Pole sana mkuu,tuachie wenye meno tuendelee kutafuna!
Mkuu ninashukuru endeleeni kutafuna pia muangalie na ninyi musije mukatafunwa.
Mkuu acha kunitisha,siku yangu ya kufa anaijua mungu peke yake!jamani utani mwingine sio mzuri, kumbuka mwenzio hajaomba hata wewe waweza kutana na balaa zaidi ya hilo kama si kisukari chukulia mfano ukapata ajali ukapooza kiunoni kwenda chini, mtu akikuambia hayo maneno utafurahi, MUNGU AKUSAMEHE HUJUI UNENALO
Kuna dada mmoja anaitwa Rahabu na dawa ya fiterawa. Mtafute. Nimemsikia kwenye redio.
Pole sana Mkuu. Fanya mazoezi kila mara, kutembea n.k. Pia kula mboga za majani kwa wingi na matunda, punguza kula vyakula vya nafaka, hasa vile vilivyokobolewa. Jaribu sana kupunguza uzito, kama una kitambi ujaribu kukipunguza. Zaidi ya yote punguza mawazo kwani ugonjwa wa kisukari huenda sambaba na ugonjwa wa shinikizo la damu.

Mkuu Dingswayo, hizo ulizozitaja ni hatua mahususi za kumfanya awe na nguvu za kiume au ni za ku-control sukari au ni ya kusaidia vyote pamoja?
Ni kweli leo nimepima Bp iko 150 kwa 100 kisukari bado sijapata jibu.