Kiswahili ni lugha ya kimaskini

Gor

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
2,791
Reaction score
850
Ndugu zangu watz nimefikia uamuzi wa kuona kuwa lugha ya kiswahili ni mojawapo ya sababisho la umaskini wetu.Mwezi December nilifanya utafiti wa kupima utajiri wa kuongea lugha ya Kiswahili,Kiingereza, na Lugha ya asili ya mama yake(Native language)kati ya mwanafunzi wa std 4 wa TZ na std 4 wa Kenya.Matokeo ni kuwa Mtanzania hakuweza kuongea kwa ufasaha hizo lugha tatu,Mkenya aliweza kuongea kwa ufasaha kabisa lugha zote tatu.Katika kiswaahili Mtanzania alikuwa anaweka 'R' penye 'L' na kinyume chake pia alikuwa anatumia maneno mengi yasio fasaha,Kiingereza hakuweza kutengeneza sentensi ya kumwomba maji mama yake na hakuweza kuongea lugha ya asili yake kabisa!.Hii ilikuwa tofauti sana na Mkenya ambaye aliweza kuongea kiswahili na kiingereza kwa ufasaha mkubwa pia aliweza kuongea lugha ya mama yake ya kiluo vizuri na kiluhya.


Rasimu ya katiba ililiona hilo hivyo kuweka lugha za taifa kuwa kiswahili na kiingereza.Hii ingefanya masomo yote isipokuwa kiswahili kufundishwa kwa kiingereza na hivyo kufanya kizazi hicho cha kitanzania kuongea kiingereza kwa ufasaha wakiwa bado primary school.Kwa mujibu wa mapendekezo ya kamati za bunge la katiba;wajumbe walio wengi wameondoa kiingereza na kuacha kiswahili kitumike kama lugha rasmi ya serikali lakini wajue wanazidi kuwatenga watanzania.Kenya wamefanya kiswahili na kiingereza ziwe lugha za taifa lakini kuanzia bush school(chekechea) ni kiingereza isipokuwa soma la kiswahili.Hii inatufanya tusiweze kujiamini na kuwa "maimuna".Sasa angalieni mapendekezo hovyo za hizi kamati za BMK ya walio wengi!.


Kiingereza ndio lugha kuu ya kitaalam na kibiashara ulimwenguni hivi.Hivyo ni vizuri tufanye watu wetu waweze kuongea kiingereza kwa kufanya kiingereza kufundishwa kuanzia chekechea masomo yote isipokuwa kiswahili tu.Yes we can.


Hebu fikiria itakuwa raha namna gani sokoni,kwenye dala dala,uswahilini,kule manerumango kwa binti kinyogoli ni these,this,what,how are you?,thank you,welcome!.:flame:
 
Umenishangaza kidogo, Utafiti wako. umeufanya kwa watoto wa primary school, alafu unatoa hitimisho jingine kabisa. Vipi mleta uzi au na wewe ni Mtanzania nini?
 
Pamoja na kuondoa Kiingereza kuwa lugha rasmi ya serikali, hawana mikakati ya kufundisha kwa ufasaha Kiingereza. Tukiacha majibu rahisi kuwa kuendekeza kiingereza ni utumwa, ukweli unabaki palepale, anayefahamu kwa ufasaha kiingereza , ana(advantage) zaidi ya yule wa Kiswahili tu. Hivyo lugha zote, na hasa KIINGEREZA kwa kuwa ni lugha ngeni, ingetiliwa mkazo kwa uzito.Dunia nzima kila mtu anahangaika kukijua kiingereza, kwani ni lugha ya biashara na taaluma. Ninachokiona ni kukwepa majukumu ya kuwajibika kwa kushindwa kufundisha Kiingereza. Hiyo haina tofauti na kuongeza ufaulu kwa kupunguza maksi.
 
Reactions: Gor
Vipi Mfananisho wako kati ya Nchi ya Kenya na Angola ambapo wananchi wa Angola hawajui Kiingereza kabisa na wanajua Kireno badala yake, Je, hapo unasemaje maana yake Kiuchumi Angola wapo mbali sana!

Je vipi kuhusu Kenya na Uganda mbona haujafananisha hapo? Na Je Uganda Na Tanzania?

