Kitabu cha Enoch kinawataja malaika 200 walioasi ambao ndio waliiba Siri na teknolojia za mbinguni kisha wakamfundisha Binadamu

Aliye mtupa joka hakuona sehemu nyingine isipokuwa huku? Sasa binadamu ameasi kwa kutokutii maagizo. Halafu unawongezea tena joka na malaika zake ambao wanauwwzo wa kudanganya ulimwengu mzima
 
Ila binadamu jamani wanajua kutunga stori na watu kuziamini
 
sawa sijasoma vitabu vingi. Ila am curious to know which book in the bible kingetolewa and why? Hapo tu bosi.
 
sawa sijasoma vitabu vingi. Ila am curious to know which book in the bible kingetolewa and why? Hapo tu bosi.
Sijaelewa Unaposema Kipi kingetolewa but in really maybe ungeuliza Vipi vilitolewa?

So for stater Kuna Kitu kinaitwa Canonical Rules au canonical Criterion..

Hizi ni criteria zilizotungwa Na kukubaliwa kuwa Vitabu vitakavyoingizwa kwenye Biblia Viweze kufuzu Criteria hizo zipo nyingi ila unaweza ukasummerize kwa Criteria 3 tu...

  • Authentic – authentic maana Yake ni kwamba nakala hizo au Vitabu hivyo vinatakiwa kuwa halali na vya kweli na pia zilitakiwa kuwa Nakala halisi na sio Copy ya Waandishi....yaani ilitakiwa kuwa mwandishi awe ni halisia (PiGrapha)
  • Authoritative – mwandishi anatakiwa kutoa taarifa za kweli ikiwemo kuwa aliona tukio likitendeka kwa macho yake na akaliandika au Anaamini kile kilichotokea na ana mamlaka nacho..Yaani kama Daudi aandike zaburi ni yeye yaani Authentic na ni maandishi yake kabisa Authoritation au kama Daudi alikuwa na mwanafunzi wake aliyemsaidia kuandika Maandishi hayo ila ikiwa na uhakika kwamba aliyeandika alikuwepo kipindi cha Daudi na alikuwa na uhusiano na Daudi kwahyo akiandika zaburi atatumia Nafsi ya Tatu Umoja yaani Yiule daudi lakini kama akiwa si Daudi na akaandika Zaburi na akatumia Nafai ya kwanza umoja au Wingi..Inakuwa Ni kinyume cha kanuni na Inakuwa Pseudepigrapha
  • Inspired – vitabu Viwe vimeandikwa kwa Uwezo wa Roho mtakatifu..
KWa kuanzia ni kwamba Vitabu vilivyoondolewa kwenye Biblia na vitabu vilivyoachwa vyote ukivipima Vinapelea kwenye Mizani ya Canon..

So naweza kusema Vitabu vyote kwenye na vilivyoondolewa ni sawa
 
Nop kuna Vitabu vingi havikuwekwa kwenye Biblia sio kwamba Vina contradiction ila vinaendana na imani ya Kipind kile..
Kama wangekuwa bado wanachambua Biblia kuna vitabu sasa hivi vingeondolewa
Dr...
Hii post yako ilisema kama wangeendelea kuna vitabu vingetolewa hapo juu unasema ningeuliza vilibyotolewa.
Anyways, hivyo vilivyotolewa apokrifa na vinginevyo hvikuwa na mashiko kama ulivyoeleza hapo. Lakini kwa wakati wetu huu sioni kitabu Cha kutoa.
 
Sahihi kabisa..
je Unafahamu Mpaka sasa wanatheolojia wanajadili na wanakubaliana kuwa Kitabu cha Ufunuo hakikupaswa kuwa Kitabu ndani ya Biblia??

Unafahamu kama kwa uchambuzi Wa criteria za canon za kiBiblia Kitabu cha Luka,Marko na Yohana ni miongoni mwa vitabu havikuandikwa na mtu aliyemuona Yesu wala kukaa naye na Viliandika Hadithi kama Walimuona yaani Pseudepigrapha na kuna Vitabu viliondolewa kwenye Biblia kwa sababu tu ya Kuwa Pseudepigrapha..

kWahyo kama wangekuwa wanafanya Uchambuzi bado vitabu hivyo wangeviondoa Kwenye Biblia kwakuwa havikukidhi vigezo..

Na kingine unafahamu kwamba hata vitabu vya Torati vyote Vitano "Pentateuch" They are NonAuthentitative Scriptures???

Kwanini Kwa sababu claimant wa Muandishi anayesemekana ni Musa Sio muandishi halisi..
torati pia Iliwahi kuandikwa na Ezra ambaye sio Musa?? Kipindi cha kutka Wana wa israel Babeli??

