Kitabu cha Enoch kinawataja malaika 200 walioasi ambao ndio waliiba Siri na teknolojia za mbinguni kisha wakamfundisha Binadamu

Kitabu cha Enoch kinawataja malaika 200 walioasi ambao ndio waliiba Siri na teknolojia za mbinguni kisha wakamfundisha Binadamu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
KITABU CHA ENOCH KINAWATAJA MALAIKA 200 WALIOASI AMBAO NDÎO WALIIBA WALIIBA SIRI NA TEKNOLOJIA ZA MBINGUNI KISHA WAKAMFUNDISHA BINADAMU

Anaandika Robert Heriel
Mtibeli

Kwa Wakristo na waumini wa Dini ya kiyahudi jina Enock siô geni Kwao. NI Moja ya binadamu ambao hawakuwahi kupatwa na umauti.

Kwa wale wasiomjua Enoch. Kw kifupi Enoch ni Moja ya Watu WA mwanzoni katika simulizi za Zamani za kiebrania ambao NI uzao wa Nuhu.

Enoch alizaliwa na Yaredi. Enock ni Babu yake Nuhu(Nuhu NI kitukuu cha Enock)

Kwa Mujibu wa simulizi za kiebrania, enock ndiye Mtu pekee aliyeweza kukutana na MALAIKA tofauti tofauti yàani zaidi ya mmoja. Binadamu Wengine waliowahi kukutana na MALAIKA walikutana aidha na Gabriel au Mikael au Rafael

Enock ndiye Mhusika pekee aliyeweza kuwataja MALAIKA wengi zaidi Kwa majina na Sifa zào za kimaumbile.

Enoch ndiye Mhusika pekee kwèñye Biblia aliyeweza kuelezea Mianga kama Jua na Mwezi na mizunguko yake.
Enock alikuwa MTU wa kusafirishwa na MALAIKA kutoka anga Moja kuelekea ñyiñgine. Ilikuwa kawaidà Kwa Enock kupotea hata miaka 50 bila kujulikana alipo.

Enock ndiye Mhusika pekee aliyeelezea Kwa majina MALAIKA 200 Walioasi na kuzaliana na WANADAMU.

Kwa jinsi nilivyoielewa simulizi ya Enock ni Kwamba, binadamu ni kama mnyama, tofauti yake ni utashi tuu.
Binadamu Hana uwezo wowote WA kubuni kitu hata Moto, sîjui, urembo, sîjui ndege, sîjui computer, sijui bastola, miongoni mwa TEKNOLOJIA zingine.

Stori ya KITABU cha ENOCH Kwa kifupi Ipo hivi;

1. Kûna mbingu 12 na kîla mbingu kuna MALAIKA wake Mkûu anayoiongoza.

2. Malaika 200 waliasi wakiongozwa na Kiongozi wao aitwaye Samzaiya. Viongozi Wengine ni Azazel

3. Katika hao MALAIKA kîla MALAIKA alikuwa na sîfa, uwezo na Ñguvu zake. Wàpo waliokuwa na mbawa Mbili, wàpo mbawa nne(serafi) wàpo WA mbawa sita (Makerubi) na yupo Malaika mmoja aitwaye Samael mwenye mbawa Kumi na Mbili(huyu role yake ipo kitofauti)

4. Malaika hawa walikuja kuzaa na Wanawake wa WANADAMU. Wakazaa majitu, nephili au miunguwatu (demigods)

5. Azazel Moja ya Malaika alioasi aliwafundisha Wanadamu Teknolojia za silaha, uchawi, unajimu, urembo kama kupaka makeup. Kitabu kinaeleza kuwa MALAIKA walioasi wakawafundisha mambo meñgi sana àmbayo Kwa Sasa ndîo tunaita Teknolojia na utandawazi.

Jambo lililonishangaza NI kuona mpaka masuala ya Teknolojia ya kutumia Dawa Fulani ili Wanawake wasibebe mimba ili kutoharibu urembo wao. Hii ilifanya Baadhi ya Wanawake waliotumia Teknolojia ya Kuzuia mimba baadaye kushindwa kupata Watoto. Enock anaeleza hayo.

6. Demigods yàani wale machotara wa Malaika na binadamu ambao Kwa uelewa wàngu ndîo nahisi wanaitwa Majini. Wakawa wanakula kupita kiasi Jambo ambalo mama zào(Wanawake wa kibinadamu) walishindwa kuwalisha, wale Demigods wakaanza Kunywa damu za watu, kisha nyama zào, kisha wakawa wanakula ndege, wanyama na samaki wa baharini. Kipindi hicho nafikiri wanyama kama Godzilla waliishia kuliwa na hawa demigods.

