Kisungura hapana

Kisungura hapana

Paul dybala

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2023
Posts
524
Reaction score
2,097
Inawezekana kisungura ikawa ni gongo Ile wanatuficha tu ....Jana nimekikataa kisungura nikamix na energy kwanza nilikosa usingizi nilihangaika Sana kitandani wakti mda huo tumbo linauma sana...

Naishauri serikali waondoe kisungura,cuca na double kick kwa sababu baada ya miaka 25 vijana watakuwa na matatizo ya Figo.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
POLISI mkoani Morogoro inawashilia watu wanne kwa tuhuma za kuendesha kiwanda Bubu cha kutengeneza na kusambaza bidhaa bandia ya pombe kali aina ya Smart Gin katika mtaa wa Tushikamane kata ya Lukobe ,Manispaa ya Morogoro.

Watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na chupa zilizojazwa 2,544 aina ya pombe hiyo, chupa tupu 2,988 ,chupa za Konyaji zilizojazwa 65, chupa tupu mbalimbali za konyaji zikiwa ndani ya mifuko minne ya salfeti, boxi moja, madumu lita 20 yaliyojazwa spiriti na mengine yenye mchanganyiko wa spiriti na maji .

Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Alex Mkama amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kufanyika kwa oparesheni na misako mbalimbali mwishoni wa Desemba mwaka huu.

Mkama amesema katika opereshani hiyo, polisi walifanikiwa kuwakamata Ramadhani Mdoe ( 30) mkazi wa Msamvu, Manispaa ya Morogoro na wenzake watatu kwa tuhuma za kukutwa wakitengeneza na kusambaza bidhaa feki ya pombe kali aina ya Smart Gin
 
Pombe na vinywaji feki ni vingi sana kwa sasa, zinafyatuliwa copy za vinywaji vingi mamlaka husika imelala na wanaopata madhara zaidi n watumiaji wa mwisho.
 
Naishauri serikali waondoe kisungura,cuca na double kick kwa sababu baada ya miaka 25 vijana watakuwa na matatizo ya Figo.
Hongera kwa kulitambua hii, mimi nawe tuwe chachu ya mabadiliko kwa vijana wengine, wanao jiangamiza kwa matumizi kupita kiasi ya hivi vinywaji.
 
Back
Top Bottom