Daktari W Sindabhalla
JF-Expert Member
- Jan 29, 2017
- 600
- 580
Habari za Uzima WanaJamiiForums.
Kuna kitabu Nimekipoteza ktk mazingira Nisiyoelewa, kinaitwa UCHAWI UNAVYOKUPATA NA KUJIKINGA Cha mwandishi MUNGA TEHENANI wa FAMILIA YA JITAMBUE.
Huyu Bw. Alikuwa anatoa Elimu yenye Ufahamu na Maarifa ya viwango vya Juu Mno ambayo sijaona mwingine Kwa hapa TZ ana Maarifa kama Yeye.
( RIP. MUNGA TEHENANI )
Katika Kitabu hicho alizungumzia Uchawi wa kuruka kwa Ungo.
Anasema, Sio lazima iwe Ungo, Lakini Kuna uwezekano wa watu kuruka kwa kutumia vifaa ambavyo havitumiwi kurukia.
Kama Yupo Mtu ataruka Kwa kutumia Ungo, sio lazima Mtu Huyo awe mchawi.
Kuruka ama kusafiri Kwa Ungo ni suala la uwezo wa kujua Namna ya Kanuni Husika inavyotumika.
Uchawi ni Matumizi Mabaya ya Nguvu hizihizi tunazo zitumia kupata Mambo Mazuri.
Hayo ni sehemu tu ya Yaliyomo Ndani ya kitabu hicho.
TAFADHARI, ikiwa unajua mahali naweza kupata kitabu hiki Nakuomba unijulishe.
Na kama unacho kitabu kama hiki naomba kopi Tafadhari.
Na ikiwa una NONDO nyingine za MUNGA TEHENANI
Naomba tujulishane Jamani.
Ni hayo tu.
***UCHAWI NI NINI
JIBU LAKE NI HILI:
Kwa mujibu wa Mwandishi kitabu MUNGA TEHENAN ( RIP )
=> Uchawi ni Nguvu.
Kwa vyovyote ambavyo Mtu atatoa tafsiri, ataishia Kusema UCHAWI NI NGUVU.
=> Kila Nguvu Ina Kanuni zake. Bila Kanuni, Kitu chochote kitasita kuendelea
Hata Kula Kuna Kanuni. Kwamfano, Unaweza vipi kuchukua Chakula na Kukishindilia kwenye Njia ya Haja Kubwa 😆 Kisha ukatoa tafsiri kwamba Umekula Chakula?
Hata ukiamini kwamba Umekula, Kama ndivyo Ulivyo fundishwa, kwamba Huko ndiko Kula, Bado Kula huko hakutazaa matunda kwasababu KANUNI ya Ulaji haikuzingatiwa.
=> UMEME PIA NI NGUVU.
Ili Umeme Uzalishwe inapaswa kuwa na vifaa Fulani sambamba na KANUNI ya kuzalisha Umeme na kuendelea kuwaka.
Zipo Kanuni za kukufanya Umeme Usiwe na MADHARA Kwa watumiaji.
Hata kama wewe ni Fundi Mbobezi Kwa mambo ya Umeme, Bado Hauwezi kutumia KAMBA za katani kama Nyaya kuzalisha Umeme.
Kanuni lazima izingatiwe kupata Umeme
=> Sasa, kama unataka kuutumia Umeme Kwa Matumizi Mabaya ya kumdhuru mwingine, hiyo inawezekana.
...... Pengine utauingiza kwenye Maji. . . Lakini, Yeye aliyetegwa atadhurika ikiwa atagusa ama kuingia kwenye Hayo maji.
....... Pengine utauunganisha na chuma Cha Mlangoni ama getini, Hali kadhalika Yeye aliyetegwa atadhurika ikiwa atagusa huo mlango/geti.
Nje ya hapo hawezi kudhurika.
Kwahiyo Nguvu zote zinakanuni.
=> Kujua kwamba Kuna Uchawi ama kuto kujua,haitoshi kumfanya Mtu aweze Kuloga au kulogwa.
=> Kuamini ktk Uchawi ama kutokuamini, , , , Haitoshi kumfanya Mtu Kudhuriwa na wachawi ama kutokudhuliwa nao.
Attachments
17395100065847162554509929673813.jpg