Kisutu: Mahakama yamhukumu Mfanyabiashara Herbinder Seth Kulipa fidia ya Tsh. 26.9 bilioni

Kisutu: Mahakama yamhukumu Mfanyabiashara Herbinder Seth Kulipa fidia ya Tsh. 26.9 bilioni

Jela si Kuzuri Mkuu hata Yeye 'atakaza' ila 'ataachia' Siku si nyingi. Anajaribu tu Kujitutumua na Kujidhira ila najua Familia pamoja na Mwandamizi Mmoja ( sasa ni Mstaafu ) Serikali ' watampoza ' kwa Ushauri na Kuridhia hatimaye nae Kuachiwa Huru hivi kwa Dhamana kama ' Swahiba ' wake huyu.
Na hasa kwa wazee ni mateso makubwa!😭😭😭
 
Ngoja na Mimi nikaibe bil 300 fidia bil26 daha nitakula bata mpaka kuku akasirike

Leo 16/06/2021 12:45

Dar es Salaam.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu, mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Seth kulipa fidia ya Sh26.9 bilioni baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia Sh309 bilioni kwa njia ya udanganyifu.

Pia, mahakama hiyo imemhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja akitakiwa kutokujihusisha makosa yoyote ya jinai.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amefanikiwa kulipa Sh200 milioni benki na kiasi kinachobakia anatakiwa kukilipa ndani ya mwaka mmoja kuanzia siku ilipotolewa hukumu.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatano Juni 16, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya mshtakiwa huyo kusomewa makubaliano ya kuimaliza kesi hiyo.

"Ni wazi kama wakili Marandu alivyotueleza mahakama kuwa Seth ni mkosaji wa mara ya kwanza na ni wazi umekubali mwenyewe kuingia katika makubaliano na DPP (mkurugenzi wa mashtaka nchini), ni wazi umekubali mwenyewe kulipa Sh26.9 bilioni, hivyo mahakama inakuhukumu kifungo cha nje cha mwaka moja, kutokujihusisha na makosa yoyote ya jinai" amesema Shaidi.

Awali, mawakili wawili wakuu wa Serikali, Marterus Marandu, Renartus Mkude na wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon na Faraja Ngukah, walidai kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa mashtaka yake baada ya kuingia makubaliano na DPP.

=====

15/06/2021
Serikali yaafiki maombi majadiliano na Seth

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mtendaji wa PAP, Harbinder Seth, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wamepitia barua iliyoandikwa na mshtakiwa huyo na kufikia makubaliano kwa kile alichokiomba. Seth aliandika barua hiyo Juni 10, kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), akiomba kukiri mashtaka yake na kupunguziwa adhabu.

Barua hiyo ilijadiliwa kwa siku mbili na upande wa mashtaka na ule wa utetezi na kisha kutolewa mrejesho.

Wakili wa Serikali Mkuu, Marterus Marandu akisaidiana na Ladslaus Komanya jana alitoa maelezo hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili Marandu alitoa maelezo hayo wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya upande wa mashtaka kuwasilisha mrejesho wa kile walichozungumza kati yao na Seth kwa ajili ya kuimaliza kesi hiyo.

“Kesi imekuja kwa ajili ya kutoa mrejesho wa barua iliyoandikwa na mshtakiwa huyu (Seth), niseme barua tumeshazipitia kwa pamoja na tumefikia mahali pa kukubaliana kuhusu kile ambacho mshtakiwa alikuwa anakiomba na baada ya hapo, tumekubaliana kuendelea na shauri hili,” alidai wakili Marandu na kuongeza:

“Kwa muktadha huo, upande wa utetezi kama hawatakuwa na pingamizi, naomba shauri hili lije mahakamani hapa kesho ( Juni 16) kwa ajili ya usikilizwaji,” alidai Marandu.

Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Seth, Melchisedeck Lutema alikubaliana na maelezo ya upande wa mashtaka na kueleza kuwa huo ndio ukweli na ndio msimamo wa pande zote mbili za majadiliano waliyofanya.

