Mpinzire
JF-Expert Member
- Jan 18, 2013
- 7,503
- 13,463
Kwanza kabisa naomba tutofautishe Lugha na Maarifa! Maarifa unayaweza kuyapata kupitia lugha yoyote na haimaanishi kuwa kujua Kiingereza basi ndiyo kuwa na maarifa.Yaani hapa bongo bhana tuna vipaji vingi sana tena watu wa maana umewahi kufikiria kwanini hatuvumi sana kimataifa na dunia kiujumla.Hii ni kwasababu ya lungha tunayotumia kama Lungha ya taifa umewahi kufikiria labda ENGLISH ingekuwa ndo lugha yetu ya taifa yaani Kwanza tungekuwa na lafuzi nzuri ya kiingereza kuliko mataifa mengi ya kiafrika yanayozungunza English,tena kungekuwa na fursa nyingi kuliko sasa kama umewahi kuchunguza mataifa mengi wanayozungumza kiingereza wazungu huwa Wana antention nayo kuliko Yale yasiyo zungumza lugha hiyo lakin pia hata Yale mataifa yasiyozungumza kiingereza yanapokuja kwenye taifa letu bado unakuta wanaongea kiingereza tena utazani ni waingereza.Tunamsifia mwalimu Kwa kuliungalinisha ili taifa Kwa luga moja lakin Mimi nasema ilikuwa ni Kwa maslahi yake binafsi kwanini hakutumia kiingereza kutuunganisha ,je umewahi kufikiria kwanini wananchi wa taifa hili ni washamba alafu wanauelewa mdogo wa mambo ukiachillia mbali wale waliosoma soma kidogo ni kwasababu hata sources nyingi zinazofungua uelewa wa watu bado zimeandikwa Kwa kiingereza.MI NA HITIMISHA KWA KUSEMA ILIKUWA MISTAKE KUBWA MNO.
1. Africa tumekosa Elimu sahihi ya sayansi:- Nasema hivi kwanini? Lengo kwa kwenda shule ni kupata maarifa ili uje kutatua changamoto zinazoikabili jamii yako. Elimu tunayoipata mashuleni hautufanyi kuwaza kutatua changamoto zinazotukabili hivo tunajikuta tunaishia kukariri ili tujibie mitihani, tufaulu tupate ajira maofisin. Kama ukiulizwa kwanini Tanzania maskini kwa kiswahili na bado ukashindwa kujibu basi ata uulizwe kwa kiingereza bado utashindwa kujibu atakama unakijua kiingereza vizuri sana, ila ukiulizwa kwa kiswahili ukaweza kujibu ila kwa kingereza ukashindwa basi tatizo lilikuwa lugha tu sawa ukaulizwa kwa kichina au kifaransa utashindwa kujibu ila majibu unayo kwa lugha yako mama.
2. Tanzania ianze kufundisha kwa kutumia kiswahili mpaka vyuoni ila Kiingereza libaki kama somo ikiwezekana Kifaransa, Kijeruman na Kichina pia vifundishwe:- Hoja yangu inakuja kwasababu Watanzania Lugha yetu ya mama ni Kiswahili, na kiswahili ndiyo lugha yetu ya kufikiria, yaani unapokuwa unafikiria changamoto zako za kifedha kwa mfano kuwa ukiamka asubuh utaingilia wapi ili upate fedha hutumii kingereza kuwaza ila unatumia kiswahili, bas tungekuwa tuipata elimu ya siyansi na ufundi kwa kutumia kiswahili ambayo ndiyo lugha yetu mama tungewez kutatua changamoto zinazoikabiri jamii yetu.
3. Kumfundisha kwa kutumia kiingereza au kuongea kiingereza kwasana hakutotufanya tuendelee:- msingi wa hoja hii angalia bara zima la Africa, hasa kusini mwa jangwa la Sahara! Matatizo yetu yanafanana japo tunatumia lugha tofauti, kwaiyo ni vema tukajikita kuboresha mitaala ya elimu zetu ili tuweze kujididimiza katika "Uwazi mtupu" (Abstract thinking) hapa tutakuja majibu kuanzia katika jamii zetu na mpaka katika matatizo ya dunia tutashiriki kuyatatua. Inapaswa kujua kuwa kumwambia mtoto the Biology is the study of living organisms, sio kumfundisha kiingereza bali ilo ni somo la Biology tu kama vile unaweza kumfundisha somo la biology kwa kiswahili pia kuwa ni elimu ya viumbe hai.
Mwisho kabisa:- Hakina Taifa lililoendelea kwa kutumia Lugha ya kuazima.
Uingereza kabla ya kuanza kutumia kiingereza ilikuwa inatumia kifaransa, na msingi wa Elimu tuliyonayo duniani sio Uingereza ila Uarabuni na mataifa mengine kama Ugiriki etc hivo wao kwanini hawakutumia kiarabu kufundishia katika mashule yao?