kwa mujibu wa kamusi mpya ya Kiswahili sanifu, Fisadi ni mtu mbaya,mtongozaji,mharibifu,mpotevu, mwasherati, kama vile guberi.
Nadhani kwa tafsiri hiyo labda naweza kusema sio sahihi sana kama ni kutambulisha watu walioko kwenye list of shame, ingawa hao jamaa wa kwenye list of shame wanaweza kuwa na hayo yote lakini definition fupi ya kiingereza ni........ lack of integrity or honesty (especially susceptibility to bribery); use of a position of trust for dishonest gain.....hapa ukiwa ni pamoja na kutoa kupokea milingula, ten percent, danganya toto nyingi za kuwafanya wananchi wajinga, unawaambia tunajenga shule kumbe wanajenga vibanda vitakavyobomoka baada ya miezi sita. Kuna mambo mengi sana yanayohusiana na hii.