PreGE2025 Kishindo cha fainali jimbo cup, mbunge Samizi awaomba wananchi kuiunga mkono CCM na wagombea wake

PreGE2025 Kishindo cha fainali jimbo cup, mbunge Samizi awaomba wananchi kuiunga mkono CCM na wagombea wake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
397
Reaction score
445
KISHINDO CHA FAINALI JIMBO CUP, MBUNGE SAMIZI AWAOMBA WANANCHI KUIUNGA MKONO CCM NA WAGOMBEA WAKE

Wananchi wamshukuru Mbunge Samizi kwa alivyo mstari wa mbele kwa michezo na maendeleo.

Mhe. Samizi, Mbunge amehutubia maelfu ya wananchi na mashabiki wa Mpira wa miguu wa Kata 19 zilizopo Jimboni kwake Muhambwe ambapo Jana ilikuwa siku ya fainali kwa Timu ambazo zilifuzu kufika fainali kati ya Timu 94 zilizoshiriki ligi hiyo.

Ikiwa MGENI rasmi wa fainali alikuwa BAKARI OMARY SHEKARATA-Afisa Tarafa ya Kifura na Kaimu Afisa Tarafa ya Kibondo Mjini-akimuakilisha Mhe. Kanali Mstaafu Aggrey John Magwaza-Mkuu wa Wilaya ya Kibondo ambaye alialikwa kuwa MGENI rasmi wa fainali hiyo.

Soma Pia: Kuelekea 2025 - Orodha ya CV za Wabunge kwa mwaka 2020 - 2025 kutoka kila mkoa Tanzania

Aidha miongoni mwa Timu zilizofika Nusu fainali ni;
1 MBWA MWITU
2 KIBONDO STARS
3 BUSUNZU
4 KASANA
Hatimaye
Mbwa Mwitu na Kibondo Stars kutinga Fainali.
Ambapo mshindi wa kwanza MBWA MWITU amejinyakulia kitita cha fedha 800,000/= Taslimu na seti 1 ya Jezi, Mpira 1 pamoja na kubeba Kombe. Kibondo Stars 600,000/= Taslimu na seti 1 ya Jezi, Mpira 1. BUSUNZU FC 400,000/= Taslimu na seti 1 ya Jezi, Mpira 1. KASANA FC 200,000/= Taslimu na seti 1 ya Jezi, Mpira 1.

Timu zote 30 zilizofuzu ligi hiyo amezipa Jezi seti 1 na Mpira 1 kwa kila Timu iliyoshiriki ligi. Na kuwazawadia waamuzi Seti 3 zenye thamani ya Tsh 300,000/=
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Samizi, Mbunge amewaomba wananchi na mashabiki wa soko Jimboni kukiunga Mkono Chama cha Mapinduzi na kumpa kura za kishindo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuuliza wananchi wake kama hatoshi asichukuwe fomu ya kuwania mhura wa pili ikiwa wamemtaka achukuwe fomu na kumuahidi kumpa kura za kishindo kutokana na KAZI NZURI ambazo amezifanya za kuwa mdau mkubwa wa michezo na kuwaletea maendeleo katika Jimbo la Muhambwe.

SAMIZI KUPATA KURA ZA KISHINDO JIMBONI.

Imetolewa Na;
Kitengo cha habari na mawasiliano Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Muhambwe.

IMG-20250420-WA0013.jpg
IMG-20250420-WA0009.jpg
IMG-20250420-WA0007.jpg
 

Attachments

  • IMG-20250420-WA0011.jpg
    IMG-20250420-WA0011.jpg
    635 KB · Views: 34
michezo ni afya

wakisema NRNE jitokezeni kumunga mkono mama kwenye sanduku la kura hadi wabaki na mshangao
 
Back
Top Bottom