Kisimbuzi gani cha ndani kitarusha matangazo ya Kombe la Dunia la mwaka huu?

Kisimbuzi gani cha ndani kitarusha matangazo ya Kombe la Dunia la mwaka huu?

Nauliza, ni kisimbuzi gani cha ndani ambacho kitarusha kombe la Dunia la mwaka huu?

Miaka ya nyuma tulikuwa tunaona shamrashamra za matangazo kwenye visimbuzi vya ndani mfano Startimes kwamba watarusha, lakini mwaka huu kimya na zimebaki siku kadhaa!

CCM tulishawashauri, Watanzania tunapenda mpira ambapo husahau mambo mengine, hivyo CCM wajitahidi kadri wawezavyo wawasaidie visimbuzi vya ndani (local) au Channel Ten na Channel Ten Plus wanunue haki za kurusha matangazo ya Kombe la Dunia ili wananchi wasipate muda wa kufuatilia mambo ya nchi!

Sasa kama CCM wanaanza kupuuza hadi michezo hasa soka, naona wanajitengenezea bomu, maana kwa sasa kitu pekee kinachowazubaisha Watanzania ni mpira!

CCM toeni hela visimbuzi au chaneli yenu irushe kombe la Dunia hata bure! Msijisahau sana!
Banda umiza mechi 1000 mara 64 ni 64,000/=. NENDA BANDA UMIZA.
 
Ni ujinga kudhani kuwa CCM ndio Kama mzazi wako.

Kombe la dunia mechi zote zitaonesha live kwenye DStv Lipia dish Kwa around 70k na kifurushi Kwa around 54k bei za kizalendo kabisa hizi.

Au la hasha dish la Azam wataonesha baadhi ya matches
Ukinunua dish jipya 79,000 unapewa na kifurushi cha offer cha 56,000/-
 
Back
Top Bottom