Kiswahili kumbe hakieleweki hata hapo kwa jirani Malawi, tunakikuza kuliko uhalisia, ni ajabu

Kiswahili kumbe hakieleweki hata hapo kwa jirani Malawi, tunakikuza kuliko uhalisia, ni ajabu

Kinazungumzwa Mpakani, hata msumbiji kinazungumzwa Mpakani...ndani hakipo
Yaani nchi ambazo angalau 30% ya wananchi wake wanazungumza Kiswahili ni Tanzania na Kenya tu, wengine hata 5% hawafiki japo ni majirani zetu
Hapana Congo na Burundi unatwanga kuswahili na unaeleweka ukiwa Burundi hata Bujumbura kiswahili wanazungumza
 
Takwimu zimeongopa?

Niliangalia BBC kipindi kilichoonesha wazungu huko Marekani wakiwa darasani wanajifunza Kiswahili.

Kiswahili kimeonekana kwenye Muvi inaitwa Vishwatma.

Kimesikika kwenye Nemesis 2 Nebula.

Kimesikika kwenye wimbo wa Michael Jackson.

Kimesikika kwenye American Pie.

Kimesikika kwenye Primeval.

Kimesikika kwenye Get Out.

Last time I checked Kiswahili ni lugha ya pili kuzungumzwa na watu wengi kwa Afrika lugha Ya kwanza ni kiarabu.
Ni kweli kiswahili kinakua haraka,Marekani kuna wamarekani wengi wanajua kiswahili,hata ukituwa JF Kennedy au Dulles and St Paul usishangae ukasalimiwa kiswahili baada ya kuonesha pasport yako
 
Hata Wajapani wapo wanaozungumza Kiswahili, ila huwezi kusema Kiswahili kimeenea hadi Japan.

Ili kusema lugha fulani imeenea kwenye nchi fulani basi angalau 50% ya wananchi wake wawe wanaizungumza.
Kitendo cha JPM kuongea Kiswahili ila mtu wa kutafsiri akahitajika inaonyesha Malawi Kiswahili hata hawakielewi kwa kukisikia, achilia mbali kukiongea.
Tunapenda kujikuza kama tunavyosema Tanzania inajulikana duniani kote. Hapa ninapoishi ukiongea Tz wanafikiria Tasmania. Ukitaka wakuelewe ongea Kenya hapo wanajua unakotoka. Mimi huwa nauliza unaifahamu kenya, wakisema ndiyo basi unasema sisi ni jirani ila bado hawajui hata hilo jina. Wasomi wa zamani ukiwatajia Nyerere ndo wanakuwa na mwanga kuwa unatoka Africa au Tz. Jamani mnapokuwa nyumbani mkajiaminisha mnafahamika, mnajidanganya. Tanzania haijulikani labda nchi zilizopigania uhuru tu lakini nchi nyingine za Africa yawezekana hawajui hata Tanzania ilipo. We have nothing to be proud of. Kiswahili bado saaana.
 
Mzee Kiswahili hakipimwi kwa kuongelewa sijui Marekani au Ulaya, hao wanajifunza lugha nyingi sana just for curiosity sababu ni wadadisi, Marekani wanajifunza hadi lugha za karne ya 10 ambazo zimepotea siku hizi na wanazitumia hadi kwenye movie, sembeuse Kiswahili..Wanajifunza vilugha vingi sana vidogo sio kuwa wanavihitaji bali ni katika tafiti zao na udadisi

Kiswahili kama kingekuwa kimekuwa kweli watu wangejifunza kwa kuwa wanakihitaji sio kujifunza for the sake of curiosity,

Waafrika wanaotuzunguka ndio watu wa kwanza wanaotakiwa kujua Kiswahili kama kweli Kiswahili kinapanuka, sio watu wa mbali huko ambao hatuna interaction nao
Mbona hata South Africa walimu wa Kiswahili walipewa Shavu Wakenya wakatuwahi usizarau Lugha ya Kiswaz Mkuu
 
Inakuaje kwa kila nchi wakati Tz tu hatuzidi 60M?

Upo sawa?
Hapo sasa, mwenyewe sijamuelewa ndio maana nikamuambia afafanue, Tz tupo milioni kama 56 hivi ila sio wote wanaojua Kiswahili.

Kuna vijiji vya kimasai, usukumani huko Kiswahili ni shida. Kenya ndio usiseme
 
Wewee uliyesoma kwa nini usiseme hizo nchi ambazo Kiswahili kinazungumzwa na kueleweka na hata 30% ya wananchi wake ukitoa tu hapo Kenya?
Mkuu
kwanini una roho mbaya kiasi hicho.
Kwanini unamtaka jamaa akupe mifano ya nchi ambazo hazipo duniani.


Kiswahili kinakuzwa sana kuliko uhalisia.
 