Hakimu Shaidi baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hadi Juni 16 itakapoitwa kwa ajili ya usikilizwaji au majadiliano ya kuimaliza kesi.

Hata hivyo, jana Seth alikuwepo mahakamani peke yake, wakati upande wa mashtaka walipowasilisha mrejesho huo.

Itakumbukwa Juni 10, Mahakama hiyo ilikubali upande wa mashtaka kufanya mazungumzo na mshtakiwa huyo ya kuimaliza kesi hiyo. Mahakama hiyo ilirihusu majadiliano hayo baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi mahakamani hapo la kutaka kufanya majadiliano na Seth na kisha kutoa mrejesho wa kile walichozungumza kwa ajili ya kuimaliza kesi.

Mbali na Seth, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ambao hawajaandika barua ya kukiri mashtaka yao kwa DPP ni aliyekuwa Mwanasheria wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Joseph Makandege na Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa kampuni ya IPTL, James Rugemalira.

Katika kesi ya msingi, Seth na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 12 likiwemo la kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
 
DPP Sylvester Mwakitalu leo amemuachia huru mfanyabiashara Herbinder Seth baada ya kukiri makosa na kulipa faini.

Mzee Ruge bado amekomaa, tusubiri tuone nini kinaendelea.

Source: Darmpya Blog
hata mimi ningelipa nimepiga 309 bilioni halafu nalipa 26.9 bilioni
 
hata mimi ningelipa nimepiga 309 bilioni halafu nalipa 26.9 bilioni
Nchi ya watu wajinga hii kuanzia juu hadi chini, eti mwizi anaenda kuleta mzungo wa pesa mitaani kwa kuachiwa, ni vitabu vipi vya uchumi ambavyo vina sema ukitaka kuleta mzunguko wa pesa ni kuiba ? ndio maana Lowasa alisema nchi yetu inahitaji Elimu kuwa kipaumbele chetu, hii nchi inatobanga kila kitu kwa viongozi wetu na wananchi kuwa na uelewa mdogo .
 
Kakiri kapiga bilioni 300

Adhabu bilioni 29

Nchi ya kusadikika

Banana republic
 
Wee Kweli?

Ni mwenzetu hasa , mtanzania mtafutaji na mhangaikaji katika kutafuta kitu kinaitwa pesa , kambi mahali popote lakini nyumbani Iringa Tanzania

Harbinder Seth (Singh) Iringa Tanzania from www.standardmedia.co.ke
2 Jul 2017 — ... the 1990s like business tycoon Harbinder Singh Sethi. Born and raised in Iringa, a small town in Tanzania's ...
Few people received top dollar construction contracts from the Kenyan government in the 1990s like business tycoon Harbinder Singh Sethi.

Born and raised in Iringa, a small town in Tanzania’s Southern Highlands, Sethi arrived in Nairobi in the 1980s.

At that time, the idea of tenderprenuership was still new in Kenya. But for a man who had founded his first company at 19, he knew at an early age that he could make a fortune from lucrative multi-billion shilling construction contracts from government entities.

Sethi quickly understood the Harambee spirit building up in Kenya and would from time to time show up at public functions to give ‘generous donations’. His donations would grab media headlines and endear him to government officials.

But it was not until after Ruaha Concrete Co Ltd, a firm he founded together with his siblings, was caught in scandals that his business activities in Kenya started receiving attention.

A 1997 report by the Auditor General found that Ruaha irregularly received a contract from Kenya Pipeline Company (KPC) to build a 9km access road. Despite this, the construction was still rocked by serious delays, large cost overruns and poor workmanship.

The project cost shot up two and a half times from Sh197 million in February 1995 to over Sh510 million by June 1998, when the road was finally completed. The auditor recommended that Ruaha Concrete be blacklisted and investigated.

READ MORE : How tycoon with dubious Kenyan past got entangled in Tanzania’s mega scam
 
Back
Top Bottom