Kisukari kimenitenda, sasa uume wangu ndembendembe

Kisukari kimenitenda, sasa uume wangu ndembendembe

Mungu wetu hajafa bado ni Mungu yuleyule mponyaji ATAKUPONYA Tukundane

Ninashukuru sana pamoja na kuwategemea watalaam kwa sababu nao wamewekwa na mungu ili watusaidie lakini siyo kwamba wanaweza kila kitu.ndiyo maana hata wao wanasema kuwa wao wanatibu lakini mponyaji ni mungu.nami naungana nawe pia kuwa ninaomba mungu aliye hai aweze kuingilia kati na kuweza kuniponya.
 
Last edited by a moderator:
Hakkuna ugonjwa YESU AWEZI KUUPONYA MPENDWA MUNGU ANABADILI MAJINA YA TASA WA MIAKA KADHA NAKUITWA BABA FUDENGE NINI KISUKARI;NNI KUSIMAMISHA UUME BANA;;;B4SNYTHING TAFUTA KANISA LA KILOKOLE OMBA MTU AKUONGOZE TOBA;AKUONGOZE SALA YA REHEMA UREHEMIWE NA UKOIO NA KIZAZI KILICHOPITA;SISEM KWA UBAYA UNAWEZA OMBA SANA KUMBE SRC N BABU YAKO MZAA BIBI AMA BABU;SO KAMA N LAANA LAZIMA IOMBWE REHEMA KWAKUWA AWAKO HAI MUNGU AWASAMEHE IWEZEKUNYANYUKA;SIJUI UNAMIAKA MINGAP UKIULIZA PENGINE WAO ILIGOMA KUSIMAMA MIAKA 26;BADA YA HAPO NENDA HOSPT FWATA MASHARTI NASEMA HIVI SIKUHIZI VIJANA WANATESEKA NA KISUKARI SABABU ZA DHAMBI ZA WAZAZI WAO AMA BABU ZAO JIANGALIE FANYA MAPPING YA FAMMILLY UNIAMBIE OTHERWISE MUNGU WA MBINGUNI AKUSIMMAISHE NANII YAKO IN JESUS NAME NIMESOMA MWANZO TO UFNUO SIJAONA HAKO KAGONJWA HIZO NGUVU ZA GIZA;ANGALIA KWENU AKUNA WALIOTENGENA SHETAN ANAWEZA KOSA SABABU NA MKEO AKAITUMIA KAMA KIGEZO VUNJA KEMEA FYEKA KABISA HZO LAANAA ALL THE BEST

Nina umri wa mika 40.Kuhusu swala la toba sina ubishi nalo kwani haliko kwa ajili ya uponyaji wa mwili tu.kwani hata mungu huwezi kumuona bila kufanya hivyo.Kwenye ukoo wetu sijamuona mtu mwenye matatizo kama yangu wala sijasikia kama kuna mtu yeyote alishawahi kuwa na maradhi kama hayo.Isipokuwa mke wangu anavidonda vya tumbo mdogo wa mke wangu ana vidonda vya tumbo baba mkwe anavyo binti yangu wa miaka 15 anavyo.Kuhusu swala la mke wangu kuwa huenda anaweza kuvunja ndoa kutokana na matatizo niliyo nayo.katika hilo ninamshukuru mungu kwa kunipa mke asiyetetereka vinginevyo kipindi cha miaka 3 ambacho hatujashirikiana naye angekuwa ametimka pamoja na kwamba kipindi fulani nililazimika kutumia mfumo dume ili kuweka mambo sawa.Isipokuwa nitatumia pia ushauri wa mudau mmoja alie nishauri hapo awali kuwa inatakiwa siku ninapo kwenda kwa daktari niende na mke wangu ili naye akasikilize maelezo yanayo tolewa na daktari.
 
Ni vyote. Maana sukari katika damu ikipungua, hata shinikizo la damu linapungua na mwili unarudia hali yake kutegemea na jinsi ulivyoathirika.