Sasa wewe usiwe boya, 50% ya population ikiwa inajua Kiswahili, basi hata walio kwenye mkutano kwa kuwa ni sample iliyotoka kwenye nchi hiyo hiyo, roughly 50% watakua wanajua Kiswahili, sijui kana unajua hesabu vizuri kuelewa hili

Kanisani mhubiri anaongea Kiingereza kinatafsiriwa Kiswahili sababu majority hawaelewi Kiingereza, wanaolewa English wanakuwa wachache sana ndio maana kunakuwa na mfasiri

Malawo sijasema hawajui Kiswahili eote kabisa, ila wanojua ni wachache mno kiasi kwamba mtu akiongea Kiswahili na taifa la Malawi inabidi kitafsiriwe kwa Kiingereza ndio angalau wabanchi wengi wakuelewe
Umeanza matusi tena mbona ulikua na mada nzuri tu?

Sawa twende hadi utaelewa.

Umesema wengine wanaojua kiswahili watakuepo ikiwa 50% of popn itakua inazungumza lugha husika.

Sasa umejuaje kama wote waliohudhuria hawajui kiswahili?

Ikiwa wapo/ watakuepo wanaojua kiswahili hiki ulichoandika ni sahihi?
 
Muda huu nipo Bujumbura Burundi (Buyenzi) na nawasiliana na wenyeweji wangu na watu wengine kwa kiswahili bila wasiwasi. Kabla ya pasaka nilikuwa Uvira Congo DR, nimewasiliana na wenyeji kwa kiswahili bila wasiwasi. Tatizo lenu mnakurupuka tu kupost msiyoyafahamu!
Majirani zetu wanaozungumza kiswahili kwa ufasaha ukitoa kenya ni 1.Burundi, 2. Congo, 3.Rwanda then zinafata hizo nchi nyingine. Huko Malawi, Zambia, Mozambique na hata Uganda hakujawahi kuwa na wazungumzaji wengi wa kiswahili kwa kiwango cha kumfanya Rais au kiongozi yeyote kuwasiliana na jamii yao kwa lugha hiyo. Acheni umbumbumbu wa kupost bila research.
Sasa wewe kuwasiliana na hao ndugu zako ndio kuwa DRC wanajua Kiswahili kwa 50% ? Unafikiri Congo au Burundi nzima ipo kwa hao ndugu zako?
Wewe ndio mbumbumbu wa mwisho zaidi
 
Sawa! Huko Malawi, Msumbiji, Zambia Kiswahili huzungumzwa hasa mipakani mwa hizo nchi na Tz hasa na wafanyabiashara kutoka huko au raia wenye kukifahamu ila huko kwingine hutumia lugha zao tu.
 
Sasa wewe kuwasiliana na hao ndugu zako ndio kuwa DRC wanajua Kiswahili kwa 50% ? Unafikiri Congo au Burundi nzima ipo kwa hao ndugu zako?
Wewe ndio mbumbumbu wa mwisho zaidi
Nani kakwambia nimekuja kwa ndugu zangu!!? Mbona unakuwa mpubavu kiasi hicho? Inamaana ndugu zangu ndo wanaonihudumia hotelini, wananihudumia sokoni/madukani, wananisafirisha, wananitembeza na kunipa kila huduma!!??? Mpumbavu ni mtu asiyethamini alichonacho.
 
Sasa wewe kuwasiliana na hao ndugu zako ndio kuwa DRC wanajua Kiswahili kwa 50% ? Unafikiri Congo au Burundi nzima ipo kwa hao ndugu zako?
Wewe ndio mbumbumbu wa mwisho zaidi
Bahati mbaya hata jiografia ya Burundi huifahamu. Mpaka nafika Bujumbura nimepita mikoa na wilaya kibao na zote wanazungumza kiswahili.
 
Mbona unachuki na lugha mama ya waafrika. Kiswahili ni kibantu na kiarabu. Afrika inakaliwa na wabantu na waarabu kwa kiasi kikubwa
 
Kwani lugha yao hasa ni ipi
Lugha kubwa na ambayo pia ni lugha ya Taifa ni kichechewa,ila wana kugha zingine ndogo ndogo mfano Notthern region wanazungumza Sana Kitumbuka,maeneo ya Nkata bay wanazungumza kitonga while southern region( Blantyre,Zomba,Sanje,Chikwawa na wilaya nyingine huko anakotoka Rais wa Sasa wilaya ya choyro) wanazungumza lugha yao
 
Ukisikia kwenye vipindi vya Radio na Tv na mijadala mbalimbali jinsi Kiswahili kinavyokuzwa na huku Wakikiponda Kiingereza, utadhani Kiswahili ni lugha moja iliyoenea sana

Ila Kumbe ukienda nchi ambayo tunapakana nayo kabisa, Malawi hapo licha ya kuwa tume interact kwa miaka zaidi ya 55 sasa bado Kiswahili hakieleweki huko, Ushahidi ni hapo TBC, wanaongea English na kilugha chao, Magufuli mwenyewe ilibidi aongee Kiingereza na rais wao jana, na hata leo alipoona kuongea Kiingereza muda mrefu pengine itakuwa changamoto akaongea Kiswahili ilibidi kuwepo na mkalimani ili awatafsirie watu wa Malawi kwa Kiingereza..!

