Neno Shukrani pia linatokana na neno la kiarabu "Shukran". Waarabu wengi wanatamka hivyo au kusema hivyo badala ya ahsante/asante.
Lakini jamani angalieni neno hili "WANYE" ambalo limetumiwa na mwandishi huyu. Ametumia neno hili vibaya. Hapa alitakiwa kuandika "Wenye visus vya ukimwi". Wahamiaji hawawezi "kunya" virus vya ukimwi.
Mfano: Hatuwezi kulazimisha watu "wanye" virus vya ukimwi.
"mtu anye"
"watu wanye"
KISWAHILI NI LUGHA YETU LAKINI TUNAKIFAHAMU VIZURI ?
...........................................................................................................
Waziri Mkuu wa Australia apingwa kwa kukataa wahamiaji wanye virusi vya ukimwi
2007-04-14 16:23:44
Na EAR HabariMashirika mbali mbali ya misaada duniani, yamekasirishwa na hatua ya waziri Mkuu wa Australia Bw. John Howard kupinga wahamiaji wenye maambikizi ya virusi vya Ukimwi kuingia nchini humo.
Akiongea na radio moja wakati wa ziara yake mjini Melbourne, katika jimbo la Victoria, ambapo aliulizwa juu suala hilo, kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya Ukimwi nchini humo, hasa katika jimbo hilo, Bw. Howard amependekeza kupigwa marufuku kwa wahamiaji walioathirika kuingia nchini humo, kwa madai kwamba hatua hiyo inaweza kupunguza ongezeko la maambukizi.
Hata hivyo wanaharakati wa mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Ukimwi nchini Australia wamesema kwamba sheria ya uhamiaji ya nchi hiyo tayari ina vipengele vinavyowabana waathirika, ambapo pia Taasisi ya taifa ya misaada Uingereza, imeyaita mapendekezo hayo kuwa ni kinyume cha sheria na ya kibaguzi.
· SOURCE: EAR
IPPMEDIA