Na vipi vyakula vya kumsaidia hilo tatizo lingine la nguvu za kiume alilolitaja?
 
Pole sana mkuu. Nakushauri kuepukana na stress na kuzingatia kula vizuri sana na kufuata ushauri wa kidaktari. Pia waweza kutembelea health kuna products muhimu kwa ajili ya matatizo ya sukari, vidonda vya tumbo na kupungua nguvu za kiume.
 
Pole sana mkuu. Nakushauri kuepukana na stress na kuzingatia kula vizuri sana na kufuata ushauri wa kidaktari. Pia waweza kutembelea health kuna products muhimu kwa ajili ya matatizo ya sukari, vidonda vya tumbo na kupungua nguvu za kiume.

Nashukuru mkuu lakini health inapatikana wapi?.
 
Aisee! Pole sana mkuu. Kwa kweli hali yako imenisikitisha sana. Tafadhali, usikate tama. Endelea kufuata masharti ya Daktari, Mungu atakuafu na hayo matatizo.
 
Aisee! Pole sana mkuu. Kwa kweli hali yako imenisikitisha sana. Tafadhali, usikate tama. Endelea kufuata masharti ya Daktari, Mungu atakuafu na hayo matatizo.

Asante kwa ushauri wako.
 
Pole sana mkuu, hiyo ni mitihani ambayo mwanadamu anaweza kupitia. Usije ukalichukulia jambo hili kama ni laana na hivyo kukupelekea kukata tamaa. Mungu yupo naamini yeye ndiye mwenye uwezo wa kukuponya.

Zingatia sana ushauri unaopewa na madaktari usijaribu kukata tamaa , najua unasikia maumivu makali ila jipe imani kuwa kuna siku utapona.

Yesu alikuja kwa ajili ya kuupoonya ulimwengu mwamini yeye.
Mungu akupe nguvu
 
Pole sana mkuu, hiyo ni mitihani ambayo mwanadamu anaweza kupitia. Usije ukalichukulia jambo hili kama ni laana na hivyo kukupelekea kukata tamaa. Mungu yupo naamini yeye ndiye mwenye uwezo wa kukuponya.

Zingatia sana ushauri unaopewa na madaktari usijaribu kukata tamaa , najua unasikia maumivu makali ila jipe imani kuwa kuna siku utapona.

Yesu alikuja kwa ajili ya kuupoonya ulimwengu mwamini yeye.
Mungu akupe nguvu

Asante sana na iwe kama ulivyoniombea.
 