Urefu wao(hao Demigods) ulikuwa Mita thelasini kwenda juu na walikuwa na uwezo mchangayiko yàani uwezo WA kibinadamu na kimalaika.

7. Wanadamu wakawa wanalia kutokana na kuuawa na hawa Watoto chotara(demigods au wanefili).
Kilio Chao kilitokana na dhulma ya uhai, kuchukuliwa Wake zào, kuteswa n.k.

8. Kilio Kikafika Mbingu ya Tano Huko alikuwepo MALAIKA Mikael, Gabriel, Rafael na Uriel. Malaika hao nao cheo chao NI kikuu. Wakaweka kikao huku wakilalamika wao Kwa wao Kwa matendo yanayofanywa na kina Samzaiya na Azazel na wenzao.

Mikael akiwa Kiongozi wa Malaika AMBAO hawakuasi akamuita Baba yao(Mungu). Mungu akawauliza kûna nini mbona kuniita. Wanasema(akina Mikael), tazama Samzaiya na Azazel wanachokifanya Huko Duniani. Wameiba Siri za MBINGUNI Ambazo Mwanadamu hakupaswa kuzijua lakini waô wamewapa. Wamewafunisha siri zetu, Kisha wakazaa nao Watoto. Ndio maana unasikia kilio Huko Duniani. Umwagaji WA damu umekuwa Mkubwa.

9. Mungu akatoa Amri akina Samzaiya na wenzake wakamatwe Kisha wafungwe katika maeneo mbalimbali mpaka Siku ya hukumu.

10. Kuhusu Demigods Mungu akawaambia atafutilia mbali Watoto na kizazi cha demigods na Wanadamu walioasi (walioungana na demigods) Kwa kutumia Gharika.

11. Basi kulikuwa na vita Kali Baina ya Malaika walioasi na MALAIKA waaminifu. Upande WA waliasi ukiongozwa na Samzaiya na Azazel huku upande WA MALAIKA waaminifu ukiongozwa na Mikael, Gabriel, Rafael na Uriel.
Mungu akamteua Malaika WA Mbingu ya Tano Aitwaye Samael kuhakikisha Haki inatendeka katika vita hiyo. Samael maana yake sumu y Mûngu, Malaika wa Kifo àmbayo majukumu yake yalikuwa mosi, kuhakikisha Haki inatendeka, pili, kushawishi na kujaribu viumbe Wengine Mpaka Malaika wènyewe,

12. Samael ndiye aliyeuweka MTU WA ujuzi WA Wema na ubaya pale Bustani ya Edeni na kumtumia nyoka kumdanganya Eva.

13. Samael ndiye aliyemtuma Ammado yàani Malaika wa ukahaba kumlaghai Adamu Kisha adamu akalala na Ammado na kuzaa naye Mtoto

14. Samael alikuja kuanguka baàda ya kumchukua Lilith kuwa Mkewe na kwenda naye kwèñye Mbingu ya Tano

15. Samael ndiye aliyepigana na Yakobo usiku ule ambao Yakobo alikuwa anaenda Kwa Labani Mjomba wake.
Samael ndiye prosecutor na ndiye aliyemletea majanga Ayoub katika kupima Haki na ukamilifu wa Ayoub

16. Ingawaje Watu wengi wanamhusisha Lucifer kuwa ndiye aliyemdanganya Eva lakini Samael ndiye aliyefanya Jambo hilo.

17. Nuhu hakuwa Mtoto WA kawaida. Jambo lililopelekea babaake Aitwaye Lameki kutaka kumkana Kwa kuona amebambikiwa, Methuselah babaye Lameki akapeleka habari hizô Kwa Enoch(Babu yake Lameki)
Nuhu tofauti na Watoto Wengine wanapozaliwa kwa Wakati huo. Alikuwa amezaliwa akiwa mweupe kupitiliza mwenye nywele kama za dhahabu. Kwa Sasa ungemuita albino. Lakini kama hiyo haitoshi, macho yake yalikuwa yakiwaka kama taa na kujuza mwanga chumbani
Jambo hilo lilimfanya Baba yake, Lameki kuona huenda Mkewe alilala na demigod au Moja ya wale Malaika walioasi.

