Tukundane
JF-Expert Member
- Apr 17, 2012
- 11,993
- 9,212
Mwaka 1995 nikiwa mkoani Kagera tumbo lilianza kujaa gesi na kunguruma sana likiambatana na kuharisha. Niliweza kutumia dawa mbalimbali za hosptali ambazo sizikumbuki kwa vile ni muda murefu umepita.Dawa hizo zilinisaidia sana mpaka nikasahau kama nilikuwa na tatizo hilo.Wakati huo wote sikuweza kupata tatizo lolote la uume.Baada ya miaka 10 hivi kupita nilibadilisha mazingira nikahamia mkoa mwingine ambao unabaridi kali kuliko mkoa wa Kagera.Hapo ndipo tumbo liliibuka upya likarudi kama lilivyo kuwa hapo awali.Nimetumia dawa mbalimbali za hosptali tumbo linatulia baada ya muda mfupi linatibuka tena.Kutokana na dalili nilizokuwa ninazieleza kwa daktari aliamuwa kunipima vidonda vya tumbo na kunikuta navyo.Niliandikiwa dawa ya vidonda vya tumbo ninapo zitumia dawa hizo ninapata nafuu lakini baada ya muda fulani vinatibuka tena sehemu ya Chembe ya moyo.Nikiwa ninatafakari namna ya kumaliza tatizo la vidonda vya tumbo. lilijitokeza tatizo lingine la kukosa nguvu za kiume kiasi ambacho nilianza kulalamikiwa na mke wangu kuwa nimesha anza kutoka nje ya ndoa.kwa vile nijuwa kuwa ninatuhumiwa tuhuma ambazo nilikuwa sina ilibidi nitumie mfumo dume ambao ulinisaidia kuweka mambo sawa.Zaidi ya kukosa nguvu za kiume uume ulianza kusinyaa na kuingia ndani utafikiri panya anataka kutoka kwenye shimo sasa anachungulia ilikujuwa usalama wake ukoje kabla ya kutoka nje.kwa sasa nguvu zimeisha kabisa hata kile kidogo nilichokuwa nacho kimenyang'anywa nina miaka 3 sijafanya tendo la ndoa ninatamani lakini sisimamishi mke wangu namuona kama mama mkwe.Badae miguu ilianza kufa ganzi,vidonda vikaanza kujitokeza vidole vya miguuni,vidole vya mikononi vikaanzakujikunja,nikawa ninapata kiu mara kwa mara na kunywa maji sana na kukojoa sana,mate yakaanza kukauka mdomoni kitu kilicho kuja kunishitua sana macho yaliishiwa nguvu kabisa kidogo yapofuke.Ndipo nilipoamuwa kwenda hosptali na kugunduliwa kuwa na kisukari ambacho kilionyesha kuwa na kiwango cha 24 baada ya kuanza kutumia dawa kikaanza kushuka kwa kiwango cha 17,13,11 kwa sasa kinacheza kati ya 12 mpaka 4-5.wakati wote huo kisukari kipande kisipande kiwe kati hali ya baba tafuta watoto ina kuwa ni kwa heri baba wa Taifa.Samahani kwa kuwachosha.