Kishapu: Tshirt ya maandamano kumpinga Mpendazoe yavishwa Mbwa

Kishapu: Tshirt ya maandamano kumpinga Mpendazoe yavishwa Mbwa

Mgoyangi

Senior Member
Joined
Feb 6, 2008
Posts
184
Reaction score
9
Katika hali inayoonesha siasab za kuchekesha, baadhi ya wananchi katika mji mdogo wa Maganzo waliamua kumvisha Tshirt mbwa wakati wa maandamano ya kumlaani Mpendazoe kuhama CCM. Tshirt hizo zilizogawiwa kwa waandamanaji zikiwa na picha ya Mnec Sulemani Nchambi zilikuwa na maandishi Bandua Mpendazoe Bandika Nchambi, hali ambayo inatafsirika kuwa Mnec huyo ameanza kampeni za ubunge kabla ya muda.
 
DSC03224..JPGDSC03223..JPGDSC03220..JPGDSC03221..JPG
 
Hapo sana bandua mpendazoe bandika mbwa! huyo bwana atakuwa maeanza kampeni. NEC wako wapi? au ndo wamekaa ofisini kusubiri CCJ wanafanya nini?
 
kwa hiyo "bandua Mpendazoe, bandika mbwa"!

Wajua vichwa vya watu wengine vya wanachama nikutaka tu kujiweka katika jamii ati nao waonekane lakini ukirudi undani mwao wengi wao ni wafuasi bendera fuata upepo kabisa na hawaijui nini maana ya shahada yao ya kupiga kura bali wapo kusubili kula this time ndio kiboko yao ukikamatwa imekula kwao upokee na kumpa wote ndani.

Sasa hiyo style ya kumvarisha mbwa iyo Tshrt ya mpendazoe ni ushabiki kama ilivyo toke kule Tarime kati ya CCM na Chadema.

Amakweli hii ndio siasa yetu sie wabongo na tuta bakia hapo hapo

 
If there's somebody from kanda ya ziwa who real eager to change the ongoing political winds in the region, let them learn from this behaviour ya hao watu na wajue namna ya kuwasaidia ili kuleta ukombozi. Huko ndiko kura huwa zinaharibikia kwa kutumia wapiga kura bendera fuata upepo. kanda ya ziwa, saidieni hao wapiga kura.
 
Kanda ya Ziwa ndio wamelogwa na Mwenge wa Uhuru.Ndio huko watu wako poor,kuna madini,watu hawana elimu.
 
Hata kama ameanza kampeni JK mwenyewe unadhani vidampa wake je. Angekuwa mpinzani sheria ingemwajibikia, Sheria yenyewe inarejeshwa tena bungeni, juzi jamaa mmoja alikuwa na bango la CCJ huko Mwanza alikamatwa na polisi kisa kaanza kampeni. Ahaa.... Bongo bwana!
 
Katika hali inayoonesha siasab za kuchekesha, baadhi ya wananchi katika mji mdogo wa Maganzo waliamua kumvisha Tshirt mbwa wakati wa maandamano ya kumlaani Mpendazoe kuhama CCM. Tshirt hizo zilizogawiwa kwa waandamanaji zikiwa na picha ya Mnec Sulemani Nchambi zilikuwa na maandishi Bandua Mpendazoe Bandika Nchambi, hali ambayo inatafsirika kuwa Mnec huyo ameanza kampeni za ubunge kabla ya muda.

Inaonyesha jinsi wana CCM walivyo na roho mbaya hata mnyama ambaye wala hana akili yeyote wanaamua kumtumia kwenye laana zao. Kama hawana upendo hata kwa mbwa mnyama ambaye yupo tayari kumtii binadamu muda wote, je kweli hawa waweza kua na upendo wa kweli kwa binadamu wenzao ambao wanaweza kufikiri na kujua lipi baya na lipi zuri. CCM wamejisajau wakidhani wao tu ndio wanajua.
 
Hiyo ni warning sign, lazima wasome alama za nyakati. you can fool some people sometime but you cannot fool all the people all the time.CCM wajue hilo!!
 
Nilikuwa najaribu kuangalia kama ile chupa ya castle kule juu ina uhusiano na huyu mshikaji, maana wengine hu zinawatuma vibaya!! Ahh lakini kimtokacho mtu si ndiyo kiujazacho moyo wake??? Mungu jalia watu taifa lako!
 
Back
Top Bottom