Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Mhe. Rais ameweza kujenga Ofisi yake kwenye standard ambazo hakuna msaliti anayepata mwanya; hii imepelekea mambo yafuatayo kwenda kama Ofisi ya Mhe. Rais inavyopaswa kuwa
1. Ofisi yake Kwa sasa imeweza kuwa na Siri kubwa; hakuna Siri kuvuja kama ilivyokuwa awamu za nyuma. Hii imefanya akina kigogo kukosa news na hivyo hadhi ya Ofisi hii kuendelea kupanda.
2. Mfumo wake wa kutafakari mambo umeondoa kabisa MALALAMIKO kwenye jamii; hakuna chuki au kisasi katika kufanya teuzi au kutengua; hakuna adui WA kudumu kwake.
3. Mfumo wake wa utendaji umerejesha heshima Kwa viongozi WA umma; hakuna mwenye kiburi cha madaraka kiasi cha kudharau adharani wananchi kama walivyoweza kufanya akina Sabaya na Makonda
4. Hakuna kiongozi ambaye NI mtoto WA mama; wakati wowote rafiki anaweza kuwa adui na hivyo hata wale wasioguswa wanaweza kuguswa.
Kwa msingi huu wapo Mawaziri na makatibu wakuu wameanza kumzoea mama kimatendo; wapo watu wanataka kumwonyesha mama kwamba wao NI Bora kwake kuliko wengine. Naamini Kwa kilichotokea kwenye ripoti ya CAG na ukimya WA mama siku mbili tatu kishindo kikubwa kinakwenda kusikika
Jambo ambalo SINA uhakika nalo NI uwezo wa mama kumfikisha kiongozi mahakamani; mama amezaliwa na roho wakusamehe na kuona mateso siyo Haki ya binadamu....