Kisutu: Maafisa wa EU, UN na Mabalozi wa Marekani, Sweden na Ujerumani wahudhuria Kesi ya Ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe

Kisutu: Maafisa wa EU, UN na Mabalozi wa Marekani, Sweden na Ujerumani wahudhuria Kesi ya Ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe

Ha
Wewe ni mee or kee maana nakushangaa hujitambui.

Hivi kwa mtu mwenye akili zake anaweza kumtenganisha mbowe na serikali?

Mnaingizwa cha kike mnakubsri kicha mnasahau matatizo mliyokuwa nayo
Hayo ni maoni na mtazamo wako,pia inaonyesha wewe ni mbaguzi,me au ke inaingiaje hapa. Zaidi hizo ni propaganda uchwara Bila shaka za mwanakijani mmoja.
 
31 August 2021
Mahakama Kuu
Divisheni Maalum ya Makosa Uhujumu Uchumi na Rushwa

Dar es Salaam, Tanzania

Wakili Msomi Peter Kibatala - Aikumbusha Mahakama maalum haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya ugaidi, Jaji ahairisha kesi mpaka kesho


Video courtesy of Mubashara Studio.

Upande wa utetezi wasema Divisheni Maalum ya Mahamaka Kuu ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa haina mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi ya ugaidi. Jopo la upande wa utetetezi likiongozwa na Peter Kibatala wamuomba jaji wa divisheni hiyo maalum ya Mahakama Kuu kuwaachia huru watuhumiwa wa ugaidi Freeman Mbowe na wenzake kutokana na kwamba kisheria divisheni hiyo haijapewa mamlaka kisheria kushughulika na kesi ya ugaidi .

Upande wa serikali umesema kuwa Mahakama Kuu Maalum Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa ina mamlaka kisheria hivyo kesi hiyo iendelee kusikilizwa ktk Divisheni hiyo ya Mahakama Kuu.

Katika suala hilo mbele ya Mahakama Maalum ya Uhujumu Uchumi na Rushwa walikuwepo wawakilishi wa toka balozi mbalimbali ikiwemo Marekani na Uingereza, Asasi za Kisheria na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa.

Jaji wa Divisheni Maalum ya Mahakama Kuu amehairisha kesi mpaka kesho tarehe 1 September 2021 baada ya kusikia hoja za upande wa utetezi na ule wa upande wa serikali ili kujiridhisha kama Divisheni ya Mahakama Kuu ina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kisheria au la.

Kesi hii imefikishwa divisheni hii maalum ya Mahakama Kuu baada ya hatua ya kutajwa (committal) kukamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu ambayo pia ipo jijini Dar es Salaam.
Committal - a hearing where magistrates work out if there is enough evidence of a serious crime to justify a trial by jury
 
Matendo tu ya wafuasi wa Mbowe ni ushahidi tosha kuwa jamaa alikuwa anwafundisha uovu na ujambazi dhidi ya Serikali.
Fanya utafiti mdogo tu kwa wale wote wanao Mshabikia Mbowe utabaini kuwa; wengi wao ni watu wana matendo maovu sana,
wengi wao ni watu wanao shabikia ama kuhamasisha uvunjifu wa amani.
wengi wao wamekaa kishari shari,ugomvi,ubishi na kutoa lugha za matusi.
wamekaa kikatili katili, wapenda vurugu, wanao penda kushabikia mambo ya kikatili kama vile matukio ya mauaji, mfano hivi karibuni ktk tukio la mauaji ya Askari wafuasi wa Mbowe walifurahiansana.n.k.
Huyu jamaa ni Gaidi aliye jificha kwenye chama cha siasa hivyo ni lazima ashughulikiwe na sheria bila huruma.
Eti! wanahamasisha mabalozi waje kwa wingi Mahalamani ili kuwatisha Majaji waogope!! maarifa madogo kweli, yaani wanatapa tapa tu.
 
Hivyo ndivyo ilivyokuwa leo Mahakamani, ambapo Wadau wa Maendeleo wa Tanzania kutoka kwenye Taasisi za Kimataifa wameshiriki kesi hiyo ya Ugaidi kwa lengo la kujua kinachoendelea, Maofisa hao wengi wao wamefika ili kujiridhisha na mwenendo wa kesi hiyo.

