Kisheria wabunge hawana mamlaka ya kupinga serikali 3

DCONSCIOUS

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Posts
1,269
Reaction score
473
Bunge la Katiba halina mamlaka kisheria kubadili chochote kilicho ndani ya rasimu!Ukirejea katika sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya iliyoridhiwa na Bunge la Jamhiri ya Muungano wa Tanzania na kusainiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete na kuwa SHERIA rasmi,utaona yafuatayo:

1. Tafsiri ya kifungu cha 25 (2)cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba juu ya Majukumu ya Bunge la Katiba Mpya inasema hivi: "Bunge Maalumu la Katiba litakuwa na jukumu la kuijadili rasimu ya Katiba na kuipitisha tu"Sheria hii ya mabadiliko ya Katiba inalifunga Bunge Maalumu la Katiba kuishia katika kujadili na kupitisha rasimu hiyo bila kuondoa neno wala kuongeza neno litakalobadili maana ya neo hilo.

Vivyo hivyo Bunge la katiba litafanya kazi ya kuboresha masharti ya Katiba yaliyomo ndani ya rasimu ya Katiba pasipo kuweka masharti mapya ambayo kwa taathira yatabadili ama kufifisha masharti ya kikatiba yaliyomo kwenye Rasimu hii ya Katiba Mpya.

Sasa msimamo wa ccm kuwa wao wanataka serikali mbili unatoka wapi ilihali katika rasimu hakuna pendekezo la serikali mbili wala moja, bali ni serikali tatu tu iliyopendekezwa na Watanzania 64%?T

aarifa zinasema ccm imechomeka rasimu mbadala huko Bungeni na kutia hofu kuwa huenda rasimu ya Watanzania iliyoratibiwa na Mzee wetu Warioba imetiwa kapuni.
 
CDM walipokuwa wanapigia kelele sheria ya mabadiliko ya katiba,ccm walikuwa wanachekelea,sasa wanataka mambo yabadilishwe kwenye rasmi ya katibampya wanajikuta walishajiwekia pingamizi la kisheria na sasa wanaanza kutapatapa
kujinusuru.
 
Mkuu wao walikuwa na maeneo yao ya interest kama wakuu wa mikoa, wilaya na kuhakiksha rais ndiyo anateua wajumbe badala ya kuidhinisha walioteuliwa na makundi.Kipengere kama hicho ccm haikuwa issue lakini sasa, wanausikilizia msumeno unavyokata.
 
Tafsiri ya kifungu cha 25 (2)cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba juu ya Majukumu ya Bunge la Katiba Mpya inasema hivi: "Bunge Maalumu la Katiba litakuwa na jukumu la kuijadili rasimu ya Katiba na kuipitisha tu"Sheria hii ya mabadiliko ya Katiba inalifunga Bunge Maalumu la Katiba kuishia katika kujadili na kupitisha rasimu hiyo bila kuondoa neno wala kuongeza neno litakalobadili maana ya neo hilo.
 
Mkuu wao walikuwa na maeneo yao ya interest kama wakuu wa mikoa, wilaya na kuhakiksha rais ndiyo anateua wajumbe badala ya kuidhinisha walioteuliwa na makundi.Kipengere kama hicho ccm haikuwa issue lakini sasa, wanausikilizia msumeno unavyokata.
Tuko pamoja mkuu,hata hili la kutobadilisha chochote walidhani warioba ataweka mambo ya kuibeba ccmm wakapitisha kisibadilishwe kitu fasta,leo wamejikuta walipokuwa wanavuka walivunja madaraja sasa wanataka kurudi wanakuta mafuriko.
 
"Bunge Maalumu la Katiba litakuwa na jukumu la kuijadili rasimu ya Katiba na kuipitisha tu"Sheria hii ya mabadiliko ya Katiba inalifunga Bunge Maalumu la Katiba kuishia katika kujadili na kupitisha rasimu hiyo bila kuondoa neno wala kuongeza neno litakalobadili maana ya neo hilo.

.
Kuna mtu alinidokezea kwamba Rasimu ya pili ndiyo KATIBA YENYEWE tunayoisubiri, mimi kwa uzuzu wangu nikambishia na bado nabisha!!
 
kuna Yule mwanasheria jk alisema anachanga wenzake, jana alisema bunge linaloendelea sasa hivi lina mamlaka ya kuvunja muunga mda wowote likihamua, ndio nikaamin maneno ya jk
 
Magamba hawawezi kujitungia sheria ngumu namna hii kwani itawabana mbavu wao wenyewe.
 
Subirini mje muone kiherehere cha magamba Lukuvi na mwasheria wao mkuu Werema watakavyojitahidi kupotosha kwa nia ya kuchakachua, hata hivyo ninapata imani jembe langu lipo Tundu Lisu kiboko yao
 
haya majizi ya ccm yatahangaika sana lakini hayatashinda kamwe. serikali 3 ni maamuzi yetu nikiwemo mimi nisiye na chama. sasa kama wataamua kuyabadilisha maamuzi yetu hawatabaki salama.

