POLISI mkoani Morogoro inawashilia watu wanne kwa tuhuma za kuendesha kiwanda Bubu cha kutengeneza na kusambaza bidhaa bandia ya pombe kali aina ya Smart Gin katika mtaa wa Tushikamane kata ya Lukobe ,Manispaa ya Morogoro.
Watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na chupa zilizojazwa 2,544 aina ya pombe hiyo, chupa tupu 2,988 ,chupa za Konyaji zilizojazwa 65, chupa tupu mbalimbali za konyaji zikiwa ndani ya mifuko minne ya salfeti, boxi moja, madumu lita 20 yaliyojazwa spiriti na mengine yenye mchanganyiko wa spiriti na maji .
Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Alex Mkama amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kufanyika kwa oparesheni na misako mbalimbali mwishoni wa Desemba mwaka huu.
Mkama amesema katika opereshani hiyo, polisi walifanikiwa kuwakamata Ramadhani Mdoe ( 30) mkazi wa Msamvu, Manispaa ya Morogoro na wenzake watatu kwa tuhuma za kukutwa wakitengeneza na kusambaza bidhaa feki ya pombe kali aina ya Smart Gin