Mwaka 1995 nikiwa mkoani Kagera tumbo lilianza kujaa gesi na kunguruma sana likiambatana na kuharisha. Niliweza kutumia dawa mbalimbali za hosptali ambazo sizikumbuki kwa vile ni muda murefu umepita.Dawa hizo zilinisaidia sana mpaka nikasahau kama nilikuwa na tatizo hilo.Wakati huo wote sikuweza kupata tatizo lolote la uume.Baada ya miaka 10 hivi kupita nilibadilisha mazingira nikahamia mkoa mwingine ambao unabaridi kali kuliko mkoa wa Kagera.Hapo ndipo tumbo liliibuka upya likarudi kama lilivyo kuwa hapo awali.Nimetumia dawa mbalimbali za hosptali tumbo linatulia baada ya muda mfupi linatibuka tena.Kutokana na dalili nilizokuwa ninazieleza kwa daktari aliamuwa kunipima vidonda vya tumbo na kunikuta navyo.Niliandikiwa dawa ya vidonda vya tumbo ninapo zitumia dawa hizo ninapata nafuu lakini baada ya muda fulani vinatibuka tena sehemu ya Chembe ya moyo.Nikiwa ninatafakari namna ya kumaliza tatizo la vidonda vya tumbo. lilijitokeza tatizo lingine la kukosa nguvu za kiume kiasi ambacho nilianza kulalamikiwa na mke wangu kuwa nimesha anza kutoka nje ya ndoa.kwa vile nijuwa kuwa ninatuhumiwa tuhuma ambazo nilikuwa sina ilibidi nitumie mfumo dume ambao ulinisaidia kuweka mambo sawa.Zaidi ya kukosa nguvu za kiume uume ulianza kusinyaa na kuingia ndani utafikiri panya anataka kutoka kwenye shimo sasa anachungulia ilikujuwa usalama wake ukoje kabla ya kutoka nje.kwa sasa nguvu zimeisha kabisa hata kile kidogo nilichokuwa nacho kimenyang'anywa nina miaka 3 sijafanya tendo la ndoa ninatamani lakini sisimamishi mke wangu namuona kama mama mkwe.Badae miguu ilianza kufa ganzi,vidonda vikaanza kujitokeza vidole vya miguuni,vidole vya mikononi vikaanzakujikunja,nikawa ninapata kiu mara kwa mara na kunywa maji sana na kukojoa sana,mate yakaanza kukauka mdomoni kitu kilicho kuja kunishitua sana macho yaliishiwa nguvu kabisa kidogo yapofuke.Ndipo nilipoamuwa kwenda hosptali na kugunduliwa kuwa na kisukari ambacho kilionyesha kuwa na kiwango cha 24 baada ya kuanza kutumia dawa kikaanza kushuka kwa kiwango cha 17,13,11 kwa sasa kinacheza kati ya 12 mpaka 4-5.wakati wote huo kisukari kipande kisipande kiwe kati hali ya baba tafuta watoto ina kuwa ni kwa heri baba wa Taifa.Samahani kwa kuwachosha.


Mkuu Tukundane

Pole kwa yanayokusibu. Sipendi kukuchosha sana na maneno mengi yasomsaada wowote kwani hakuna kipywa juu ya sababu na madhara ya kisukari kama wadau mbalimbali walivyochangia.

Kama upo serious na AFYA yako, chukua HATUA kwa kunipigia ili tuongee zaidi.

0713 366 473

KARIBU.

FEEL LOVE NOW!
 
Ndugu Zangu

Tusijidanganye. Kwanza kabisa tuangalie. Nini chanzo cha kisukari?

Wataalam wanauita "ugonjwa" huu kuwa "lifestyle disease", yaani ugonjwa unaoambatana na jinsi mtu unavyoishi. Hilo la kwanza. Je, ni kwa namna gani unavyoishi mpaka upate kisukari? Swali zuri. Sitatumia lugha ngumu. Mtu unapoishi maisha ya kubahatisha, yaani bila ya kuwa na mwongozo thabiti wa kumcha Mungu (haijalishi wewe dini gani), ni lazima kwamba suala la maadili kwako wewe litakuwa halipo. Hebu ona ndugu yetu huyu jinsi anavyotuhumiwa na mkewe kuwa anatoka nje ya ndoa, wakati sio kweli. Hayuko peke yake. Jiulizeni: Ni kwa nini mkewe afikie hatua hiyo? Mmenipata?

Unapokosa maadili, hutajali umemdhulumu nani, umemwibia nani, umetoa au umepokea rushwa kutoka kwa nani, umezini na nani, n.k. Pengine hata biashara ya kusafirisha wahamiaji haramu, sembuse dawa za kulevya, zote zako. Mpo?

Sasa hapo tayari umeshakuwa mtumwa wa Shetani. Amekukaba. Hakuachii. Hata ufurukute namna gani. Unapogutuka, tayari una matatizo. Uliacha kwenda kwenye nyumba za ibada kumwabudu Mungu miaka mingi. Hapo ulipokuwa una matatizo ya kiafya, wala hukujua tatizo ni nini, na wala hukuwa na nguvu na ujasiri wa kulijua tatizo na kulipatia tatizo. Shetani asingekubali kukuruhusu upone. Akakujaza hofu, ukaogopa, hukufanya lolote.