Bunge la Katiba halina mamlaka kisheria kubadili chochote kilicho ndani ya rasimu!Ukirejea katika sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya iliyoridhiwa na Bunge la Jamhiri ya Muungano wa Tanzania na kusainiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete na kuwa SHERIA rasmi,utaona yafuatayo:

1. Tafsiri ya kifungu cha 25 (2)cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba juu ya Majukumu ya Bunge la Katiba Mpya inasema hivi: "Bunge Maalumu la Katiba litakuwa na jukumu la kuijadili rasimu ya Katiba na kuipitisha tu"Sheria hii ya mabadiliko ya Katiba inalifunga Bunge Maalumu la Katiba kuishia katika kujadili na kupitisha rasimu hiyo bila kuondoa neno wala kuongeza neno litakalobadili maana ya neo hilo.

Vivyo hivyo Bunge la katiba litafanya kazi ya kuboresha masharti ya Katiba yaliyomo ndani ya rasimu ya Katiba pasipo kuweka masharti mapya ambayo kwa taathira yatabadili ama kufifisha masharti ya kikatiba yaliyomo kwenye Rasimu hii ya Katiba Mpya.

Sasa msimamo wa ccm kuwa wao wanataka serikali mbili unatoka wapi ilihali katika rasimu hakuna pendekezo la serikali mbili wala moja, bali ni serikali tatu tu iliyopendekezwa na Watanzania 64%?T

aarifa zinasema ccm imechomeka rasimu mbadala huko Bungeni na kutia hofu kuwa huenda rasimu ya Watanzania iliyoratibiwa na Mzee wetu Warioba imetiwa kapuni.
 
Bunge la Katiba halina mamlaka kisheria kubadili chochote kilicho ndani ya rasimu!Ukirejea katika sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya iliyoridhiwa na Bunge la Jamhiri ya Muungano wa Tanzania na kusainiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete na kuwa SHERIA rasmi,utaona yafuatayo:

1. Tafsiri ya kifungu cha 25 (2)cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba juu ya Majukumu ya Bunge la Katiba Mpya inasema hivi: "Bunge Maalumu la Katiba litakuwa na jukumu la kuijadili rasimu ya Katiba na kuipitisha tu"Sheria hii ya mabadiliko ya Katiba inalifunga Bunge Maalumu la Katiba kuishia katika kujadili na kupitisha rasimu hiyo bila kuondoa neno wala kuongeza neno litakalobadili maana ya neo hilo.

Vivyo hivyo Bunge la katiba litafanya kazi ya kuboresha masharti ya Katiba yaliyomo ndani ya rasimu ya Katiba pasipo kuweka masharti mapya ambayo kwa taathira yatabadili ama kufifisha masharti ya kikatiba yaliyomo kwenye Rasimu hii ya Katiba Mpya.

Sasa msimamo wa ccm kuwa wao wanataka serikali mbili unatoka wapi ilihali katika rasimu hakuna pendekezo la serikali mbili wala moja, bali ni serikali tatu tu iliyopendekezwa na Watanzania 64%?T

aarifa zinasema ccm imechomeka rasimu mbadala huko Bungeni na kutia hofu kuwa huenda rasimu ya Watanzania iliyoratibiwa na Mzee wetu Warioba imetiwa kapuni.
JF bana!, kila mtu ni mwanasheria!, ana uwezo wa kutafsiri sheria!.

Issue nyingine jape simple ni too tenchical kwa asiye mtaalamu!.

Uhalali wa katiba, utatokana na wananchi!. Watu waliopewa mandate na wananchi, ni wabunge wa bunge la katiba na sio Tume ya Warioba!.

Kazi ya tume ilikuwa ni kukusanya tuu maoni, ya wananchi, wawakilishi wao ndio wenye uamuzi wa mwisho!.

This is the situation!.

Sherehe ya harusi (katiba) inaandaliwa, kamati ya maandalizi inatumwa kuwauliza waalikwa watapenda kula nini?.
Kuna watakaopenda kula ugali, "serikali moja", kuna watakaopenda kula pilau "serikali mbili" na kuna watakaopenda kula biriani "serikali tatu!".

Kamati inaamua kufuatia wapenzi wa biriani kuwa wengi, kamati inaamua chakula cha harusi ni biriani!, "wengi wape!".

Kumbe "Bwana Harusi" anapenda pilau!, hivyo anaamua kuwaelekeza wapishi waandae pia mapishi ya pilau na hata ugali!.

Siku ya harusi imefika, chef (bunge la katiba) anarudi kwa mara ya mwisho kuhakiki kinapikwa nini kati ya ugali, biriani na pilau, ndipo bwana harusi anawauliza hao wageni wanapenda nini, wengi kwa sauti moja wanaitikia "pilau!", Bwana harusi anamwambia chef apike pilau!. Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi, hawezi tena kupinga eti pilau isipikwe kwa sababu mwanzo walio wengi walichagua biriani!.

Uamuzi wa wajumbe wa tume ya katiba walio wengi ndio final na sio mapendekezo ya tume ya Warioba!. Ya Warioba ni mapendekezo tuu yanaweza kukubaliwa, kurekebishwa, kuboreshwa au kukataliwa!.

Pasco.
 
Ndii tatizo la kuwaza kula mda wote badala hata ya kufikilisha ubongo kidogo.. mimi nimejenga hoja kwa kutumia kifungu cha sheria wewe unaleta habar za misosi ya ketchen party unaakili wewe.....mlizane ikuru wamefwata juice eee watu leo mmepigwa chenga ya kisigino mnabaki kutapatapa tu.
 
Back
Top Bottom