Ugaidi katika nchi ni jambo baya linaloweza kuwatisha wawekezaji , hivyo ilikuwa ni lazima wadau wa maendeleo kuhudhuria kesi hiyo ili kupima kiwango cha ugaidi kwa lengo la kulinda wawekezaji kutoka kwenye nchi zao, maana ni hatari kuwekeza kwenye nchi yenye Ugaidi.

hii nchi kuna laana flani, hawa jamaa wa kijani kuna damu zinacchuruzika mikononi mwao mpaka kizazi cha 4, siwataji majina ila wanajijua.
 
Hii ni ishara ya mbowe kutumiwa kufanya Ugaidi
umenena Mkuu.
hivyo viongozi wetu na haswa vyombo vya ulinzi na usalama havina budi kuwa makini sana.
kuna wafadhili wa vurugu wapo nyuma ya huyu Gaidi, hayupo peke yake.
bora serikali imembana mapema alitaka kuingiza nchi kwenye machafuko.
 
Jaji wa Divisheni Maalum ya Mahakama Kuu amehairisha kesi mpaka kesho tarehe 1 September 2021 baada ya kusikia hoja za upande wa utetezi na ule wa upande wa serikali ili kujiridhisha kama Divisheni ya Mahakama Kuu ina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kisheria au la.


01 September 2021
Dar es Salaam, Tanzania

Mahakama yasema kesi ya ugaidi ya Mbowe kuendelea ktk Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi​




Jaji mmoja wa mahakama kuu mjini Dar es Salaam Elinaza Luvanda amesema leo kuwa kesi ya ugaidi inayomkabili kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe inaweza kuendelea.

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, maaarufu kama mahakama ya Mafisadi, imetupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, la kwamba mahakama hiyo haina Mamlaka ya kusikiliza kesi yenye mashtaka ya Ugaidi.
Uamuzi huo umetolewa leo, Septemba Mosi, 2020 na Jaji Elinaza Luvanda, baada ya kupitia hoja za pande zote mbili.

Jaji Luvanda amesema Mahakama yake ina mamlaka ya kusikiliza Mashauri ya ugaidi na kwamba pingamizi lililowasilishwa na upande wa utetezi halina mashiko na hakubaliani nalo.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo, leo Septemba Mosi, 2021 majira ya saa mbili asubuhi ili kusikiliza majibu ya pingamizi hilo walilokuwa wameliweka.

Jana Agosti 31, 2021 Mbowe na wenzake waliwasilisha pingamizi mahakamani hapo wakipinga mahakama hiyo kuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi yao kwa mashtaka ya ugaidi na kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia Ugaidi kesi yao inapaswa kusikilizwa na Mahakama Kuu ya Kawaida na si hiyo ambayo ni Divisheni Maalum.

Baada ya washtakiwa hao kuwasilisha pingamizi hilo, Serikali imepinga hoja hizo ikidai kuwa kwa mujibu wa marekebisho ya Sheria mbalimbali namba 3 ya Mwaka 2016 Makosa yaliyoko kwenye Sheria ya Ugaidi yaliwekwa kwenye Sheria ya Uhujumu Uchumi na kwamba kwa hali hiyo Mahakama hiyo ya Ufisadi ina mamlaka ya kusikiliza mashtaka yao. (Ingia ktk box hapa chini kufahamu hiyo Mahakama maalum)

Tanzania (2016)​

Tanzania’s Economic, Corruption and Organised Crime Court was established by the 2016 Economic and Organised Crime Control Act. Source : Anti-corruption court legislation for 27 countries
Kutokana na hoja hizo, Luvanda anayesikiliza shauri hilo, alipanga kutoa uamuzi leo.

Hata hivyo, leo kabla ya kuanza kwa shauli hilo ulinzi umeimarishwa katika mahakama hiyo kuanzia getini hadi ndani ya viunga vya mahakama.

Utaratibu wa kuingia katika mahakama hiyo kwa leo, kila anayeingia lango Kuu la Mahakama hiyo, lazima aonyeshe kitambulisho na awe amevaa barakoa.