Binadam wamesahau kwamba Mungu aliwaumba ili waje KUITAWALA DUNIA NA KILA KILICHOMO NDANI YAKE, wala si KUTAWALIWA NA DUNIA. Binadam wana changamoto kuu tatu: Matamanio ya kimwili; matamanio ya malimwengu; na majaribu, hila na fitina za Shetani. Kama ukikubali kutawaliwa na matamanio ya mwili, basi utakuwa mlevi wa kila mwili wako utakachotamani. Kama ukikubali matamanio ya malimwengu, utataka kumiliki vitu ambavyo huwezi kuvimiliki, hatimaye utafanya kila hila uvimiliki, ikiwemo wizi, dhulma, rushwa, biashara haramu, n.k. Hapo, wakati Shetani akiwa anakumiliki, utamuacha Mungu, utamsahau, utamtupa. Utaacha kumuabudu, huku ukijipa imani kwamba: Nitamkumbuka Mungu nikiwa mzee. Sasa ni kijana. Acha nitafune maisha. Je, una ahadi na Mungu kwamba atakuacha uishi hadi maisha ya uzeeni? Kama Mungu anamchukua mtoto mchanga aliye tumboni kwa mama yake, sembuse wewe?

Sasa turejee kwenye hili tatizo la huyu ndugu yetu. Tunamsaidiaje?

Ninachosema nina uhakika nacho, kwa kuwa hata mimi ninasumbuliwa na kisukari, lakini sasa nimeamua kupona, na nimeshamwambia Yesu kwamba: Sasa basi maradhi haya. Sina haja nayo tena, nawe Bwana wajua hilo.

Jambo la kwanza unalopaswa kulifanya ni kukabidhi kila ulicho nacho; maisha yako, akili yako, nafsi yako, mali zako zote, kwa Mungu. Sijui wewe ni dini gani, lakini sasa unapaswa kubadilika. Umrudie Mungu.

Baada ya hapo, ukishaongea na Mungu, umeshaomba na kutubu dhambi zako, umesamehewa, sasa anza maongezi rasmi na Mungu. Mwambie Mungu akusimamie maradhi yako hayo, upone. Na usifikirie kwamba ati utaenda hospitali na kupona.

Hivi nyie mliona wapi mtu akapona kisukari hospitali? Unaambiwa uende "diabetes clinic". Pale unaenda kufanya nini zaidi ya kukubali kwamba wewe ni mgonjwa wa kisukari. Hebu tujiulize. Kisukari ni nini? Kisukari kinasababishwa na nini?

Ninavyojua mimi, kutokana na experience yangu ya muda mrefu, kisukari kinasababishwa na jambo moja tu: Msongo wa mawazo (depression and stress) unaosababishwa na misukosuko ya maisha. Wakati binadam anapopatwa na misukosuko huishia kuwa na mawazo mengi, ambayo husababisha ubongo wake uache kufanya kazi unaotakiwa kufanya. Unaanza kufanya kazi ya ziada ya "kuprocess" mawazo. Badala ya ubongo kusimamia viungo vya mwanadam, sasa unaanza kusimamia mawazo, ambayo hayaishi. Hatimaye viungo vinachoka na kuanza kuathirika, kimoja baada ya kimoja. Viungo vinavyosababisha mzunguko wa damu kuwa sahihi - adrenal gland - vinaacha kufanya kazi, kwa kuwa havipokei maelekezo kutoka kwenye tezi zilizopo kwenye ubongo, yaani Thyroid Gland, Parathyroid Gland na Piniary Gland. Hawa ndio mamesenja wakuu wanaopeleka taarifa kwa viungo; ini wewe safisha damu, ondoa sumu; figo, nawe safisha damu; kongosho (pancreas), hebu toa insulin ili hiyo sukari ipate kutembea vizuri mwilini isigandamane na kumwumiza mtu wetu; spleen, ambayo hutengeneza damu, ndiyo nayo ina mchango mkubwa sana. Ikitengeneza damu ambayo ni nzito, haitatembea vizuri mwilini, hapo matatizo ya blood pressure yanaanza kutokana na mishipa ya damu ama kusinyaa au kuzibwa na damu zinazogandamana (blood clots).

