Mimi MTZ kabisa kwa taarifa yako. Na hii ni taabu moja uliyo nayo. Badala ya kuulizia ushahidi, unakimbilia kusema "wewe ni Mkenya." Umejikita kwenye "ad hominem" argument, fallacy ambayo inajulikana kabisa. Halafu unataka kujua walionipa utaalamu huko. Sasa nikikutajia wataalamu wa mbali utaanza malalamiko mengine. Lakini soma maandiko ya wataalamu wa Kibongo kabisa kama akina Massamba na utaona hayo. Ushahidi upo wa kiisimu na kiakiolojia. Kama utaona unaweza, basi nitakupa marejeleo ya wataalamu wa kutoka nje ya Bongo pia.