Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
- Thread starter
- #41
SURA YA THELATHINI NA TATU: MWISHO WA SAFARI.
Asubuhi tulipoamka tukaanza kazi ya kupakia hazina melini. Ilikuwa si kazi nyepesi maana tulikuwa watu wachache. Wale waasi watatu hatukuwaona tena, lakini tuliweka mtu mmoja kushika zamu, maana wasije wakatushambulia ghafla. Vipande viwili vya dhahabu vilitosha mzigo wa mtu mzima. Mimi kazi yangu ilikuwa kukaa pangoni na kufunga sarafu za dhahabu katika mifuko, tayari kwa kupakiwa melini.
Lo! Sarafu hizo zikikuwa ni za kila namna na kila nchi, na vidole vyangu viliuma sana kwa kuzihesabu kwa sababu zilikuwa nyingi sana. Basi kazi hii ikaendelea kila siku mpaka zikaisha zote.
Siku moja tulipokuwa tukitembea tulisikia sauti za watu wakiimba, na tukajua ni wale waasi watatu wamelewa. Yule John Fedha aliwekwa huru kabisa, akawa anatembea apendavyo, lakini hapana hata mmoja aliyemuamini wala kumpenda. Tukashauriana tuwafanye nini waasi wale, ikawa sote nia moja, kuwaacha kisiwani. Basi tulipokuwa tayari kujipakia tukawawekea akiba ya chakula na baruti kisha tukangoa nanga.
Wale watu watatu walipoona tunaenda zetu wakaja mbio pwani, wakapiga magoti kutusihi tusiwaache kisiwani, lakini wamechelewa! Hatukuweza kujitia katika hatari ya uasi tena.
Basi bwana Livesi akawaita na kuwaeleza tulipowawekea akiba ya chakula na baruti. Lakini wakazidi kusihi kwamba wahurumiwe. Basi meli ikaanza kutoka pwani. Nao walipoona kuwa hatuwachukui wakaelekeza bunduki zao kutupiga. Risasi zikipita juu juu hivyo ilitulazimu tulale chini mpaka tutoke katika upeo wa shabaha zao.
Basi tukaendelea hivi mpaka saa sita, kutazama nyuma nikaona kile kilima kirefu cha kisiwa kiko mbali kabisa, wala kisiwa chenyewe hakionekani. Sasa nikafurahi kuona mwisho wa kisiwa chenye hazina. Na kwa kuwa tulikuwa wachache sana, ilitupasa wote tushirikiane katika kazi kwa bidii sana. Tukaelekeza meli yetu kwenda kusini ya Amerika. Huko tulikusudia kupata mabaharia wengine wa kutusaidia. Tulipofika ilikuwa jioni, nikifurahi mno tulipoegesha meli bandarini, tuliona watu, tukaona watu weusi wa nchi zile, nikajua sasa hatari ya safari yetu imekwisha. Basi bwana Livesi na bwana Treloni wakashuka pwani, wakanichukuwa na mimi pamoja nao. Tukatembea pwani na kuzungumza na watu wa huko. Tuliporudi ilikuwa ni usiku, na mara tulipopanda melini Ben Gun akatujia na akasema kuwa John Fedha ametoroka na kuwa yeye alimsaidia kutoroka. Basi sisi hatukumlaumu, maana kusema kweli tulifurahi kuwa ametoroka kwa kuwa yeye alituletea kisirani katika safari yetu. Basi tukapata mabaharia wengine kutusaidia. Tukafanya safari njema kabisa, mpaka tukafika mji wa Uingereza, Bristol.
Tulipofika tukapata habari kuwa ile meli ya pili ndiyo kwanza inajitayarisha kusafiri.
Kweli ulevi na shetani umewamaliza wengine. Lakini hatukupata kisirani kama wale walioimba. 'Na mtu mmoja tu ndiye aliyesalia katika sabini na tano waliotoka.'
Sote tulipata mali nyingi tulipogawana ile hazina. Nahodha Smollet akaacha kazi yake ya kusafiri na kukaa raha mustarehe. Gray akaendelea na kazi yake na sasa yeye ni nahodha wa meli kubwa nzuri. Ben Gun alipata mali nyingi sana lakini katika muda wa siku kumi zilikwisha zote! Akaja kuomba. Tukamweka kuwa mlinzi wa nyumba yetu naye akaridhika. Hatukusikia tena habari za John Fedha, nadhani anaishi raha mustarehe.
Bunduki na fedha zingine tuliacha kulekule kisiwani, na labda ziko huko hata leo, wala nami sina nia ya kusafiri tena kwenda kuzichukua. Hata sasa nikilala naota safari na kisiwa, na pengine nasikia mawimbi yakipigapiga mchangani, na pengine nasikia sauti ya kasuku yule, Kapteni Flinti akilia, "vipande vya dhahabu! Vipande vya dhahabu!"
Mwisho.