Haya ni maelekezo ya kitaalam zaidi, ambayo yanahitaji ufafanuzi wa kina. Nipo tayari kutoa ushauri.

Suala ni kwamba, HAKUNA DAWA YA HOSPITALI inayoweza kumtibia mtu mpaka akapona kisukari. Lakini tiba asilia zina mfumo tofauti. Haziendi kwenye "kudhibiti" tatizo; zinaenda kwenye kutibu tatizo, yaani, kwa upande wa kisukari, zinaenda kutibia kongosho pamoja na viungo vyote vingine ambavyo vinasababisha hali hiyo kuwapo, ili viungo hivyo vifanye kazi yake. Huu ndio mtazamo wa tiba asilia, ambayo ilitumika na mababu zetu tangu hata kuja kwa mkoloni.

Mkoloni alikuja, akafanya utafiti wa dawa zetu, akaziona zinafaa, akaenda kuzichakachua, kwa kuwa tuyari tulikuwa na kasumba ya kumwona Mzungu kuwa mtu bora zaidi yetu, basi tukaamini kila kitokacho kwake ni cha heri. Kumbe yeye lengo lake ni kuja kufanya biashara kwenye miili yetu.

Kuna dawa za kuwatibia watu malaria, wakapona kabisa, wasiugue tena. Kuna dawa za kuwatibia watu matatizo ya moyo, presha, kisukari, ini, n.k., wakapona kabisa, wasiugue tena. Kuna dawa hata za kuwatibia watu HIV, wakapona kabisa, lakini tunaambiwa - TENA NA WAZUNGU HAO HAO - kwamba hakuna dawa. Wao wanatetea soko lao, kwani sisi tukipona, wao wataenda wapi? Sasa hivi suala la HIV limekuwa mradi mkubwa sana, wa mabilioni ya dola. Wako watabibu wa tiba asilia, wenye dawa, lakini kila wakienda kusajiliwa pale kitengo cha Tiba Asilia, Muhimbili, wanawekewa ngumu ILE MBAYA! Wanapewa gharama kubwa kubwa wasiweze kumudu huo uchunguzi wa dawa zao, na huku watu wanaangamia.

Watu kukatwa miguu kwenye hospitali, au vidole vya miguuni, kwa sababu ya kisukari, imekuwa jambo la kawaida kama kwenda sokoni Kariakoo kununua mahitaji. Hospitali nyingi - we nenda kafanye uchunguzi, usisikilize maneno yangu - zimegeuka kuwa chinja chinja. Hivi ukimkata mtu mguu kwa sababu ya kisukari, unamuongezea au unampunguzia mawazo? Unamuongezea au unampunguzia mawazo?

Jamani, tiba ipo, hata mimi nimeanza kuitumia, na nitapona. Suala la nguvu za kiume nimeanza kuziona, zinarejea, taratibu. Suala kubwa ni kuwa na IMANI, kumkabidhi Mungu maisha yako, uone kama atakugeuka. Mwamini Mungu. Atakusimamia.

Pole. Ila ninashukuru hujafikia hatua ya kuugua hadi kukatwa vidole kama mimi. Nilishakatwa kidole kimoja, waliposema nakatwa vingine viwili, vya mguu wa kushoto nikasema: Sasa basi. Nilishamkabidhi Yesu suala hili. Tutaenda kumwona Dr. Mkweli.

Je, Dr. Mkweli ni nani? Ukitaka kumjua, niandikie ujumbe binafsi, nitakueleza.

Tumsifu Yesu Kristu!
 
Back
Top Bottom