SI KWELI Kishindo cha Maandamano ya July 7, kufunguliwa kwa Shule kwaahirishwa

SI KWELI Kishindo cha Maandamano ya July 7, kufunguliwa kwa Shule kwaahirishwa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Hii ndio Taarifa ya sasa kutoka Tamisemi

Sasa shule zote zitafunguliwa July 13
1782902694280.png
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na barua inayosambaa ikidaiwa kutolewa na serikali kueleza kuwa muda wa wa kufungua shule umesogezwa mbele kutoka Julai 6, 2025 hadi Julai 13, 2026 kutokana na sababu zilizotajwa kwenye barua.

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejirirdhisha kuwa Taarifa hiyo si ya kweli na haijachapishwa na mamlaka husika kama ilivyodaiwa.

Taarifa hiyo imekuwa na baadhi ya dosari ikiwemo kutumia utambulisho wa Ofisi ya Rais TAMISEMI badala ya Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI kama wizara hiyo ilivyohamishwa kutoka ofisi ya Rais kwenda kwenye ofisi ya Waziri Mkuu.

Aidha jina la waziri wa elimu lililowekwa si sahihi wametumia jina la Dkt. Lyabwene Mtahabwa ambaye si Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na badala yake Waziri ni Prof. Adolf Mkenda.

Wizara hizo pia kupitia mitandao yao ya kijamii wamekanusha taarifa hiyo na kueleza kuwa siyo sahihi. Sambamba na hilo kupitia akaunti yao ya JamiiForums wizara ya elimu wameweka kalenda yao ya mwaka wa masomo 2026 ambapo tarehe ya kufungua shule ni Jula6, 2026.
Jukumu la kuilinda hii nchi ni jukumu letu wote,je wewe mkuu upo upande upi?

Kwasababu maandamano ni haki ya wananchi Kwa mujibu wa katiba.

Lakini je,wote tuna Elimu ya maandamano?

Kilichotokea 29 October mm mwaka jana, ilikuwa ni maandano,au fujo?

Kama Una akili timamu usiandamane.
Uhai na ustawi wako ni wa Thamani
Nyerere alitaka vijana wasiwe goigoi, wailinde katiba na haki ya wananchi
 
kwanini umewaza kwamba huyo atakuwa mtu wa uvccm ?
haiwezekani akawa a free thinker ?
Anataoika alicholishwa na viongozi wake. Ana sound familiar sana na kinacho imbwa na viongozi majukwaani hivi karibuni
 
Anataoika alicholishwa na viongozi wake. Ana sound familiar sana na kinacho imbwa na viongozi majukwaani hivi karibuni
haiwezekani mtu akawa huru na akatoa mawazo yake ynayofanana na hao watu wa ccm ?

kwa mfano TLS hutoa matamko yanayowafanya waonekane kama wapo upande wa Chadema, lakini ndani ya TLS wapo watu wengi kuanzia watumishi wa serikali, mawakili wenye itikadi za upinzani na hata wa Chama tawala.
 
Nisingeiamini nisingepoteza muda kukuuliza source. Nimeamini ndo maana nakuuliza, unless wewe ndo unaamua shule zifunguliwe lini, au taarifa bado si official otherwise kuna sehemu umeitoa hii habari. Tunaomba source kama hutojali.
Nakazia hoja. TAMISEMI au Serikali inatenda kwa kutoa Taarifa au Maelekezo kwa Maandishi/Waraka.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom