Kiswahili darasani kingereza kwenye mtihani

Kwetu Kwao

Member
Joined
Jun 7, 2012
Posts
16
Reaction score
3
Ni kawaida ktk shule zetu mwalimu hata wa somo la english aingiapo darasan kuamkiwa "shikamoo mwalimu" naye huitikia "marahaba kaeni chini" na somo la dakika 80/40 litaendeshwa kwa kiswahili na kingereza juu juu, imezoeleka mwalimu awe wa history,geography, civics,math n.k kufundisha kwa lugha ya kiswahili na mwalimu anayeongea english muda wote huchukiwa na wanafunzi wake lakini tuelewa mitihani hujibiwa kwa kingereza. Hivi unategemea mwanafunzi ataandika nn kwny mtihan? anakuwa na kazi ya kuhamisha concept aliyofundishwa na mwalimu kwa kiswahili to kingereza "ifike hatua tutambue kuwa kingereza ni cha waingereza"
 
We mzungu mweusi vp huoni fahari kuzungumza lugha ya kiswahili ambayo n miongon mwa lugha zinazotambulika kimataifa? Hakuna taifa liloendelea kwa kupga teke lugha yake ya asili mf. Uingereza-kiingereza, China-kichina, japan-kijapan, ujerumani-kijerumani, france- french n.k. Nini hatima ya kiswahili kisipothaminiwa na waswahili kitapotea km zlivyopotea lugha maaruf km Kilatini na kigiriki. Badiri mtazamo wako
 
Suala hapa sio lugha wala nini,kichwa cha mtu kina nafasi kubwa katika kujifunza vitu mbalimbali.Nakumbuka wakati tupo shule zetu za msingi ambapo kiswahili ndicho kinatumika katika masomo yote kasoro english bado utakuta mtu hana chochote cha kujaza kwenye mtihani,sasa mtu kama huyu utasema lugha tatizo?Kama kichwa chako kizito, kizito tu,hata ufundishwe kwa kilugha chako!Kwanza english rahisi saaaana,tatizo watanzania hatupendi kujisomea vitabu mbalimbali,MAJITU YANAPENDA KUSOMA MAGAZETI YA UDAKU TU
 
nafikiri hata wewe Kwetu kwao ulifundishwa kwa njia hio. sababu kubwa ni kwamba ukifundishwa kiingereza tu bila kutafsiriwa hautaelewa.
 
Kiingereza ni kigumu sana, yaani kupita Physics, Chemistry na Hesabu.
Hesabu zimeanzia MISRI, Chemistry, hata baba yangu ni mkemia wa miti shamba.
Babu yangu ni mwana fizikia ndio maana anarusha ungo angani.
Kiingereza kilikuja na meli na katu, hakibebeki kwa mtumbwi
 
maybe na hao walimu,kizungu hawakijui vizuri
 
nafikiri hata wewe Kwetu kwao ulifundishwa kwa njia hio. sababu kubwa ni kwamba ukifundishwa kiingereza tu bila kutafsiriwa hautaelewa.

Basi kama kuelewa mpaka utumie kiswahili kwanini tufundishwe kwa kiswahili tu. Kingereza kwa Waingereza bhana
 
bujibuji, wee kiboko nimeipenda comment zako - zimenifurahisha
 
bujibuji, wee kiboko nimeipenda comment zako - zimenifurahisha

jamaa linaongea kiutaniutani lakini ndivyo ukweli ulivyo, babu zetu walikuwa na akili n noumar halafu si tunasema siku hizi kuna makauzu wao walikuwa makauzu zaidi ukileta zako ulikuwa unasondekwa porini kama miez 9 ukitoka adabu mbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…