Kisheria hii imekaaje?

Kisheria hii imekaaje?

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Wakuu Mimi umri wangu ni miaka 44 mpaka nafikia umri huu sijabahatika kupata mtoto wa ndoa zaidi ya kubambikiwa watoto wa nje ya ndoa, Mimi ni mjasiriamali japo pia ni mtumishi serikali katika idara ya afya, nilichelewa kuowa kutokana Na ugumu wa maisha niliokuwa nao.

Mwaka jana mwezi wa nilibahatika kufunga ndoa Na binti mwenye miaka 23 , binti wa kiislamu, Huwa nasafiri mara nyingi sana hasa ninapoteuliwa kwenda kwenye semina za afya , mke wangu amekuwa ni mtu wa kulalamika kuwa ninaposafiri ninamuacha mpweke kwa muda mrefu.

Huwa nikisafiri natumia muda wa wiki tatu mpaka mwezi mzima, mke wangu kwa Sasa anadai amechoka hali hiyo kwani pia analalamika pia simridhishi kwenye tendo la ndoa...anadai taraka ili aondoke akaendelee Na maisha mengine..tumeishi kwa mwaka mmoja Na miezi miwili, Na hatukubahatika kupata mtoto,

Je nauliza ndani ya muda huu nilioishinae anaweza kudai chochote katika Mali zangu ili tugawane,..namiliki pikipiki 3 kama bodaboda, nyumba mbili Na maduka manne ya kuuza nataka,
 
Hivi Sheria ya Ndoa si ipo wazi kuhusu mgawanyo wa Mali mara baada ya talaka?

Na kwanini ufikirie kumuacha binti wakati changamoto zenu mnaweza kukaa Chini na kuzitatua?

Hata hivyo Mkeo naona yupo sahihi kuhusu upweke, mwenzio nilipokuwa na Ndoa changa kama yako Mwaka 47, nilikuwa na safiri na Mke wangu kwenye shughuli zote za shamba.

As long unapoenda semina unalala Lodge kwanini usimchukue na yeye uambatane naye? Unamwacha lodge uliyofikia na wewe unaingia semina room, ukitoka unamkuta mwenzio alishapumzika Mchana kutwa, kwahiyo ni suala la kutupia tu hadi semina iishe unakuta Binti wa watu ameanza kutamani udongo na vitu vichachu chachu.
 
Kiislam mwanamke akidai talaka na akataka kujitoa katika ndoa yeye ndo anarudisha mahari uliyompa na anajivua.

Kisheria za nchi, sheria ya ndoa mtagawana zile mali mlizozichuma mkiwa pamoja tu, na kwa zile ambazo ulizichuma ukiwa pekeyako haitahesabika kuwa ni sehemu ya mali ya ndoa hivyo hatapata kitu hizo utabaki nazo zote.
 
Hivi Sheria ya Ndoa si ipo wazi kuhusu mgawanyo wa Mali mara baada ya talaka?

Na kwanini ufikirie kumuacha binti wakati changamoto zenu mnaweza kukaa Chini na kuzitatua?

Hata hivyo Mkeo naona yupo sahihi kuhusu upweke, mwenzio nilipokuwa na Ndoa changa kama yako Mwaka 47, nilikuwa na safiri na Mke wangu kwenye shughuli zote za shamba.

As long unapoenda semina unalala Lodge kwanini usimchukue na yeye uambatane naye? Unamwacha lodge uliyofikia na wewe unaingia semina room, ukitoka unamkuta mwenzio alishapumzika Mchana kutwa, kwahiyo ni suala la kutupia tu hadi semina iishe unakuta Binti wa watu ameanza kutamani udongo na vitu vichachu chachu.
Jama hana nguvu za kiume,hiyo changamoto sio ndogo,aachane na mambo ya ndoa
 
Ndio, mbaya mwanamke mwenyewe ni darasa la Saba, mahari nilitoa milioni 2 tena yote hawakutaka nitoe nusu
Basi hakikisha umpe talaka kwa mujibu wa uislamu na hiyo ni rahisi mwambie hivi kama yeye ndo amekuchoka sio wewe umemchoka, basi ajikomboe kwa mujibu wa uislamu demand kiasi akulipe ili aweze kutoka kwenye ndoa.

Unaweza kumwambia kwenye ile mahari milioni mbili ambayo nilikupatia nipe shilingi elfu 20 kisha jivue kwenye ndoa, so mtaita mashahidi na atasema kuanzia leo mimi sio mke wa Mwizukulu mgikuru na namrudishia hii elfu 20 kama sehemu ya mahari, hapo atakaa mwezi mmoja tu eda kuhakiki kama ni mjamzito kisha ataendelea na maisha yake.

Usikubali kufanya complications za mahakamani fanya nilivyokushauri, anyway darasa la pili sio tatizo.
 
Back
Top Bottom