KISUTU: Yanga kupewa siku 14 kupeleka maombi ya mapitio (Review) ya case iliyofunguliwa na Mzee Magoma

KISUTU: Yanga kupewa siku 14 kupeleka maombi ya mapitio (Review) ya case iliyofunguliwa na Mzee Magoma

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
673
Reaction score
1,318
IMG_5128.jpeg
Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Dar es Salaam, Kisutu, leo tarehe 19 Julai 2024, maombi yaliopelekwa na Bodi ya Wadhamini wa Klabu ya Michezo ya Young Africans (YANGA) kwa ajili ya kuongezewa muda wa kuwasilisha mapitio (Review) ya uamuzi wa Mahakama hiyo katika Kesi ya Kiraia Na. 187 ya 2023 yametolewa uamuzi. Maombi haya yalitokana na madai ya kwamba walikosa haki ya kusikilizwa na kuwepo kwa dosari za kisheria kwenye hukumu iliyotolewa.

Katika maombi haya, yaliyopelekwa chini ya Kifungu cha 14 cha Sheria ya Ukomo wa Muda, Cap 89 R.E 2020, mleta maombi, kupitia hati ya kiapo ya Mkurugenzi wa Sheria wa YANGA, Simon Patrick, alidai kuwa hawakupatiwa nyaraka zozote zinazohusiana na Kesi ya Kiraia Na. 187 ya 2022. Alipata habari za hukumu hiyo kupitia vyombo vya habari mnamo tarehe 16 Julai 2024, ndipo alipochukua hatua za kupata nyaraka za kesi hiyo.

Yanga walidai kuwepo kwa dosari za kisheria zifuatazo katika hukumu ya mwanzo:​
  1. Mahakama hiyo haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo; ni Mahakama Kuu pekee yenye mamlaka ya kushughulikia masuala yanayohusu uhalali wa Bodi ya Wadhamini.​
  2. Wajibu maombi (Kena mzee Magoma) hawakuwa na haki ya kuhoji (Locus standi) shughuli za Yanga.​
  3. Kesi Na. 187 ya 2022 iliwasilishwa kinyume na sheria.​
  4. Waleta maombi (YANGA) walinyimwa haki yao ya msingi ya kusikilizwa.​
Hakimu yeye alijikita zaidi katika hoja ya nne (4) kuhusu Haki ya kusikilizwa na kusema kwamba ni haki ya kikatiba chini ya Ibara ya 13 (6) (a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayosema kuwa haki na wajibu wa mtu yeyote inapokuwa inaamuliwa na Mahakama au chombo kingine, mtu huyo atakuwa na haki ya kusikilizwa na haki ya kukata rufaa au kupata tiba nyingine ya kisheria dhidi ya uamuzi huo.

Mahakama ilizingatia hoja zote zilizotolewa na mleta maombi na ikaona kwamba hoja ya kukosa kusikilizwa ni ya msingi na inatosha kuyapa maombi haya nguvu za kisheria. Mahakama iliamua kuiruhusu YANGA kuwasilisha maombi ya mapitio ndani ya siku 14 kutoka siku ya uamuzi.

Mahakama iliridhika kwamba Yanga hakuonesha uzembe katika kuchukua hatua baada ya kugundua kuwepo kwa hukumu dhidi yao, na hivyo iliona ni vyema kutoa muda wa kuwasilisha maombi ya mapitio ili haki itendeke.​
 
Fatma Abeid Amani Karume kashakana kwamba hauhisi na kesi hii, hivyo kuna walakini wa madai ya awali ya kina Magoma...kwa sababu ya forgery
 
Mpaka sasa hivi viongozi wa yanga na mashabiki zake wanatapa tapa tu hakuna aliyejibu hoja hata mmoja.
 
Fatma Abeid Amani Karume kashakana kwamba hauhisi na kesi hii, hivyo kuna walakini wa madai ya awali ya kina Magoma...kwa sababu ya forgery
Na ww ulitaka aseme tofauti magoma sio chizi.
 
Back
Top Bottom