Kwa kifupi ni kwamba wewe Kenya haupajui vizuri, kwa taarifa yako wananchi wengi wa Kenya kwa mfano Nairobi zaidi ya 70% hajui lugha yoyote kwa 100% yaani hawawezi kuongea kilugha chao vizuri, hawawezi kiingereza vizuri na pia hawawezi Kiswahili vizuri matokeo yake wamekuja na lugha mpya ambayo ni mseto wa Kiswahili na kiingereza na lugha nyingine waniita ,,sheng'', hivyo nenda Nairobi hata kutembea tu na usifikia kwa wadosi nenda uswazi ambako ndiko zaidi ya 70% ya Watu wa Nairobi wanaishi!
Hivyo kwa Maswala ya Lugha TZ tuko mbali sana si ajabu ktk Kusini mwa jangwa la Sahara tunaongoza Afrika!


 
Nimeshuhudia wanachuo wa ngazi ya diploma wakiandika sentesi kwa lugha ya kiswahili kwenye mtihani!.Nashukuru waliitwa na kupewe ONYO KALI na Lecturer.
 
Nyie ndo mnataka na kufuta kiingereza kwenye rasimu,bado nasema kiswahili hatufiki kokote sb hatuna pesa pia hatuna utaalam wowote.
 
Nyie ndo mnataka na kufuta kiingereza kwenye rasimu,bado nasema kiswahili hatufiki kokote sb hatuna pesa pia hatuna utaalam wowote.

Si Ujibu kwanza nilichokuuliza? Kama hauna Jibu sema tu!
 

Look at you
 
Si Ujibu kwanza nilichokuuliza? Kama hauna Jibu sema tu!
Ndugu yangu,katika mfumo huu wa uchumi kiswahili,kireno na kikwenu haitufikishi popote,Mradi tunafuata uchumi wa kibepari mabwana zetu ni Wamarekani na Waingereza,penda usipende.
 
Mleta Mada na wanao muunga mkono wamekosea kidogo. Kama Mkenya, kuna mambo amabayo najua, na naona tayari wamekosea.

Kwanza, Athari za lugha ya mama (kwa maoni yangu,) zimejaa Kenya kushinda Tanzania. Sijui ni kabila gani huko TZ ambalo lina tatizo na L na R. Ni lazima liwe kabila kubwa sana kwa sababu nilimeona kosa hilo pahala pengi. Uzuri wa TZ ni kuwa hili ndio tatizo pekee. Lingine - ambalo silielewi sana, ni tunapokuja kukanusha. utapata MTZ anasema, Sitokuja, Sitolia, na Mkenya atasema, Sitalia, Sitaenda.

Lakini unapokuja kwa mambo mengine, WATZ wako sawa sana, haswa kwa yale yanayohusu kujieleze na sheria za matumizi ya lugha (Grammar.) Mambo kama Ngeli, na hayo, waTZ wako juu, lakini sijui shuleni wako vipi. Juzi nilitazama kitabu cha darasa cha tatu cha Kenya nikaona wanasoma vitu kama Kihusishi Kionyeshi, Kihusishi Kimilikishi. Hadi darasa la saba/nane wanasoma Nomino ambata na vitu kama hivyo. Hapo awali, vitu hivi nilivisoma nikiwa kidato cha pili na nilitokwa na jasho sana.

Kuhusu kujua lugha zote tatu, utapata kuwa Kabila ambalo limeshikilia lugha yao ya mama sana ni wakikuyu na waluo. Shida ni kuwa waluo sio wabantu na hivyo hao huwa na ugumu sana kuongea kiswahili. Hawatilii maanani kabisa sheria za lugha. Lakini wakikuyu, hata awe tajiri kivipi, utapata mtoto yuaongeleshwa lugha ya Mama nyumbani. Mimi Mluhya lakini lugha ya mama sikijui.

Tukija sekta ya umaskini/utajiri, hamuelewi vile nyinyi mlibarikiwa kwa kuwa na kiongozi aliyeona umuhimu wa lugha ya Kiswahili. Tatizo lenu ni kuwa mlitaka kufanya vitu nusu-nusu. Ushawahi kujiuliza ni kwanini wazungu huwa hawana haraka ya kutumia lugha za watu wengine? Kwanini waafrikana kule afrika Kusini walisisitiza kutumia lugha yao kwenye shule zao? Viongozi wa kiafrikana walihakikisha watoto wao wamesomea shule zinazofundisha kwa kiafrikana hadi chuo kikuuu. Na hii ni lugha amabayo haiongelewi na watu zaidi ya miliona thelathini. Kwa nini sisi waafrika tunapenda kujidunisha?

Utapata wakuu katika serikali ya TZ wanapeleka watoto wao Kenya au Uganda ili wajue kiingereza vyema. huu ni upuzi na ujinga. Hiki ndicho chanzo cha umaskini.

Lile ningependa kusema ni nyie mpigane na ufisadi, siasa duni, na uwekezaji mbaya katika sekta ya elimu, mwaajiri waalimu wazuri wa kiingereza na mtafanikiwa. Ningekuwa Rais wa Kenya, ningehakikisha kiswahili kinatumika kufundisha hadi chuo kikuu.
 
Mi ni mtu mzima. Nilianza kujifunza Kiingereza nilipofikia darasa la tatu zama hizo. Nadhani ilikuwa vema kabisa nianze literacy katika lugha iliyokuwa karibu nami zaidi kabla sijaanza lugha za kigeni. Nilipofika sekondari kulikuwa na kipindi kifupi cha adjustment. Lakini baada ya hapo nimeweza kujifunza Kiingereza kwa kiwango kizuri tu kwa kiwango cha kitaalamu kabisa.
Mwanzilishi wa thread hii, unajaribu kufanya maoni yako kuwa facts au kitu kinachotokana na utafiti wako. Kwa mfano, wataalamu waliochunguza juu ya lugha za mafunzo ya awali watakuambia unalolidai la kuanza na lugha ya kigeni ni wazo ambalo si zuri kwa makuzi ya elimu ya watoto. Pia, kama ilivyo katika mfano wangu mwenyewe huo, kuanza kujifunza lugha ya kigeni baadae zaidi si chanzo cha kutokujifunza Kiingereza vizuri. Mimi na wale tuliosoma wakati wetu tulijifunza Kiingereza vizuri tu.
Kama utaangalia mifumo ya elimu ya nchi mbalimbali za ulaya utaona wanakisema sana Kiingereza. Lakini hawaanzi elimu yao na Kiingereza. Lakin wanapoanza kujifunza lugha za kigeni wanazifundisha vizuri pamoja na resources zinazotakiwa.
Wazo la kuabudu Kiingereza kiasi cha kuona kwamba lugha nyingine hazifai hapa duniani NDILO hasa wazo la kimaskini. Umaskini wa mawazo. Tunatakiwa kujifunza lugha nyingi na kupata umahiri wa hali ya juu. Kila lugha ina mambo muhimu. Stop this self-hatred.
 
wewe umekosea sana... maskini ni utafiti wako

angalia uturuki... ni sharti kwa katiba kwamba lugha ya asili iwe kituruki... hata ni haramu kufunza kiingereza mbele ya lugha ya taifa. Hii nchi ina utajiri sana. Ni nchi pekee inayotumia lugha ya kituruki.

angalia japani... hii nchi ni kisiwa na wote huko wanatumia lugha yao ya kijapani. Sio wengi wanaotumia lugha hii duniani... kitu kama milioni 60. bado hii nchi ni superpower.

angalia nchi nyingi zingine... ni hivyo hivyo.

kukuza lugha ya taifa ni kuimarisha utamaduni na kitambulisho ya nchi. Nchi ya kufaulu sio ya kuiga majuu. Stawisha mila ya afrika. Tanzania inakua sana siku hizi... yani uchumi inapanda asilimia 7 kila mwaka. Ngoja tu.
 

well said mkuu.,
 
mimi nakipenda kiswahili sana na naona ndio kinanifanya niwe mtanganyika na natamani ndio iwe lugha rasmi ya mawasiliano mitaani lakini shule kuanzia vidudu mpaka chuo kikuu english mwanzo mwisho kiswahili hakina misamihati ya kisayansi hakifai
 
bora iwehivyo hivyo tu kama ilivyo sasa primary level kiswahili kwakua hakuna vitu vya kusoma kwa undani zaidi mpaka kusema tutumie kiingeleza na sekondali level watumie kiingeleza.
 
Tanzania sio masikini wala tusidanganyane. Ni watu wachache wanaojilimbikizia madaraka na mali kwa ubinafsi wao ndio unaotesa watanzania. Watu hawa wachache ndio wanatupiga kiini macho kila siku eti sisi ni masikini wakati wao, familia na marafiki zao wanakula nchi kama wanaishi peponi.
Mkikaa kukisingizia kiswahili na kiyao ni kupoteza muda tu, wakati wajapani na wachina washatuacha nyuma miaka mia kenda, sisi tumebaki kufikiri kiingrereza ndio dawa ya umasikini.
Jukwaa huru, kila mtu na maoni yake, lakini kuna mambo mengine tufikirie kwanza kabla ya kuweka humu, tutachekwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…