Hata hivyo ni watu watachache ndio wameruhusiwa kuingia katika ukumbi wa mahakama kwa ajili ya kusikiliza shauri hilo, huku wengi wao wakisalia katika viwanja vya mahakama hiyo kutokana na tahadhari ya ugonjwa wa Uvico -19.

Mawakili wa utetezi wamesema awali kuwa Freeman Mbowe na wenziwe wanakabiliwa na mashtaka yafuatayo:
Mashitaka wanayokabiliwa ni kupanga kumshambulia kiongozi, kutoa Tshs. 600,000 kufadhili ulipuaji wa vituo vya mafuta na mikutano ya hadhara na kukata miti kuitandika barabarani kuvuia magari kupita.
conspiring to attack a public official, and of giving 600,000 Tanzanian shillings ($260/220 euros) towards blowing up petrol stations and public gatherings and cutting down trees to block roads.
 

01 September 2021​

Dar es Salaam, Tanzania

Tanzania Court Dismisses Objections To Opposition Leader's Trial​


AFP - Agence France Presse
September 1, 2021

The terrorism case against the leader of Tanzania's main opposition party can go ahead as planned, a high court judge in Dar es Salaam said Wednesday, dismissing objections by his party.

Chadema party chairman Freeman Mbowe and his supporters have described the charges as a politically-motivated effort to crush dissent, and accused police of torturing him in custody.

His lawyers had argued that the high court's Corruption and Economic Crimes Division where he appeared had no powers to hear the case, which was previously being handled by a magistrate's court.

But on Wednesday judge Elinaza Luvanda said that "this court has the jurisdiction to hear terrorism cases and therefore I don't agree with the objection made by defendants."

The hearing took place under tight security, with some representatives from foreign embassies and Chadema's senior leaders in attendance, but many journalists were banned from entering the courtroom by police.

Mbowe has been behind bars since July 21 when he was arrested along with a number of other senior Chadema officials in a night-time police raid hours before they were to hold a public forum to demand constitutional reform.

The 59-year-old has been charged with terrorism financing and conspiracy in a case that has sparked concerns about democracy and the rule of law under President Samia Suluhu Hassan.

On Monday, Mbowe had appeared in court to pursue a case against top legal officials, claiming his constitutional rights had been violated during his arrest and when he was charged.

His defence team says he was held without charge for five days and then charged without his lawyer being present.

The opposition has denounced the arrests as a throwback to the oppressive rule of Tanzania's late leader John Magufuli who died suddenly in March.

There had been hope Hassan would bring about a new era of democracy after the increasingly autocratic rule of Magufuli, nicknamed the "Bulldozer" for his uncompromising style.

But Chadema leaders say the arrests reflect a deepening slide into "dictatorship".
Prosecutors say the allegations against Mbowe do not relate to the constitutional reform conference Chadema had planned to hold in the port city of Mwanza in July, but to alleged offences last year in another part of Tanzania.


Chadema has said prosecutors accuse Mbowe of conspiring to attack a public official, and of giving 600,000 Tanzanian shillings ($260/220 euros) towards blowing up petrol stations and public gatherings and cutting down trees to block roads.
 
01 September 2021
Mahakama Kuu
Divisheni Maalum ya Makosa Uhujumu Uchumi na Rushwa

Dar es Salaam, Tanzania

Kesi yahairishwa baada ya upande wa utetezi kuwakilisha pingamizi jingine



Jopo la Mawakili wanaowakilisha watuhumiwa wa ugaidi, linaoongozwa na wakili msomi Peter Kibatala wamewakilisha pingamizi jingine dhidi ya jinsi hati ya mashtaka dhidi ya Freeman Mbowe na wenziwe 3 ilivyoandikwa na kuwakilishwa Mahakama Kuu . Jaji wa Mahakama Kuu aahirisha kesi mpaka tarehe 3 September 2021 atapotoa uamuzi na upande wa mashtaka wametakiwa kujibu hoja hiyo ya upande wa watetezi.
 
Mama muachie huyu mtu! Maana anakubalika hayo ya ugaidi yasikusumbue,utatia doa utawala wako.
 
Back
Top Bottom