Kiswahili Kilichovunjika-Jengo la Maliasili na Utalii

Kiswahili Kilichovunjika-Jengo la Maliasili na Utalii

Bobby

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2008
Posts
2,182
Reaction score
1,896
Wengi wetu especially wakazi wa Dar ninahakika mnalifahamu jengo jipya la Wizara ya Maliasili na Utalii lililopo kandokando ya barabara ya Nyerere karibu na traffic lights za Chan'gombe. Kiukweli jengo hili lililopewa jina la Mpingo House ni zuri ila kuna kitu kimoja kinanikera binafsi hasa kwa kuwa ninakiona at least mara mbili kwa siku. Kitu hicho ni kuwa jengo hili kwa mbele limeandikwa hivi:


Wizara ya Maliasili na Utalii Makao Makuu= Ministry of Natural Resources and Tourism Headquarters

Sina shida na upande wa kiingereza ambacho nadhani kiko sahihi. Tatizo langu ni upande wa Kiswahili. Kwa maoni yangu kilichoandikwa hapo si Kiswahili bali ni Kiingereza kilichotumia manano ya Kiswahili. Kama nilimwelewa vizuri mwalimu wangu wa Kiswahili shule ya msingi, upande wa Kiswahili ulipaswa kusomeka hivi " Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii". Vinginevyo hiyo ni direct translation ya Kiingereza kitu ambacho sidhani kama ni sahihi. Naomba wataalamu wa lugha watusaide kwenye hili. Ni kweli huenda likaonekana ni kosa dogo lakini kwanini tukosee hata kama ni kidogo hasa ukizingatia sisi ni wamiliki wa Kiswahili?
 
Naunga mkono hoja......vinginevyo wangeweka mabano au kamstari kabla ya neno Makao Makuu

Wizara ya Maliasili na Utalii (Makao Makuu)

au

Wizara ya Maliasili na Utalii - Makao Makuu
 
No wonder watz tunaiata CENTRAL POLICE STATION kwa kiswahili KITUO CHA KATI CHA POLISI badala ya KIKTUO KIKUU CHA POLISI.......
 
mbona Neno Mpingo silioni hapo? Au ni jina la kimoyomoyo?

Mkuu hayo maneno ya Mpingo House yapo, sema yamejificha kidogo katikati ya maneno ya kiswahili na kiingereza niliyoyaeleza. Of course unahitaji macho yenye uwezo mkubwa wa kuona kama yangu ili uweze kuyaona kwa mbali.
 
Naunga mkono hoja......vinginevyo wangeweka mabano au kamstari kabla ya neno Makao Makuu

Wizara ya Maliasili na Utalii (Makao Makuu)

au

Wizara ya Maliasili na Utalii - Makao Makuu

Babu nimependa ulivyodadavua hapo juu, huu ni ushahidi tosha kwamba enzi zenu hakukuwa na shule za kata.
 
No wonder watz tunaiata CENTRAL POLICE STATION kwa kiswahili KITUO CHA KATI CHA POLISI badala ya KIKTUO KIKUU CHA POLISI.......

Mkuu hili nano neno kwa kweli. Ni kama kwenye hotuba moja ya marehemu Baba wa Taifa (sitaki kumwita Mzee Nyerere na ninachukia kabisa mtu akimwita hivyo) aliwaponda wasomi wetu kwamba wanaongea kiingereza kwa kiswahili. Akatoa mfano wa maneno ya "this leads to" tunavyoyatafsiri kwa kiswahili kwamba "hii inapelekea..." Kwangu mimi huu ni ulimbukeni. Pamoja na mapungufu mengi ya kiswahili ninauhakika kuna maeneo kinaweza kusimama peke yake pasipokuegemea kwenye lugha nyingine na bado kikatoa maana iliyokusudiwa.
 
Back
Top Bottom