Unafahamu chochote Kuhusu Documentary Hypothesis (JEPD theory) inaprove Torati sio.Autharitative na sio Authentitative kitu ambacho hata Theology inaprove hilo..

So kwa mujibu wa those Facts Bado Biblia kama ingekuwa inafanyiwa marekebisho vingi vingeendelea Kupunguzwa
 
Planet X au Nibiru naifahamu, pia tokana na Summerian Mythology ndio asili ya Annunaki.
Na mara ya mwisho the great deluge ilitokana na effect ya Nibiru katika dunia, kwamba inapokaribia Dunia kila baada ya miaka 3600 orbit ya dunia inashift na kusababisha maafa.
 
Ni miaka 2000 So inategemea Mwaka 2050 au 2060..
Safi sana Mkuu Uko well Informed
 
Uko sawa kabisaa. Lakini naona hivyo vitabu vya Luka na wengine uliowataja pamoja vimeandikwa na watu tofauti lakini vina coherence maana yake kuna uvuvio wa ROHO mtakatifu katika uandishi.
 
Hizi mambo za Ancient alien's, Sumerian Tablets, Annunak the book of Enoch, Gospel of Peter, Revelation by Peter, Gospel of Mary Magdalene, Lilith, na mambo yanayofanana na haya, usipokua makini unaacha kumuamini Mungu.
Kwa nini revelation of Peter imeondolewa kwenye Biblia?
 
Visa vya Anunaki hivyo.
 
Uko sawa kabisaa. Lakini naona hivyo vitabu vya Luka na wengine uliowataja pamoja vimeandikwa na watu tofauti lakini vina coherence maana yake kuna uvuvio wa ROHO mtakatifu katika uandishi.
Even a Fabricated Story can Form Coherence Mkuu...
NA ndo maana kuna kipimo maalumu cha Kupima Story kabla ya kuiamini..

Kipindi Nilipokuwa nasoma Bible Textual Analysis sanaa sana kwenye OT [Old testaments] (Textual Critiq)

Kuna maandishi mengi yana Ideas Sawa na yana maana Sawa na Ni hadithi za zamani zimeandikwa na watu tofauti ila zinakosa ubora wa Kuwa Za ukweli na Walishindwa kuyaweka kwenye Biblia Kwa sababu kwanza ni uongo pili vinakosa Analytical Truth..

ntakuandikia kimoja kama sio viwili tu..
Uthibitishwaji wa Nyakati (Nyakati inapimwa kwa Vitu Vingi kama Lugha iliyotumika Muda huo, Aina ya Uandishi, Miji ya Mda huo Na hata majina ya Miji)..

Kwa mfano..

Baba Yako alikuandikia Barua ya maelezo kabla ya yeye Kufariki mwaka 2001 akakuambia..

"Mwanangu Nimekuachia Mali nyingi sana ila mali hizo niliamua Kuzigawa katika sehemu mbali mbali Zingine zipo Mkoa wa Manyara na zingine zipo Mkoa wa Geita Mwanangu tumia Hizo mali vizuri, Kwani ni mali pekee Zenye utajiri wa Nafsi kuliko Utawala wote wa Rais Obama"

ukiisoma Kwa haraka haraka Habari hii kwa mwaka 2012 mpaka mwaka 2024 Unaweza ukaona Ni sawa na haina Shida ila kama ukituma critical Thinking and analysis utaona shida nyingi sna..

Kwanza mwaka 2001 hakukuwa na Mkoa unaitwa Manyara wala Mkoa wa Geita na wala Mwaka 2001 hakukuwa na rais anaiyeitwa Obama..

So obvious its fabticated story iliyotungwa Kwenye miaka Ya 2010 mpaka mwaka 2018 hivi..

Kwahyo ulifanya Textual analysis ya Maandiko ndani ya Biblia Yanafail kuendana na authentification na Autharitative Regulation..

Umesema Luka Ilikuwa na Uvuvio wa Roho mtakatifu, samahani kwa kusema hivi "I doubt that"..

Luka(Alikuwa ni Daktari wa Binadamu) mwenyewe anasema Ukisoma Luka 1:1-4..

Kuwa ametafuta Kwa kufanya Research na kuuliza wazee walioishi miaka hiyo na baada ya kuwauliza akaandika.. kwahyo unamaanisha Research pia Zina uvuvio??

na Elewa neno alilotumia Luka Kutunga

Kutunga Ni kubuni Jambo ambalo hapo kabla halikuwepo.. (Kama BAKITA wanavyitafsiri)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…