wapo wagonjwa, majeruhi wanatamani kuwa wewe, usikubali kupoteza maisha yako.

Wengi wanaofikia uamuzi wa kujiua ni wale wanaopenda kujitenga pindi wanapokuwa katika wakati mgumu, kitendo cha kujitenda ni sumu kikatae, ishi na watu uvae viatu, wewe sio wa kwanza kufikwa.

Tambua thamani yako, kuwa mwanaume au mwanamke ni thamani tosha, haya yanayotokea ni makovu yanapita, ni mambo ambayo ni lazima uyapitie ili kujua nini unachokifanya kama mtu mzima na mtu timamu. Unapofanya maamuzi ya kuua au kujiua au kuharibu mali ni kukosesha thamani maisha yako na kupoteza thamani ya utu wa mtu. Kwanini ubadili maisha yako kuwa mfungwa?, mkimbizi?, muuaji?. Hapana yatazame maisha yako katika namna nyingine yenye manufaa, tizama familia yako, marafiki zako na jamaa zako wanaokuzunguka namna wanavyokutazama kabla ya kuingia kwenye hayo mahusiano.

Kila mtu unayepishana nae huwa na magumu yake lakini ukomaa nayo, sharti mungu angefungua mawazo ya watu, ungejiona wewe ni afadhali kuliko wengine.

Kumbuka kusudi la maisha yako. Tokea unakuwa hukuyajua mapenzi, mpaka unabalehe ndio ulipoanza kuyajua mapenzi, kabla ya yote unakuwa na malengo yako yaani ndoto zako, jifunze namna ya kuzifikia angalau ndoto zako. Kuwa na mwenza haimaanishi ndio uishi kama moto kwa kumsaidia yeye aweze kutimiza ndoto zake, au ndio wewe uwe umemaliza kila kitu lahasha ni wakati wa watu wawili kuungana kuyafikia malengo yenu, endapo kama atakutenda basi rudi nyuma angalia wapi umerudi na uanze safari yako. Ikumbukwe mapenzi ni kitu tunachokikuta njiani, pambana na hasira zako zisikutoe kwenye njia yako unayotaka kupita. Ujasiri wa kuushinda moyo ni ujasiri wa kufaulu maisha ya mapenzi.

Kuwa tayari kujifunza, ni msemo wa kila siku na wenye kuzoeleka kuwa “ elimu haina Mwisho ” sio tu darasani ila mpaka katika mapenzi tunamengi ya kujifunza, mahusiano ni maisha, kila siku unapaswa kujifunza, ni rahisi sana kumuona mwenzio aliyefiwa na ukampa pole, lakini ni ngumu kupokea pole pale unapokuwa umefiwa, na hivyo ndio yalivyo mapenzi pale unapotendwa, hivyo ni lazima tujikaze sisi binadamu kuyakabili magumu pindi yanapotufika.

Wewe ni jasiri. Mtu yeyote aliyemudu changamoto za maisha hapaswi kukubali kitu kingine kikamuangusha, anapawa kupambana na tatizo na sio kulikimbia kwa kujiua au kuua. Jamii bora inajengwa nawe jasiri wa mapenzi, inapaswa kuzitumia changamoto zote za mahusiano na maisha kujiimarisha kiakili, kiuchumi na kiafya.

Kisasi bora. Fanya maisha yako yawe bora zaidi, jiwekeze katika watu wengine na shughuli za uchumi, endelea kuishi katika macho ya aliyekushusha thamani, kuwa mwalimu wa wengine katika hizi changamoti, okoa maisha ya wengine na ishi katika ndoto zako.

Tambua, maisha kupata na kukosa yote tumeumbiwa sie binadamu na hata yasikupe maamuzi mabaya yatakayo haribu maisha yako, kataa kabisa kisasi kisicho na manufaa ni sumu kinayagharimu maisha yako, familia yako na ndugu zako. Kumbuka hakuna tiba ya mapenzi zaidi ya mapenzi, kuwa mvumilivu, kumbuka mapenzi upumbaza ipo siku utasahau na utapenda tena, kama ni fungu lako utampata mnayeendana lakini pia hawezi kuwa mkamilifu kwa kila kitu, ndio mana tumefunzwa “ bora shetani unayemjua, kuliko maliaka usiyemjua”. Lakini bado wengine waliwaza mbali wakasema "kuwahi sio kupata, bali ukipata jua la kufanya, ngoma ikikushinda waachie wanaoweza kuicheza, ukiing'ang'ania itakutia kilema".

