KITABU #2.02; Successful Real Estate Investing (Kuwekeza Kwenye Majengo Kwa Mafanikio Na Robert Shemin)

KITABU #2.02; Successful Real Estate Investing (Kuwekeza Kwenye Majengo Kwa Mafanikio Na Robert Shemin)

Aliko Musa

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2018
Posts
209
Reaction score
315
Kwenye uchambuzi unaofuata nitakuwa nakushirikisha makosa matatu (3) au zaidi kila siku. Kitabu hiki hakina sura, hivyo nitakushirikisha namba za makosa hadi kufikie kosa la 75 kwenye kitabu hiki.

KOSA #01; Kutokuanza Kuwekeza Mapema Kwenye Ardhi Na Majengo.

Hili ni kosa kubwa sana ambalo nilifanya mpaka nilipofikia umri wa miaka 28. Ningefundishwa mapema na kuambiwa umuhimu wa kuanza kuwekeza mapema, leo ningekuwa nimepiga hatua kubwa sana kiuwekezaji.

Kisa Kutoka Kwa Mtoto Chris.

Mmoja wa wanafunzi wangu ambaye alikuwa ni mdogo kabisa aitwaye Chris alinunua kozi yangu alianza kuwekeza mapema.

Mama yake Chris alifika kwenye semina za Robert Shemin, kipindi hicho Chris akiwa na umri wa miaka 16 tu. Chris alianza kutafuta nyumba mara moja baada ya kumaliza kozi ya Robert.

Chris aliweza kutengeneza faida halisi (net profit) ya shilingi milioni 11 za kitanzania (sawa na dola 4,800 za kimarekani).

Kisa Kutoka Kwa David.

David akiwa na umri wa miaka 58 alistaafu kazi yake bila kupewa kiinua mgongo (mafao ya uzeeni). David alihudhuria moja za semina za Robert Shemin.

David apendezwa sana na mbinu ya kununua kwa kupanga kutoka kwa mwenye nyumba. David alinunua nyumba kwa kuwa mpangaji.

Hakuweza kulipia kiasi chochote cha fedha kwa sababu alinunua kwa kuwa mpangaji kutoka kwa muuzaji aliyehamasika. Ndani ya siku 30 za mwanzo baada ya kuandika mkataba na mwenye nyumba huyo, David aliweza kutengeneza zaidi ya milioni 13.5.

David alirudi kwa mwalimu wake bwana Robert Shemin huku akitokwa na machozi ya kujutia kuchelewa kuanza kuwekeza kwenye ardhi na majengo.

David alimuomba Robert kuendelea kutumia historia ya David kwenye semina zake zitakazofuata. Somo la muhimu; muda wa kuanza kuwekeza ni sasa.

KOSA #02; Kutofuatilia Mzunguko Wa Ardhi Na Majengo; Kuongezeka Na Kupungua Kwa Bei.

Sababu kubwa ya kubadilika kwa bei za ardhi na majengo ni uhitaji na upatikanaji wa ardhi na majengo (demand and supply).

Uwepo wa nyumba nyingi zinazouzwa kuliko idadi ya wanunuzi, hupelekea kushuka kwa bei ya nyumba hizo zinazouzwa.

Vilevile, uwepo wa idadi kubwa ya wawekezaji wenye uhitaji wa kununua ardhi au nyumba kuliko idadi ya nyumba zinazouzwa, hupelekea kuongezeka kwa bei ya nyumba husika.

Uwepo wa nyumba nyingi za kupangisha kuliko idadi ya wapangaji waliopo kwenye eneo husika hupelekea kushuka kwa kiasi cha kodi ya upangishaji kwenye mtaa husika.

Pia, uwepo wa idadi kubwa ya wapangaji kuliko idadi ya nyumba/vyumba vya kupangisha, hupelekea kupanda kwa kiasi cha kodi ya upangishaji.

Ongezeko la ajira ni sababu kubwa ya kuongezeka kwa uhitaji wa ardhi au nyumba. Sehemu ambayo kuna ongezeko kubwa la ajira za kudumu huongezeka uhitaji pia.

Majengo ya shirika la taifa na mashirika ya apatimenti mara nyingi huwa kwenye ukuaji mzuri wa uhitaji wa ardhi au nyumba.

Usitumie muda mwingi kufanya utafiti wa mizunguko hii ya ardhi na majengo, badala yake chukua tahadhari kuhusu mizunguko hiyo.

KOSA #03; Kutokuwa Na Uanachama Hai Kwenye Vyama Vya Uwekezaji Kwenye Ardhi Na Majengo.

Hii ni sehemu bora sana ya kuanza nayo kama kweli unahitaji kujenga mafanikio makubwa kupitia uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Mawasiliano ya watu muhimu kama vile wahandisi ujenzi, maafisa ardhi, mawakili, washauri wabobezi kwenye majengo, wapimaji wa ardhi (land surveyors), mafundi ujenzi, na wengine utapata kwenye vyama vya wawekezaji kwenye ardhi na majengo.

Kama Ilivyo Kwenda Kanisani.

Kwenda kwenye mikutano ya wawekezaji kwenye majengo ni kama ilivyo kwenda Kanisani. Waumini huendelea kwenda kanisani ili kusikiliza shuhuda za waumini wenzao.

Hivyo imani huboreshwa kidogo kidogo kadiri waumini wanavyoendelea kukutana pamoja na kubadilishana mawazo ya kiimani.

Ndivyo ilivyo pale unavyochangamana na wawekezaji wengine kwenye ardhi na majengo. Huyu atakupa hamasa hii na mwingine atakupa ushuhuda wa aina ile.

Huu ni mwanzo tu wa uchambuzi wa kitabu cha rafiki yangu Robert Shemin kiitwacho Successful Real Estate Investing; how to avoid the 75 most costly mistakes every investor makes.

Kwa ambao sio wanachama wa kundi la whatsapp liitwalo REAL ESTATE BEGINNERS hawatapata tena chambuzi za kitabu hiki kwa njia yoyote ile.

Muhimu; hujachelewa kupata chambuzi za kitabu hiki. Tafadhali jiunge na kundi la REAL ESTATE BEGINNERS kwa kulipia Tshs.5,000/= ambayo ni ada ya siku 30.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi kwenye majengo.

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom