Wengi wetu especially wakazi wa Dar ninahakika mnalifahamu jengo jipya la Wizara ya Maliasili na Utalii lililopo kandokando ya barabara ya Nyerere karibu na traffic lights za Chan'gombe. Kiukweli jengo hili lililopewa jina la Mpingo House ni zuri ila kuna kitu kimoja kinanikera binafsi hasa kwa kuwa ninakiona at least mara mbili kwa siku. Kitu hicho ni kuwa jengo hili kwa mbele limeandikwa hivi:
Wizara ya Maliasili na Utalii Makao Makuu= Ministry of Natural Resources and Tourism Headquarters
Sina shida na upande wa kiingereza ambacho nadhani kiko sahihi. Tatizo langu ni upande wa Kiswahili. Kwa maoni yangu kilichoandikwa hapo si Kiswahili bali ni Kiingereza kilichotumia manano ya Kiswahili. Kama nilimwelewa vizuri mwalimu wangu wa Kiswahili shule ya msingi, upande wa Kiswahili ulipaswa kusomeka hivi " Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii". Vinginevyo hiyo ni direct translation ya Kiingereza kitu ambacho sidhani kama ni sahihi. Naomba wataalamu wa lugha watusaide kwenye hili. Ni kweli huenda likaonekana ni kosa dogo lakini kwanini tukosee hata kama ni kidogo hasa ukizingatia sisi ni wamiliki wa Kiswahili?