Kiswahili cha dealine na addiction

Kiswahili cha dealine na addiction

Bisansaba

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
292
Reaction score
109
Mtu anaweza dhani kuwa maneno deadline na addiction hayana visawe vyake katika lugha ya kiswahili. Unaweza kuta mtu anasema "...hivi deadline ni lini...?" au "....jamaa kesha addict kwenye mapenzi/dawa za kulevya. kumbe angeweza sema hivi ".....hivi makataa ni lini?" au "....jamaa kesha kuwa mraibu wa mapenzi/dawa za kulevya.

Tujifunze kiswahili kina maneno mengi sana ambayo watu hawataki kuyatumia!
 
Nimeipenda hii japo kuna wasomi wetu uchwara wenye mzio na lugha yetu tukuka watakuja na vikwazo kibao
 
unaonekana unajua, we tumwagie ujuzi wako
 
deadline: muda wa mwisho/siku/tarehe ya mwisho/kuwahi muda uliotolewa
addiction: uraibu (buhu?)
 
Safi sana! Elimu nzuri hata 'monitoring' kisawe chake ni kuperemba pia 'database' ni kanzi data
 
duh blaza Bisansaba kweli we noma wale jamaa Kinondoni walikubania bure tu
 
Last edited by a moderator:
Safi sana! Elimu nzuri hata 'monitoring' kisawe chake ni kuperemba pia 'database' ni kanzi data

Hiyo "kuperemba" rafiki angu Diswe huwa akiitumia anamaanisha kungonoka, leo ndo nimejua maana ya neno hilo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom