Kiswahili chatumika misa ya Papa Benedict Roma

Redondo

Member
Joined
Dec 13, 2012
Posts
13
Reaction score
0
Wakuu, kuna misa ya Mwaka Mpya inaendelea sasa hivi Rome na kuonyeshwa live na kituo kimoja cha televisheni kiitwacho EWTN. Misa inaendeshwa kwa lugha ya Kilatini lakini nimefurahi sana kumuona Sista mmoja wa Kiafrika wakati wa maombi akitumia kiswahili fasaha kuwasilisha maombi huku akiombea amani duniani. Lugha nyingine zilizotumika kuwasilisha maombi ni Kitaliano, Kiingereza, na Kihispania.
 
Tz tungelikuwa na mihela walai hii Lugha tungekomaa ingekuwa Lugha ya Africa maana inchi zaidi ya tano wanaongea hii lugha!
leave alone izo international languages kama kifalansa english etc
 
Inafurahisha sana. Baadhi ya wasomi wetu wanakidharau kiswahili lakini kwa kweli ni lugha inayokubalika sana sehemu mbalimbali ulimwenguni. Ngoja ni-search hiyo channel mkuu.
 
Tz tungelikuwa na mihela walai hii Lugha tungekomaa ingekuwa Lugha ya Africa maana inchi zaidi ya tano wanaongea hii lugha!
leave alone izo international languages kama kifalansa english etc
Kiswahili is also an international language, no doubt about it. Umoja wa nchi za Africa (AU) wamekwisha pitisha lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya Afrika. Sema tu sisi waafrika bado tuko katika usingizi mzito wa kasumba ya kikoloni, kwa hiyo inakuwa vigumu sana kukubali maswala flani flani hivi!
 
Mbona serikali ya maccm inashindwa kukitangaza zaidi?
 
safi, hata mie huwa nahudhuriaga ibada kwenye kanisa moja hapa (ibada kwa lugha yakiingereza) sema wahudhuriaji wengi ni wanigeria na wacameruni....ila mara kibao wamekuwa wakiimba nyimbo za kiswahili. Ninapanga kuwauliza wamejifunzia wapi, maana hakuna muafrica mashariki kwenye hiyo kwaya
 
Big up maria.
Changamkia hilo dili la kufundisha kiswahili....
Usilazie damu.
Kuna vitabu vizuri sana nimeviona mtandaoni vinafundisha kiswahili.....
 
Kiswahili hoyeeee
wanaopata fursa ya kukifundisha nje ya nchi changamkieni dili hiyo
pesa nzuri sana mtapata.....usisubiri kuona eti sijui nini????
Changamka...kamata pesa
kiswahili ni dili sana....
Kuna kitabu nimekiona kinaitwa "kiswahili bidhaa adimu" kinaelezea udili wa kiswahili.
Aluta kontinyua wapenda kiswahili.....tajirikeni...ni ajira hiyo
 
Kiswahili hoyeeee
wanaopata fursa ya kukifundisha nje ya nchi changamkieni dili hiyo
pesa nzuri sana mtapata.....usisubiri kuona eti sijui nini????
Changamka...kamata pesa
kiswahili ni dili sana....
Kuna kitabu nimekiona kinaitwa "kiswahili bidhaa adimu" kinaelezea udili wa kiswahili.
Aluta kontinyua wapenda kiswahili.....tajirikeni...ni ajira hiyo
 
Yaani,ni tatizo letu la kutojiamini tunapokuwa pamoja na wageni;tunaona aibu kuwaongelesha Kiswahili pale tunapokuwa tuko katika maongezi binafsi,ya kibiashara.Yaani utashangaa ghafla mtu ame-switch kwenye Kiingereza au lugha nyingine tofauti na Kiswahili;kwa kufanya hivyo hata mgeni anaona haifai kutumia wakati wewe mwenyeji unakidharau!!
Hebu badilikeni,hivi wewe ukienda kwa huyo mgeni kwao unafikiri ndiyo ataongea Kiswahili?Ni mpaka uwe umemfundisha halafu hata kama ukikutana naye kwa mara nyingine atakuwa tayari kutoa ushirikiano katika lugha yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…