BLackList tz
New Member
- Aug 3, 2022
- 1
- 0
By Erick Mange
Leo nakuja na maada hii nyeti kabisa katika maendeleo na kukua kwa lugha ya kiswahili katika nchi yetu na duniani kwa ujumla.
Mara kadhaa nmekuwa nkijiuliza kwanini tumeamua kutumia kiingereza kama lugha ya kufundishia wakati lugha ya taifa ni kiswahili?
Sipati majibu.. kuna umaana gani wa kuiita lugha ya kiswahili lugha ya taifa?
Tunajifunza ata kwa mataifa mengi duniani wanajitahidi kutumia lugha zao za taifa kama lugha ya kujifunza na kufundishia. Mfano mzuri ni nchi kama china, korea, na mataifa mengine mengi.. ambapo hii inamjengea mwanafunzi uelewa na kujivunia uhalisia wa taifa lake.
Katika taifa letu sahivi mtu ukiwa unajua kuongea kiingereza unaonekana msomi, mwenye akili na unaabudiwa sana. Lakini ni tofauti kabisa na ukiwa unajua kiingereza na kiswahili unababaika unaonekana mjanja sana.
Ni kutokana na jinsi tusivyoipa kipaumbele lugha yetu, Ebu angalia mataifa ya wenzetu mpaka kwenye simu wanatumia lugha zao angalia waingereza, wachina, wakorea, wajapani n.k lakini sisi watanzania tunaendelea kukikandamiz kiswahili wenyewe.
Na ndio maana hata katika mziki wasanii wengi hupenda kutumia na kiingereza ili kuonekana wajuaji zaidi. Point yangu ya msingi ni hii.
Naomba Serikali ilitilie maanani hili suala tena kwa haraka sana maana mara kadhaa hili wazo limekuwa likitolewa na wadau mbalimbali lakini limekua likipotezewa tu. ipitishwe rasmi kuwa Kiswahili ni lugha rasmi ya kujifunzia na kufundishia italeta Mabadiliko chanya na kukuza lugha ya yetu.
NI HAYO TU MACHACHE LAKINI NI JAMBO LA MSINGI

Upvote
2