Rai yangu kwa jamii, usijifiche na tatizo lako wala kujitenga na jamii yako, watoa elimu ya mahusiano wapo, unapoweka bayana changamoto yako ni rahisi kupata faraja na tiba.

Rai yangu kwa Wizara kupitia dawati la jinsia, elimu ya mahusiano itolewe katika jamii, dawati la jinsia lipewe muda wa kutoa elimu katika jamii juu ya mahusiano na ndoa, badala ya kusubiria kuletewa kesi.

Imarika katika elimu ya mahusiano, Taifa la Tanzania linakutegemea, kuyapenda maisha yako ni uzalendo, imarika.

Elimu ya mahusiano siyo tu darasani bali ni kwa kupitia changamoto unazokumbana nazo, ujasiri katika mapenzi ni kuimarika katika mapenzi ili kuepusha udhaifu wa akili na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
 
Upvote 19
Naamini itasaidia kupunguza msongo wa mawazo, visasi na kujenga jamii yenye mahusiano bora.
 
Nimekupigia Kura Naomba na Mimi unipigie Kura kupitia SoC 2022 - Tufuge nyuki kwa maendeleo endelevu na tuwalinde kwa wivu mkubwa
 
Elimu ya mahusiano siyo tu darasani bali ni kwa kupitia changamoto unazokumbana nazo, ujasiri katika mapenzi ni kuimarika katika mapenzi ili kuepusha udhaifu wa akili na kupoteza nguvu kazi ya Taini

Inasaidia Sana hii elimi
 
Assnte sana ndugu whitehossa. Kwa mawazo alika na wengine waje ipata
[emoji120]
 
Karibu kuchangia mawazo yako. Mahusiano bora yanajengwa kwa kuzungumza yenye tija na vitendo vyenye kujenga
 
Mapenzi ni hisia, yapo makundi ya watu wanateseka kwa kushindwa kujua njia sahihi ya kutatua changamoto zao za mapenzi.
1.kuw king'ang'anizi kwa mtu aliyemuacha
2. Kufikiria kujiua/ kuua
3. Kujitenga na jamii/ndugu
4. Kushindwa kufanya kazi/ kuacha/uzembe
5. Kufirisiwa/ kufirisika
6. Kupata maradhi ya mwili na akili.
Kupitia elimu kama hii inasaidia sana, watubwenye changamoto kama hii kujua nini cha kufanya yanapowafika.
 
Jikubali,Kuwa bize na mambo mengine,jichanganye muda ukiwa free,Kama inawezekana nenda mbaali nae kidogo wakati huo kujitengenezea new friends watakao kufanya uwe bize kidgo kuupa ubongo dira mpya ya kufuata baada ya iliyoyazoea.
Na pia kuvunja mahusiano huwa ni faraja ya kujipanga upya,wapi umeteleza ili wakati ujao usije rudia makos a Kama hayo,na pia huwezi juwa kwanini Mungu amependa yakomee hapo,inawezekana mbele pangekuwa na shida au kunaulopaswa kujifunza kwanza au ulienae hakuwa wako hivyo unaenda kutanishwa na wako
 
[emoji120] hakika Ndugu Iyambamgongo. Watu wanateseka kwa kuto yajua haya.
 
Kufanya uamuzi sahihi ni kuchagua kisasi sahihi cha kutunza ndoto zako, uhai wako, maendeleo yako na kuwa chachu ya wengine kuwa jasiri kama wewe.
#ujasiri katika maisha#
#imarika, mahusiano ndio msingi wa jamii yenye ustawi bora#
 
#imarika na elimika#
#kulinda maisha yako ni kulinda ustawi wako na jamii inayokuzunguka#
textgram_1667731705.jpg
 
Back
Top Bottom