Kiingereza kinapondwa sana kuwa ni lugha ya wakoloni haifai lakini ndio lugha inayotuunganisha Waafrika, yaani sisi Majirani wetu wa karne nyingi hapo Malawi hatuwezi kuwasiliana pasipo Kiingereza, ukienda majirani wengine pia hapo Uganda, Zambia, Rwanda bado hutaeleweka na wengi usipozungumza Kiingereza

So tusijidanganye Kiswahili eti ni lugha kubwa wakati inazungumzwa na nchi moja na nusu tu..! Yaani Tanzania na Kenya, Kenya wanaongea English zaidi kuliko Kiswahili, habari zao na mijadala inaongelewa kwa Kiingereza kuliko Kiswahili, Wakenya kwenye mitandao ya kijamii, Magazeti, Tv n.k wanatumia English kuliko Kiswahili

So Kiswahili kwa sasa ni kama lugha ya Tanzania tu na wala sio Afrika Masahariki achilia mbali Afrika ambako ndio baadhi ya watu wanasema

Tuachane na pride, tujifunze English.. Tukikuza Kiswahili chetu ni muhimu japo sijaona ushaishi wa Tanzania Kiuchumi au kiutamaduni utakaofanya Waafrika wengine wengi wakihitaji na kujifunza...

Sana sana wanaojifunza wanajifunza sio kwa kuwa wanakihitaji bali wanajifunza tu kwa udadisi kama amabavyo wazungu wanavyoweza kujifunza Ki Yoruba au Kichewa au Ki Twa

Kiswahili is overrated kabisa!

Ningekua Nyerere ningesema English iwe national language halafu lugha za makabila kila kabila libaki nazo zisipotezwe!

English ni bora maana ndio defacto world's language!

Ningefanya kama alivyofanya Lee Kuan Yew hapo Singapore!

Makabila yabaki,kila kabila liwe strong na mila na origins zake..Watu wakae na makabila yao kwa imani zao na mila zao bila kuingiliwa.

Sio Kiswahili kimekuja kimeua makabila mengine yote,watu hawana identity tena,wanabaki kua moderate loosers,hawapendi kwao walipotoka maana mizizi ya origins zao Nyerere aliziua tayari,wamebaki Watanzania wanotangatanga tu hawana origin of belonging!

International hatutoboi maana hatujui English na hapa nchini kwa kiswahili bado tunatangatanga hatuna origins tena!

Kwanini Wakenya ni wazalendo kupita maelezo kuhusu Kenya zaidi ya Watanzania na Tanzania yao?

Sababu ni kua,Wakenya wana ancentral lands zao zilizopo kenya na wapo emotionally attached nazo,Tanzania hakuna kabila hata moja Nyerere aliyaua for the sake of Kiswahili,watu wapo juu juu tu hawana belonging bora liende!

Hakuna ukabila maana mwanadamu mheshimu na kabila/origin yake,sio unaliua,unajenga taifa lenye mizizi feki!
 
Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa wakazi wa huko ni vululuvululu kila mtu ana lugha yake hakuna lugha kamili ya taifa
Lugha kubwa na ambayo pia ni lugha ya Taifa ni kichechewa,ila wana kugha zingine ndogo ndogo mfano Notthern region wanazungumza Sana Kitumbuka,maeneo ya Nkata bay wanazungumza kitonga while southern region( Blantyre,Zomba,Sanje,Chikwawa na wilaya nyingine huko anakotoka Rais wa Sasa wilaya ya choyro) wanazungumza lugha yao
 
K
Umeanza matusi tena mbona ulikua na mada nzuri tu?

Sawa twende hadi utaelewa.

Umesema wengine wanaojua kiswahili watakuepo ikiwa 50% of popn itakua inazungumza lugha husika.

Sasa umejuaje kama wote waliohudhuria hawajui kiswahili?

Ikiwa wapo/ watakuepo wanaojua kiswahili hiki ulichoandika ni sahihi?
Kama hii issue imefanyika lilongwe,basi wanaojua kiswahili Lilongwe ni watanzania wachache walioko hapo,wakenya,na wakongo wengi walioko kwenye kambi za wakimbizi wilaya Dowa
 
Kinazungumzwa Mpakani, hata msumbiji kinazungumzwa Mpakani...ndani hakipo
Yaani nchi ambazo angalau 30% ya wananchi wake wanazungumza Kiswahili ni Tanzania na Kenya tu, wengine hata 5% hawafiki japo ni majirani zetu
DRC na Republic of Central Africa wanazungumza kiswahili
 
Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa wakazi wa huko ni vululuvululu kila mtu ana lugha yake hakuna lugha kamili ya taifa
Mkuu nimesema lugha ya taifa ni kichechewa ila si wamalawi wote wanaojua vizuri kichechewa hasa hasa Northen Region kwa maana ya wilaya za mzimba,Rumphi,Nkata bay,Karonga,Chitipa na Khothakoto.Huko wanazumza Sana kitumbuka kuliko kichechewa
 
Back
Top Bottom