Kiswahili: Methali, Vitendawili, nahau, Misemo n.k

Wanajopo mwanangu kaniletea vitendawili hivi nimeshindwa.
1 Kiangazi chote nalala, yakija masika nakesha
2 Inaonekana mara mbili ktk dk 1, na mara moja tu kwa mwaka


2) Herufi 'K'. kwavip, dakika ina 'k' mbili na neno mwaka lina 'k' moja
 
Asante sana mkuu. Umenikumbusha zamani wakati nikiwa shule ya msingi palikuwepo na kijitabu kinaitwa Swahili Sayings From Zanzibar kilichokuwa na methali za kutosha ambazo tulikuwa tukizikariri tu pasipo kufahamu maana yake. Kitabu hiki sijawahi kukiona tena madukani ijapo nina imani kuna baadhi ya watunzaji wazuri bado wanancho.
 
Wakuu naomba mnidadavulia methali hii: PEMA USIJAPO PEMA UKIPEMA SI PEMA TENA.
 
Wakuu kuna methali moja inaitwa MGAAGA NA MPWA HALI WALI MKAVU. Mgaaga ni MJOMBA. Maana ya methali hii ni kuwa mjomba anapokuwa na mpwaye, hawezi kula wali mkavu kwa kuwa mpwa atafanya maarifa hadi kitoweo kipatikane. Maana yake halisi ni kuwa ikiwa kuna mtu anayeweza kusaidia kutatua tatizo lako, huna haja ya kuwa na wasiwasi.
Hivi ndivyo nilivyokuwa nikiilewa methali hii tangu zamani.

Baadaye nimekuja kusikia hawa "wahenga" wa siku hizi wameibadili hii methali na kuwa: MGAAGAA NA UPWA HALI WALI MKAVU. Maana yake mtu anayerandaranda (mgaaga) ufukweni mwa bahari au ziwa (upwa), hawezi kula wali mkavu kwa kuwa huenda akapata kitoweo ama kutoka kwa wavuvi au akavua yeye mwenyewe.

Hii methali imekaaje wadau? Which is which? Mimi nadhani imechakachuliwa.
 

Ya pili ndiyo sahihi. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu. Wengine huzigeuza tu. Kwa mfano "Bandu bandu humaliza gogo". Wengine wakasema "Bandu bandu, baba yake Sadru." Au:"Simba mwenda pole ndiye mla nyama" eti wao wakasema: "Simba mwenda pole, iko gonjwa tu? Hapa wakiwatania wale ndugu zetu wa mashariki.
 
Amen Kiongozi
 
Ahsante Kiongozi.

Umetisha
 
Kiongozi ufafanuzi wako umeenda Shule.

Ahsante sana
 
Choko choko mchokoe pweza....
Naogopa kutoa Jibu la kubahatisha


La kuvunda.....

Halina Ubani

Papo kwa papo.....

Na hapa pia naogopa kutoa Jibu la kubahatisha

Ukiona vyaelea.....

Ujue vimeundwa

Kitendawili....teega..juu majani,katikati kuni na chini chakuka
Mti wa Muhogo.

Juu Majani, ni Kisamvu.

Katikati Kuni, ni ule Mti wenyewe wa Muhogo.

Na chini Chakula, ni Mihogo
 
Haba na haba.....
Hujaza Kibaba


usiache mbachao......... .
Kwa Msala Upitao


Usitukane wakunga..........
Naogopa kubahatisha

Akutukanae mchana.......... .
Hakuchagulii Tusi


Ukiyastaajabu ya musa............ .
Utayaona ya Firauni


Mchumia juani...................
Hulia Kivulini


usiache mbachao..........
Kwa Msala upitao

Zimwi likujualo...........
Halikuli ukakwisha


Mdharau mwiba..............
Huota Matende


Chokochoko chokonoe.........
Naogopa kubahatisha


Dua lakuku......
Halimpati Mwewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…