Kiswahili cha bbc baada ya Zuhura Yunus & Salim Kikeke kuondoka

Kiswahili cha bbc baada ya Zuhura Yunus & Salim Kikeke kuondoka

Kiswahili ni lugha changa bado, bado haijaenea sana. tofauti na Tanzania, inazungumzwa tu ikiwa kwa kukosewa kosewa sababu haifahamiki vizuri,
 
Lugha yako ulipewa na nani? Uliinunua wapi? Unaweza kumkataza mtu asitumie lugha kwa kuwa ni "ya kwako"?

Huu ushamba wa kiwango cha juu sana
Hee,makasiriko ya nini broo,we kama huna chako usifikiri kila nchi haina chake,ni wazi inajulikana worldwide kiswahili asili yake ni Tz,hutaki acha,nyie msio na identity yenu kazi yenu kurukia vya wenzenu halafu mnajifanya vya kwenu,ongeeni kiswahili fasaha sio mkikosolewa na wenye lugha yao mnaona nongwa
 
Kiswahili ni lugha changa bado, bado haijaenea sana. tofauti na Tanzania, inazungumzwa tu ikiwa kwa kukosewa kosewa sababu haifahamiki vizuri,
Inakosewa kosewa na wasio wa lugha hiyo sio waswahili wenyewe

Bakenya bhana,wanatamani kusema kiingereza ni lugha yao,ila wakiwaza kuwa ni ya beberu wanabaki kusonya tu,🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hakuna nchi yenye hati miliki ya Kiswahili ingawa watumiaji wengi zaidi duniani wako Tanzania ambapo imefanywa lugha ya taifa.

Pamoja na yote, Wakenya kama kawaida yao, walipogundua kuna fursa nzito ya Kiswahili duniani, walianza kampeni ya kukieneza (Kuki-champion) kimataifa hususan kuanzia miaka ya 80. Walitoa walimu, wafasiri na kutumia wasanii wao. Huku Tanzania kama kawaida yetu tukiendelea na politiki zetu zisizo na tija hadi leo.

Uliza huko nje, Kiswahili ni lugha ya wapi? Usishangae kusikia Kenya ikitajwa. Mwenyewe ukisikika na Kiswahili unaweza kukisiwa Mkenya kabla hujajieleza kuwa ni Mtanzania, nchi isiyofahamika. Angalau ujipe nasaba ya uZenji (Zanzibar) kidogo utaeleweka.

Kulalamika haisaidii, lazima tuwe serious kufanyia kazi rasilimali zetu muhimu.
 
Nilikua naangalia sana kipindi wapo wakina kikeke,Hilary,zuhura na yule dada mkenya ila sasa sikifatilii kabisa
 
Inakosewa kosewa na wasio wa lugha hiyo sio waswahili wenyewe

Bakenya bhana,wanatamani kusema kiingereza ni lugha yao,ila wakiwaza kuwa ni ya beberu wanabaki kusonya tu,🤣🤣🤣🤣🤣
Lugha kama inazungumzwa eneo kubwa lazima iwe na variations tofauti tofauti, ndio hatua ya kwanza lugha inapoanza kuenea haiwezi kuenea ikiwa vilevile

Mfano Spanish ya Chile haiwezi kufanana na Spanish ya Mexico au Spain
 
Matamshi yatabadilika kulingana na maeneo ila sio msingi wa maneno ya kisarufi,yaani huwezi ita fruit vinginevyo halafu mwenye lugha yake(native speaker)aseme ipo poa
 
Matamshi yatabadilika kulingana na maeneo ila sio msingi wa maneno ya kisarufi,yaani huwezi ita fruit vinginevyo halafu mwenye lugha yake(native speaker)aseme ipo poa
Hivi unajua hata maana ya sarufi? Maana unatoa mfano ambao hata sio wa kisarufi

Ngoja nikujibu sasa kwa huo mfano wako
Kwa British English mafuta ya petroli yanaitwa petrol ila kwa American English yanaitwa Gasoline,
British likizo wanaita Holiday, Marekani wanaita vacation

Tanzania tunaita jogoo, Kenya wanaita jimbi
Tunaita umeme Kenya wanaita stima
 
Back
Top Bottom