Kama ni hivyo, basi kuna favourism vilevile ya Ubantu dhidi ya sisi wengine ambao ni Non-Bantus. .. Na hii ni mabaya zaidi. Kiswahili hakina maneno yanayotoka ktk Non-Bantu languages kama Kimasai, Kimang'ati, Kijaluo, Kisandawi, n.k.
Wachawi wajichanganye nw wanaotumia Kiswahili na baadae kuleta kitu au dhana MPYA isiyokuwepo ndani ya Kiswahili. Sifa ya Kiswahili ni kupokea dhana mpya kwa lugha ya mtowa dhana mpya na kuitia ndani ya Kiswahili. Upo mpango maalum unaokubalika kusarifu lugha ya kigeni na kuingizwa kwenye Kiswahili.
Hii sababu ya dhana mpya ndiyo iliyosababisha Kiswahili kiwe na maneno mengi ya Kiarabu. Kama tulivyokwisha juulishwa na wengi kuwa Waarabu walikuwa na wakati mwingi kuleta dhana zao kuliko lugha nyengine ,na hapo zilipoingia lugha nyengine katika jamii inayotumia lugha ya Kiswahilitayari mambo na dhana nyingi za kidunia.
zilikwishatiwa kwenye Kiswahili kupitia Kiarabu. Lugha kama Kiingereza kilpokuja kilpingana na taathira za Kiarabu lakini tayari lugha ya Kiswahili ilishajenga maneno yake kwa kupitia Kiarabu hivyo haikuwa rahisi kuondowa taathira hiyo bila ya kuondowa Kiswahili chenyewe.
Lugha za Kihaya, Kisukuma, Kimasai na nyengine za Tanzania zilikutana na Kiswahili hivi karibuni tu na tayari Kiswahili kiko mbali kwa tabia yake ya kuiba maneno ya lugha nyengine. Kuingizwa kwa maneno mapya huja pale tu panapokuwa na sababu yaani pana dhana mpya na Wamasai, Wasukuma, Wahaya na makabila mengine si wazuri katika kuvumbua vitu vipya vitakavypleta maneno mapya ya kukifanya kiswahili kiyatie ndani ya lugha yao.
Tukubali kuwa Hayo maneno ya Kiarabu yaliyomo yamepitia mfumo wa kawaida wa KIswahili katika kumeza maneno kiasi kwamba hat Waarabu wenyewe wapata tabu kuelewa maneno hayo kuwa ni maneno ya Kiarabu kiasili. Pia tukubali kuwa athari ya maneno ya Kiarabu imekwisha sasa kwa vile wanaoleta dhana mpya sasa ni Wzungu na Wachina hivyo kwa tabia yake Kiswahili kitabeba maneno hayo na tone mifano ya maneno friji, televisheni, kompyuta na mengineyo,ambayo juu ya kuyalazimisha kuitwa jokfu, Runinga, na mengineyo wengi wa waswahili wataendelea kuviita kwa dhana ya muundaji kwani ni tabia ya Kiswahili kupokea dhana mpya kwa nama aliyeileta alivyofanya. Kiswahili si lugha ya kulazimishwa bali ni lugha inayokuwa yenyewe.