Canal hawana ofisi sehemu yoyote hapa Tz na kisimbuzi chao hakijasajiriwa na mamlaka (TCRA) hapa Tz hivyo kinatumika tu kwa kuwa kipo nchi jiran za Rwanda, Burundi na DRC na mawasiliano yake yanafika Tz (wenyewe wataalam wanaita beam kitu kama vile)
Harafu lugha rasmi ya chanel za kisimbuzi hiki ni Kifaransa na hakina option ya kubadili lugha, pia kwa kuwa hakipo Tz (yaani hakijasajiriwa TCRA) malipo yake yapo kwa franca fedha hii inatumika DRC, Burundi na Rwanda hivyo ukitaka kulipia ni mpaka upate connection ya mtu wa nchi hizo kisha umtumie pesa akulipie akiwa huko, hapa kuna shida kidogo ikitokea kifurushi kimekata harafu unaemtumia kukununulia hapatikani at the moment
Ila kwa ujumla kisimbuzi kipo vizuri ukicompare pesa na idadi ya ligi wanazoonesha yaanikwa elfu 40 na kitu unatizama karibu ligi zote kubwa duniani, wakati Dstv kwa elfu 69 hata UEFA champions league huipati