Kisu kimegonga mfupa, views kwa wasanii zimepungua sana baada ya mabando kupanda bei

Kisu kimegonga mfupa, views kwa wasanii zimepungua sana baada ya mabando kupanda bei

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Sote tunajua katika ukanda wa Afrika, Nchi yetu ndio ilikuwa na mabando ya bei rahisi kuliko nchi yoyote hapa afrika (sub saharan)

Hii iligeuka kuwa silaha kwa tasnia yetu ya muziki wa bongo flava katika sura ya bara la Afrika, Ilikuwa rahisi sana msaga sumu kupata views milioni kuliko msanii wa Afrika kusini, kenya, Ghana, Zambia, n.k kupata hata robo ya hizo views.

Views zilikuwa ni silaha yetu, ziifanya hata watu wa mataifa mengine kuanza kutufatilia,

hata kwenye tuzo za kimataifa hizo views zilikuwa na uzito wake.

Ukija pia kwenye platform za kuskiliza miziki kupitia Boomplay na audiomac nako pia tulikuwa tunakmbiza maana internet ilikuwa bei rahisi.

Ila sasa tangu wikki iliyopita kiukeweli kumekuwa na mabadiliko sana huko youtube

Tukianza na youtube, hali ni mbaya, HataLavalava aliekuwa havumi sana ilikuwa kawaida kupata views laki 4 ndani ya siku lakini hadi sasa ana views kupata views 174K na hizi huenda nyingi ni za mashabiki namba 2 wa bono flava kutoka Kenya

1635075906310.png


Maua sama nae ngoma yake ipo trending number 1, tulizoea ngoma kishika usukani basi kwenye siku ya 4 itakuwa na views walaki laki 7 ila hadi sasa ni views laki 2 tu nazo si ajabu zikiwa nyingi kutoka kenya

1635075871149.png


Malkia zuchu nae naona upepo umemwendea ndivyo sivyo, video ina wiki ila ni views laki 7 tu, kiukweli zuchu ilibidi hapa awe na views hata milioni na laki 7, hapa napo wakenya wamehusika sana.

1635077509421.png


Kiufupi tutarajie anguko, Mabando kwa sasa mtu anaingia youtube kwa machale sana, i heri aingiziwe video kwenye simu yake huko vibandani.

Kwa kipindi hiki mashabiki wa kenya huenda watajaza views zaidi kuliko watanzania

Kwa sasa nadhani wa nigeria wamefurahia sana hili swala.

Huenda kabla mwaka haujaisha mabando yatapandishwa tena na huu utakuwa msumari wamoto kwenye upande wa youtube views.
 
Hawa majamaa si naskia ni ma superstars huwa hawategemei fans wa hapa bongo imekuwaje views ziwe hivyo?
 
Ungejipa muda kwanza uone.

Kwanza Bongo fleva iki-hit bongo, imehit na Kenya. Kwahiyo kwa nchi mbili 1M views ni chache.

Pili, Unaongelea Harmonize wakati unaweka wimbo wa kwenye Akaunti ya mtu mwingine.
 
Hawa majamaa si naskia ni ma superstars huwa hawategemei fans wa hapa bongo imekuwaje views ziwe hivyo?
Mziki wetu wa bongo hapa fans wengi ni wa bongo na kenya, kwa sasa nadhani ni wakenya wengi wana view hizo video huku watanzania wakiwa wanaingia youtube kwa machale
 
mziki wetu wa bongo hapa fans wengi ni wa bongo na kenya, kwa sasa nadhani ni wakenya wengi wana view hizo video huku watanzania wakiwa wanaingia youtube kwa machale
Kwa hiyo kumbe bongo fleva bado wanaendelea na hiyo tabia ya kutudanganya mi niliodhani wameacha
 
Hata diamond asilimia 60 ya watu wanaotazama video zake ni wakenya
 
Kufa kufaana.

Watupigie kelele mabando yashushwe.
 
Yaani bando langu niache kwenda nchini TWITTER kufuatilia bunge la wananchi la MARIA SPACES eti nikasikilize ushubwada wao nyimbo hazina ubunifu wala content 🤣🤣 nimelogwa...!!!
 
Back
Top Bottom