Wakuu, kuna misa ya Mwaka Mpya inaendelea sasa hivi Rome na kuonyeshwa live na kituo kimoja cha televisheni kiitwacho EWTN. Misa inaendeshwa kwa lugha ya Kilatini lakini nimefurahi sana kumuona Sista mmoja wa Kiafrika wakati wa maombi akitumia kiswahili fasaha kuwasilisha maombi huku akiombea amani duniani. Lugha nyingine zilizotumika kuwasilisha maombi ni Kitaliano, Kiingereza, na Kihispania.