PreGE2025 Kiswaga amwambia Dr.Dugange wazi "Nitagombea na nimejipanga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Katika harambee hiyo Enokc Kiswaga ambaye ni Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na mzaliwa wa kata hiyo ya Imalinyi amemwambia Mbunge wa Jimbo hilo Festo Dugange kuwa anagombea ubunge wa Jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
-
Kiswaga amesema hasubiri kuoteshwa na wala hajifichi anataka vita ya maneno ikaishie kwenye box la Kura. Pia Bwana Kiswaga amechangia kiasi cha Shilingi Milioni tatu 3,000,000/= katika harambee hiyo.
-
Ikumbukwe Mwaka 2020 Bwana Kiswaga alipata kura 175 katika kura za maoni na kuwa mshindi wa kwanza, akimuacha Gerson Lwenge aliyepata kura 159 na Festo Dugange kura 92 ambapo Dugange aliteuliwa na kuwania ubunge wa Jimbo la Wanging’ombe.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mvutano wa Mafahari hawa wawili umekuwa kivuto kwa wadau wa siasa na maendeleo hasa jimbo la Wanging’ombe wakisubiri nani atakuwa nani ifikapo mwezi October 2025 ?
-
Dkt. Dugange ambaye ni Mbunge wa Jimbo Hilo la Wanging’ombe Kwa sasa amehudhuria Harambee hiyo na kuchangia shilingi milioni tatu na laki tatu (3,300,000/= na Kuwaambia wananchi wa Imalinyi kuwa wawe na fadhila kwamba yeye amefanya kazi kubwa ya kupeleka kituo cha afya kwenye kata hiyo pamoja na kukarabati barabara

Hayo majina mbona ya kisukuma alafu hapo siyo usukuman

Kiswaga na lwenge mbona ni majina ya kwetu mwanza
 
Namjua Enock vizuri sana. Ukisikia watu wenye upepo ni huyu jamaa. Niliwahi kukaa nae nyumba moja pale dar. Akaondoka ikapita kama mwaka hivi, nikaja kusikia akiwa mtangazaji wa radio pambazuko fm ifakara.
Akaondoka. Nikaja kumwona anagombea ubunge 2020 na alishinda kwenye kura za maoni. Kamati kuu ikamtema. Anarudi tena. Atashinda. Na ataingia bungeni.
Nachojua. Hana elimu yoyote zaidi ya darasa la saba. Kama kujua kuongea kiingereza atakuwa kajifunza tu kujua kuongea. Kuandika inaweza ikawa shida pia.

Enock ni mmoja wa watu wanaojua kupambana bila kukata tamaa. Anajua kuishi ndoto zake.
Mwaka juzi nilikutana na jamaa m1 akaniambia eyi jamaa ni mtu wa usalama. Sikushangaa maana kwa jinsi Jiwe alivyokuwa akichukua kuyoka UVCCM na kuwajaza kule sio jambo la kushangaza.
 
Ni Watanzania kwani ubunge ukiwa msukuma hauruhusiwi kugombea Mbeya mzala vip bhana watu unakuta wamejikita vizuri na biashara zao huko dhamana zao zipo huko na si usukumani inabidi watafutie Ubunge huko huko..
 
Usalama gani mtu hajui kuandika wala kusoma?
Namjua Enock vizuri sana. Ukisikia watu wenye upepo ni huyu jamaa. Niliwahi kukaa nae nyumba moja pale dar. Akaondoka ikapita kama mwaka hivi, nikaja kusikia akiwa mtangazaji wa radio pambazuko fm ifakara.
Akaondoka. Nikaja kumwona anagombea ubunge 2020 na alishinda kwenye kura za maoni. Kamati kuu ikamtema. Anarudi tena. Atashinda. Na ataingia bungeni.
Nachojua. Hana elimu yoyote zaidi ya darasa la saba. Kama kujua kuongea kiingereza atakuwa kajifunza tu kujua kuongea. Kuandika inaweza ikawa shida pia.

Enock ni mmoja wa watu wanaojua kupambana bila kukata tamaa. Anajua kuishi ndoto zake.
Mwaka juzi nilikutana na jamaa m1 akaniambia eyi jamaa ni mtu wa usalama. Sikushangaa maana kwa jinsi Jiwe alivyokuwa akichukua kuyoka UVCCM na kuwajaza kule sio jambo la kushangaza.
 
Katika harambee hiyo Enokc Kiswaga ambaye ni Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na mzaliwa wa kata hiyo ya Imalinyi amemwambia Mbunge wa Jimbo hilo Festo Dugange kuwa anagombea ubunge wa Jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
-
Kiswaga amesema hasubiri kuoteshwa na wala hajifichi anataka vita ya maneno ikaishie kwenye box la Kura. Pia Bwana Kiswaga amechangia kiasi cha Shilingi Milioni tatu 3,000,000/= katika harambee hiyo.
-
Ikumbukwe Mwaka 2020 Bwana Kiswaga alipata kura 175 katika kura za maoni na kuwa mshindi wa kwanza, akimuacha Gerson Lwenge aliyepata kura 159 na Festo Dugange kura 92 ambapo Dugange aliteuliwa na kuwania ubunge wa Jimbo la Wanging’ombe.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mvutano wa Mafahari hawa wawili umekuwa kivuto kwa wadau wa siasa na maendeleo hasa jimbo la Wanging’ombe wakisubiri nani atakuwa nani ifikapo mwezi October 2025 ?
-
Dkt. Dugange ambaye ni Mbunge wa Jimbo Hilo la Wanging’ombe Kwa sasa amehudhuria Harambee hiyo na kuchangia shilingi milioni tatu na laki tatu (3,300,000/= na Kuwaambia wananchi wa Imalinyi kuwa wawe na fadhila kwamba yeye amefanya kazi kubwa ya kupeleka kituo cha afya kwenye kata hiyo pamoja na kukarabati barabara

no reforms no election
 
Back
Top Bottom