18. Enoch ndiye aliyemwambia Methuselah Mwanaye kuwa asihofu kuhusu Mtoto wa Lameck kwani NI wake, na ndiye atakuwa mkombozi wa Wanadamu na amepewa jukumu la kujenga Safina àmbayo Watu nane tuu ndîo watakaookoka Wakati huo ûkifika. Enoch akamuita kitukuu chake hicho jina Nuhu.

19. Samael ndiye aliyemlaghai Eva na kuzaliwa Kaini.

20. Gharika ikaja kufuta na kuangamiza Watu wôte waovu na wale Demigods ingawaje wàpo ambao waliescape

21. Nuhu alipata nafasi ya kuingia na nguo ya Adamu Ile aliyovikwa na Mungu kipindi kile walichoasi.
Baàda ya gharika Hamu Mwanaye Nuhu aliiba Ile Nguo àmbayo ilikuwa na maajabu. Kisha Nimrodi Mjukuu wa Hamu naye akaiiba. Yeye akaweza kûitumia katika shughuli zake za Kúpiga upinde. Baadaye akawa Mfalme.

22. Ibrahim alizaliwa Nuhu bado akiwa hai. Nuhu alikufa Ibrahim akiwa na Miaka 55
Hivyo hadithi zote za tangu Adamu Ibrahim alizipata Kwa Babu yake, Nuhu.

Kwa Leo tuishie Hapa.

Ijumaa Kareem

Robert Heriel
Taikon WA Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Aiseee, kwa hiyo huyo Samael ni nani kama sio Lucifer? kwahiyo kaini ni mtoto wa Samael sio mtoto wa Adamu? kuhusu technolojia ni kweli inatoka kuzimu, wana sayansi wakubwa wana mahusiano majini

Samael na lusifa NI wahusika wawili tofauti Kwa Mujibu wa simulizi za kizamani
 
Ufunuo wa Yohana 12:7-9

[7]Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

[8]nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

[9]Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

Kwenye hii vita ndiyo hiyo uliyoizungumza hapo juu? kama ndio huyo joka anayezungumzwa kama shetani ni yupi ndo huyo Samael au Lucifer?
 
Ufunuo wa Yohana 12:7-9

[7]Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

[8]nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

[9]Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

Kwenye hii vita ndiyo hiyo uliyoizungumza hapo juu? kama ndio huyo joka anayezungumzwa kama shetani ni yupi ndo huyo Samael au Lucifer?

Samael Huyu ni malaika mjaribu huja kukupima mtu aelekeaye nuruni Ndio maana alikuja kwa yakobo kumjaribu na hata kwa ayubu. Anapendwa sana upande wa giza sababu anawasaidia kuangusha watu wenye imani haba
 
Hapo mkiulizwa habari za mababu zenu hata kizazi cha tano tu hapo hamzijui

Kama hawakuandika unàtaka Watoto waô wajulie Wapi?

Waafrika NI wakati wetu kuandika historia za Maisha yetu ili Miaka 1000 ijayo kizazi chetu kisije uliza na kuongea Jambo la aibu na fedheha kama ulilolileta Hapa

Wewe hata ukifa Sasa hivi sina hakika kama umeandika popote hata Robo ya mambo muhimu ya uliyoyapitia katika Maisha yako
 
Aiseee, kwa hiyo huyo Samael ni nani kama sio Lucifer? kwahiyo kaini ni mtoto wa Samael sio mtoto wa Adamu? kuhusu technolojia ni kweli inatoka kuzimu, wana sayansi wakubwa wana mahusiano majini
Sio kweli sema baadhi Nuhu Mwanasayans wa kwanza alijenga meli kubwa ya kwanza duniani yaani safina kwa kuelekezwa na Mungu kuanzia vipimo,material hadi teknolojia ya ujenzi na uendeshaji hiyo meli

Na alikuwa mwanasayansi wa kwanza kujua teknolijia ya kufuga wanyama kuishi na binadamu ndani ya hiyio meli yaani safina bila wanyama wenyewe kudhuriana au kudhuru wengine.

Mungu ndie kiboko ya teknolojia na aweza mtumia yeyote kugundua kitu aliye tayari kuwa mgunduzi

Wazungu ,Wachina,wajapani nk wako tayari kwa ugunduzi na walijitoa hivyo miaka mingi ndio maana Mungu huwatumia kugundua sio Shetani

Mungu aweza mtumia yeyote kusaidia nchi au dunia kwenye jambo lolote la heri iwe biashara ugunduzi nk

Waafrika wengi hatujitoa kwa Mungu kuwa tutumie kwenye ugunduzi na teknolojia.

Tukiwa tayari atatutumis
 
Back
Top Bottom