Kitabu cha Erick Kabendera huenda kikafanya vitendo vya utekaji na mauji vikapungua kama sio kwisha kabisa

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Ninahakika watawala hivi sasa wako shocked na yaliyomo katika kitabu cha Mwandishi, Erick Kabendera kilichopewa jina la "IN THE NAME OF PRESIDENT "

Watawala wataanza kuingia hofu kumbe hakuna siri hata wale tuliowaamini na kuwapa kazi ya kusimamia hizi operation ndio wa kwanza kutoa siri kwa watu ambao hakupaswa kujua nini kilitokea.

Watawala wataanza kujiuliza: Kama ya Mwendake yametoka hadharani, ya kwetu hayajatoka au hayatatoka siku tukitoka madarakani?

Watawala kwa sasa wako shocked na wamevurugwa na ndio maana wako kimya hawajui wa-react vipi na itawachukua muda kabla ya kutoa mwongozo wa namna ya kujibu hizi tuhuma.

Ukimya huu unanifanya niamini aliyoyaandika Kabendera yana ukweli hata kama sio yote. Vinginevyo, wangeshatoka hadharani kukanusha na pengine hata kuitaka serikali ya Uingereza imrudishe Kabendera nyumbani aje ajibu tuhuma hizi.

Jiulizeni inakuwaje Bi. Mkubwa nae katajwa katika hiki kitabu kuwa Mwendake alitaka kumfanyia jambo baya ila mpaka sasa hakuna alietoka kukanusha ?Mnafikiri ni hivi hivi tu?

Hivyo, ukimya huu una jambo nyuma yake na si ajabu baada ya muda baadhi ya watu wakaondolewa kwenye nafasi zao na wengine kupotezwa kimya kimya.

Kitabu hiki cha Kabendera, kinaweza kuleta mapinduzi makubwa katika vita hii ya kupinga vitendo vya utekaji na mauji.

Nashawishika kuamini kuwa Kitabu hiki kingetoka mapema, huenda kina Mzee Kibao na wengine waliouwawa au kupotea yasingewakuta yaliyowakuta.

Binafsi, kitabu hiki nakiona ni silaha ya ushindi katika vita ya kupinga vitendo vya utekaji na mauaji hapa nchini.

Tundu Lissu and Erick Kabendera, they both survived assassination attempts not to continue living, but to fulfil God's mission.
 
Kipindi Cha magufuli Kila step kigogo alikua anavujisha, yeye mwenyewe alijua Kuna leaks kwenye circle yake ya karibu, ni mjinga tu anaweza kuamini kua na resources zote at hand alizonazo Bado alimuita saa 8 ikulu eti akamshoot point blank.... Hizo habari kina kigogo isingepita hata Lisaa wangekua nazo
 
Ninahakika watawala hivi sasa wako shocked na yaliyomo katika kitabu cha Mwandishi, Erick Kabendera kilichopewa jina la "IN THE NAME OF PRESIDENT "

Watawala wataanza kuingia hofu kumbe hakuna siri hata wale tuliowaamini na kuwapa kazi ya kusimamia hizi operation ndio wa kwanza kutoa siri kwa watu ambao hakupaswa kujua nini kilitokea.

Watawala wataanza kujiuliza: Kama ya Mwendake yametoka hadharani, ya kwetu hayajatoka au hayatatoka siku tukitoka madarakani?

Watawala kwa sasa wako shocked na wamevurugwa na ndio maana wako kimya hawajui wa-react vipi na itawachukua muda kabla ya kutoa mwongozo wa namna ya kujibu hizi tuhuma.

Ukimya huu unanifanya niamini aliyoyaandika Kabendera yana ukweli hata kama sio yote. Vinginevyo, wangeshatoka hadharani kukanusha na pengine hata kuitaka serikali ya Uingereza imrudishe Kabendera nyumbani aje ajibu tuhuma hizi.

Hivyo, ukimya huu una jambo nyuma yake na si ajabu baada ya muda baadhi ya watu wakaondolewa kwenye nafasi zao na wengine kupotezwa kimya kimya.

Kitabu hiki cha Kabendera, kinaweza kuleta mapinduzi makubwa katika vita hii ya kupinga vitendo vya utekaji na mauji.

Nashawishika kuamini kuwa Kitabu hiki kingetoka mapema, huenda kina Mzee Kibao na wengine waliouwawa au kupotea yasingewakuta yaliyowakuta.

Binafsi, kitabu hiki nakiona ni silaha ya ushindi katika vita ya kupinga vitendo vya utekaji na mauaji hapa nchini.

Tundu Lissu and Erick Kabendera, they both survived not to continue living, but to fulfil God's mission.
Kwa bakht mbaya watanzania wengi hatuna tabia ya kusoma vitabu binafs kitabu changu cha mwisho kusoma ni this taim tumoro na nilikisoma ili nijibie mtihan
 
Kabendera anaweza kutoa kitabu kingine kumuhusu “mama” sababu style ya utekaji na upotezaji watu ni ile ile

Yaani ni kama vile kile kikosi kilichopo State House hakijavunjwa na kinaendelea kuchapa kazi as if nothing has changed
 
Kwa bakht mbaya watanzania wengi hatuna tabia ya kusoma vitabu binafs kitabu changu cha mwisho kusoma ni this taim tumoro na nilikisoma ili nijibie mtihan
Ni kweli unachosema ila iko hivi:.wanasiasa na wanaharakati watakisoma na watakuwa wananukuu aya au sentensi zenye ukakasi na kuzitamka mbele ya wananchi kupitia mikutano ya hadhara na hata kuzianisha mitandaoni kama ambavyo teyari imeanza.

Kwahiyo, haihitaji wananchi kusoma kitabu kizima ila hiyo kazi itafanywa na wanasiasa na wanaharakati na umma utajulishwa
 
Aliyoyaandika Kabendera yana baraka zote za hao hao unaowasema, lengo ni lilelile kuharibu taswira ya marehemu maana ili mentality yake na ideology zake zinaogopwa na watafuna keki ya Taifa.
Kwahiyo wameruhusu iandikwe habari kuwa Mwendake alitaka kumfanyia jambo Bi. Mkubwa?
 
Kipindi Cha magufuli Kila step kigogo alikua anavujisha, yeye mwenyewe alijua Kuna leaks kwenye circle yake ya karibu, ni mjinga tu anaweza kuamini kua na resources zote at hand alizonazo Bado alimuita saa 8 ikulu eti akamshoot point blank.... Hizo habari kina kigogo isingepita hata Lisaa wangekua nazo
Kama unamuamini kigogo wa mtandao X kwa 100 % wewe ni chizi
 
Kwahiyo wameruhusu iandikwe habari kuwa Mwendake alitaka kumfanyia jambo Bi. Mkubwa?

Lengo ni lile lile kudestroy image jamaa aonekane shetani ili kila kirusi Cheney ideology Ile kikichipuka watu wakikatae maana ni hatari kwa watafuna nchi.

Tukiacha ushabiki, huko mitaani JPM ni kama kipimo cha namna gani nchi inapaswa kuongozwa.
Hata yale mengine ambayo wengine wanatudanganya hayawezekani raia utawasikia wakisema "angekuwepo JPM/mwamba hili angefanya".
 
Lengo ni lile lile kudestroy image jamaa aonekane shetani ili kila kirusi Cheney ideology Ile kikichipuka watu wakikatae maana ni hatari kwa watafuna nchi.

Tukiacha ushabiki, huko mitaani JPM ni kama SI unit ya namna gani nchi inapaswa kuongozwa.
Totally impossible.
 
Tofauti ya sisi na watu weupe ndio kama hi ya Kabendera. Nasikitika sana kwa mateso alioyapata wakati ule alivokua mahabusu, mama yake mzazi alifariki na hakuruhusiwa kwenda kumuaga mzazi wake, very sad indeed. Pamoja na masikitiko yangu kwake, lakini swali ambalo hatutaki kujiuliza ni hili, why alikamatwa na kuwekwa maabusu? Alikosea nini? Again huyu ni miongoni mwa watu waliotoka na kufutiwa kesi na DPP kwa sheria ya pre bargaining, alilipa pesa nyingi sana ambazo hadi kigogo2014 alihoji, Kabendera kapata wapi pesa zote zile? Maybe aliokua akishutumiwa nayo ni ya kweli? Anyway, kaandika kitabu ambacho ukikitazama tu unaona kabisa, kitabu hiki hakikusudiwa kwa Watanzania; huyu kaandika kitabu kisomwe na wenye dunia yao na sio "Wahaya" wenzie na sie Wamatumbi, the book is more special for western countries. Now back to my point again, hivi katika historia ya kusoma soma vitabu hasa huko kwa hao ambao Kabendera kawakusudia kusoma kitabu chake, kuna mwandishi anaweza kuandika kitabu cha namna hiyo kwa nchi yake na akaendelea kuishi nchi hiyo hiyo? Sio rahisi, hakuna demokrasia na uhuru wa habari usio na mipaka. Waandishi wa nchi zingine hujaribu sana kuficha aibu ya nchi zao. Natolea mfano wa jambo moja, wakati Osama na Alqaeda walivopiga Pentagon na world trade center, kuna chombo chochote cha habari cha USA kiliandika kuhusu Wayahudi wale waliokua wakifanya kazi pale WTC na kupona kwao? Unadhani hawakujua? No, they knew it but kwa wao kutangazia ulimwengu kuhusu hilo tafsiri yake, nchi yao ni dhaifu mno katika intelligence, wangetamani dunia isijue, hawapendi nchi yao iendelee kujulikana kwamba ni super power. Sisi hatuwezi
 
Sasa ndio ujiulize kwanini serikali mpaka sasa iko kimya?Tuhuma kama hizi wanawezaje kukaa kimya? Ni wazi huenda kuna ukweli kwa baadhi ya mambo na ndio maana kuna kigugumuzi hata tu cha kukanusha au kuhoji ukweli wa yaliyoandikwa.
 
Mapenzi ya wananchi mitaani dhidi ya JPM ni makubwa sana, na raia wamejua meeengi kuliko walivyokuwa wakidanganywa.

Fikra za raia wengi kutaka binadamu wa jamii ya JPM aiongoze tena hii nchi ndio woga ulipo kuanzia ndani na nje ya nchi.

JPM ameonyesha madhaifu mengi ya waliomtangulia wanaoamini wao ni the best, hii imewajaza nongwa na kupambana kwa hali na mali kuwaonyesha JPM hakuwa kitu.

Bahati amelala hawezi kujitetea na wahusika wanapigana na marehemu ( udhaifu mkubwa kwao na ushindi mkubwa kwa JPM)
 
Back
Top Bottom