Kiswahili cha bbc baada ya Zuhura Yunus & Salim Kikeke kuondoka

Kwa anaye kielewa anijuze. Wakenya wanaharibu sana lugha yetu. Kurasa za mitandao ya kijamii ya bbc imegubikwa na Kishwahili kibaya sana(kisicho fasaha). Ili nalo likatazamwe!
BAKITA INABIDI WAWANDIKIE BARUA KALI YA ONYO BBC KAMA WANASHINDWA KUWAAJIRI WAJUVI WA KISWAHILI WASIITUMIE LUGHA HIYO KWENYE MATANGAZO YAKE,WAKIGOMA BBC IPIGWE BAN KUSIKIKATANZANIA NZIMA
 
Umewahi kufatilia channel ya Azam inaitwa Azam One, kipindi kinaitwa Magazine.
Sawa tufanye wana makosa hayo,nchi zenye lugha yao hiyo kama UK tumeikataza isilikemee hilo?

Sisi wenye lugha yetu ya kiswahili hatutaki lugha yetu iendelee kukosewa,kama wao wanaona ni sawa lugha yao ya kiingereza iendelee kuharibiwa ni wao.
 
Kwa anaye kielewa anijuze. Wakenya wanaharibu sana lugha yetu. Kurasa za mitandao ya kijamii ya bbc imegubikwa na Kishwahili kibaya sana(kisicho fasaha). Ili nalo likatazamwe!
Tanzania haina haki miliki na Kiswahili mzee, kama wanaongea na wanaeleweka hiyo itakuwa ni version ya Kiswahili ya Kenya

Ni kama Kiingereza cha Marekani na Uingereza havifanani, wala Australia
 
Sawa tufanye wana makosa hayo,nchi zenye lugha yao hiyo kama UK tumeikataza isilikemee hilo?

Sisi wenye lugha yetu ya kiswahili hatutaki lugha yetu iendelee kukosewa,kama wao wanaona ni sawa lugha yao ya kiingereza iendelee kuharibiwa ni wao.
Lugha yako ulipewa na nani? Uliinunua wapi? Unaweza kumkataza mtu asitumie lugha kwa kuwa ni "ya kwako"?

Huu ushamba wa kiwango cha juu sana
 
Ukweli mchungu ni kwamba BBC Swahili imekosa mvuto siku hizi. Kuna siku wiki iliyopita walimuhoji Prof flani aelezee kuhusu tetemeko lililotokea Libya hata alivyoelezea ilikua balaa. Wajifunze kwa vipindi vilivyopita vya wabobezi ili waboreshe, wakiona ni majungu waache kufanyia kazi wanaenda kupoteza mvuto sana.
JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…