Kisukari kimenitenda, sasa uume wangu ndembendembe

Tukundane

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2012
Posts
11,993
Reaction score
9,212
Mwaka 1995 nikiwa mkoani Kagera tumbo lilianza kujaa gesi na kunguruma sana likiambatana na kuharisha. Niliweza kutumia dawa mbalimbali za hosptali ambazo sizikumbuki kwa vile ni muda murefu umepita.Dawa hizo zilinisaidia sana mpaka nikasahau kama nilikuwa na tatizo hilo.Wakati huo wote sikuweza kupata tatizo lolote la uume.Baada ya miaka 10 hivi kupita nilibadilisha mazingira nikahamia mkoa mwingine ambao unabaridi kali kuliko mkoa wa Kagera.Hapo ndipo tumbo liliibuka upya likarudi kama lilivyo kuwa hapo awali.Nimetumia dawa mbalimbali za hosptali tumbo linatulia baada ya muda mfupi linatibuka tena.Kutokana na dalili nilizokuwa ninazieleza kwa daktari aliamuwa kunipima vidonda vya tumbo na kunikuta navyo.Niliandikiwa dawa ya vidonda vya tumbo ninapo zitumia dawa hizo ninapata nafuu lakini baada ya muda fulani vinatibuka tena sehemu ya Chembe ya moyo.Nikiwa ninatafakari namna ya kumaliza tatizo la vidonda vya tumbo. lilijitokeza tatizo lingine la kukosa nguvu za kiume kiasi ambacho nilianza kulalamikiwa na mke wangu kuwa nimesha anza kutoka nje ya ndoa.kwa vile nijuwa kuwa ninatuhumiwa tuhuma ambazo nilikuwa sina ilibidi nitumie mfumo dume ambao ulinisaidia kuweka mambo sawa.Zaidi ya kukosa nguvu za kiume uume ulianza kusinyaa na kuingia ndani utafikiri panya anataka kutoka kwenye shimo sasa anachungulia ilikujuwa usalama wake ukoje kabla ya kutoka nje.kwa sasa nguvu zimeisha kabisa hata kile kidogo nilichokuwa nacho kimenyang'anywa nina miaka 3 sijafanya tendo la ndoa ninatamani lakini sisimamishi mke wangu namuona kama mama mkwe.Badae miguu ilianza kufa ganzi,vidonda vikaanza kujitokeza vidole vya miguuni,vidole vya mikononi vikaanzakujikunja,nikawa ninapata kiu mara kwa mara na kunywa maji sana na kukojoa sana,mate yakaanza kukauka mdomoni kitu kilicho kuja kunishitua sana macho yaliishiwa nguvu kabisa kidogo yapofuke.Ndipo nilipoamuwa kwenda hosptali na kugunduliwa kuwa na kisukari ambacho kilionyesha kuwa na kiwango cha 24 baada ya kuanza kutumia dawa kikaanza kushuka kwa kiwango cha 17,13,11 kwa sasa kinacheza kati ya 12 mpaka 4-5.wakati wote huo kisukari kipande kisipande kiwe kati hali ya baba tafuta watoto ina kuwa ni kwa heri baba wa Taifa.Samahani kwa kuwachosha.
 

pole sana mkuu!
 
Pole sana Mkuu. Fanya mazoezi kila mara, kutembea n.k. Pia kula mboga za majani kwa wingi na matunda, punguza kula vyakula vya nafaka, hasa vile vilivyokobolewa. Jaribu sana kupunguza uzito, kama una kitambi ujaribu kukipunguza. Zaidi ya yote punguza mawazo kwani ugonjwa wa kisukari huenda sambaba na ugonjwa wa shinikizo la damu.
 
Pole sana mkuu.Usikate tamaa nafikiri hapa kuna wataalamu watakupa ushauri mzuri.
 
Fuata masharti unayopewa na daktari kuhusu ugonjwa wa kisukari jogoo aweza kuwika!!
 

Ni kweli leo nimepima Bp iko 150 kwa 100 kisukari bado sijapata jibu.
 
Pole sana mkuu! That is typical diabetes mellitus type two (DM-II)! ...and it have already gone far to the extent that what you are experiencing now are the complications of DM-II. The key issue now is to control your blood sugar by having your medications on time, watching your food and regular check up. I advise you to attend a near-by diabetic clinic and see a diabetic specialist. Most of the regional hospitals have diabetic clinics but if not then it is important for you to make sure you are seeing one referral/consultant hospitals.
 
Pole sana Mkuu,Mungu ni Mwema kila wakati
kuna wataalam hapa wengi nadhani utapona

Mkuu Mzizi Mkavu,Dr Riwa na wengine wote
ambao wanaujuzi pia wameshauguza na kutoa
ushauri tafadhali njoo haraka kwa msaada.
 
wewe ulikuwa na vidonda vya tumbo, ukapata shida ya uume! sasa kwa miaka hiyo mitatu uliyoukuwa hukutani na mkeo, hata kama ulikuwa unafanya ubabe, ilikuwa inakudisturb sana kwa kujua au kutokujua na ikakupelekea kupata diabete. Jaribu herbals za wasabato(sorry kwa kuwaita hivyo) ila, dawa hizo zimesaidia sana watu wengi. Kisha muombe Mungu, jitahidi kuwa na furaha, kumbuka ' happiness is choice not aresult', itakusiadia pia kuwa fine.
 
Dah pole sana mkuu,nadhani tunapata fundisho kwamba miili yetu tusilee
tufanye body exercise frequently inasaidia sana kupunguza fat contents mwilini
Unakuta mtu amekaa kwenye kiti since morning to evening 5days a week,akitoka hapo
hapo job anapita samaki samaki kupata bia mbili tatu na nyama choma akitoka anaenda kulala,same sh.it next day...tuwe na habit ya kuifanyisha mazoezi miili yetu.
Thanks
**NIGGA**
 
Pole sana Mungu yu pamoja na ww, usiache kuomba na ufate ushauri wa daktari..! Get well soon

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
pole..acha kuwaza mambo ya wanawake
pigania uhai wako kwa sasa
kunywa mafuta ya ubuyu nasikia yanasaidia sana
 

Hili nalo neno.
 
mmh! inatia woga, haya magonjwa ya dunia ya leo, MUNGU atakusaidia kaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…