SALOK
JF-Expert Member
- Sep 20, 2011
- 3,364
- 2,001
Inasikitisha, Inahuzunisha ila uhalisia unabaki hivyo.
Nchi ya Tanzania kama yalivyo mataifa mengine Duniani inatamaduni zake na mifumo yake ya kiutawala! Democracy ndio mfumo unaotumika ktk kuendesha Nchi hususani mfumo wa vyama vingi vya siasa!
Tanzania kuna vyama vingi vya siasa vikubwa kwa vidogo! Ktk hivyo vipo vichache ambavyo ktk kipindi fulani kwa nyakati tofauti tofauti vipo vilivyokuja na sera na mikakati ya maana ktk kuonesha utayari wa kuchukua Nchi, hapa nazungumzia vyama pinzani. Lakini kwa kukosa pengine umadhubuti ktk sera na mikakati na ustahimilivu kwa sasa karibia vyote vimekumbwa na dhoruba kali la upinzani toka serikalini na chama kinachounda serikali na kisha kusambaratikia mbali huko, vimebaki majina tu, na hayo tunayashuhudia kwa NCCR-MAGEUZI, CIVIC UNITED FRONT (CUF) na CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).
Pamoja na ukweli kwamba vitimbi vya watawala na chama tawala ndio sababu kuu ya kutosimama imara kwa vyama vya upinzani, vile vilivyoonekana kuwa tishio kwa CCM, lakini pia kuna ukweli kwamba vyama vyenyewe vinaudhaifu mkubwa sana ambao ndio upenyo uliotumika kuvisambaratisha kwa urahisi.
Kukosekana umoja, Viongozi kuwa wabinafsi, kung'ang'ania madaraka, kukosekana ajenda zenye kuwaunga watu ktk misingi ya chama na mengineyo kibao! ni miongoni mwa sababu, sababu zilizopelekea kurubuniwa kirahisi, kugombanishwa na kununuliwa! na kisha kujifia kibudu. UROHO WA MADARAKA/UCHOYO NA KUENDEKEZA NJAA!
Kwa sasa hamna tena chama kilichokuwa imara dhidi ya CCM! Vyama vyote vimebaki kuwa Chawa wa CCM.
VIMETEPETA, LABDA ACT WAZALENDO AMBACHO BADO NI KICHANGA. NASEMA LABDA, TUSUBIRI TUONE!
Ni ccm ndio inaamua mijadala ktk kipindi hiki iwe nini kumuhusu nani. Nani ndani ya CCM ndiye tumaini la watu na nani hafai na kwa nini. CCM inaamua hayo! Wapinzani hawana tena ajenda, wamebaki kuparamia paramia matukio, hawana ujasiri tena wa kuanzisha ajenda za kitaifa.
Hawana tena Dira, wapinzani wamebaki kuwa machawa wa makada wa CCM. Watampamba leo Bashiru,
Kesho akizibwa mdomo watabaki kimya wakisubiri tukio jingine.
TANZANIA TUNACHAMA KIMOJA TU KILICHOSIRIASI
VINGINE HIVI NI VIKOBA TU

NINI KIMESABABISHA HALI HIYO?

CCM NDIO MWELEKEO WA NCHI
Hali ya sasa kisiasa ni kipimo tosha kuonesha uhalisia huu, kwamba ccm ndio mwelekeo wa Nchi, Genge lipi ndani CCM likitawala siasa za ndani ya chama basi Nchi itakuwa na mwelekeo huo na hakuna wa kubadili chochote. Makada wa vyama pinzani, wachambuzi wa mambo ya kisiasa, Mitandao ya kijamii na media zote kwa ujumla wote/vyote hivi vimekuwa chawa wa CCM.