Kitabu cha Panga la Shaba


poa msalimie mzee wa kutoa nyongo hapo..
 
wazo zuri mkuu.
Usisahau mrabaha wa hao wenye wazo chanzi katika filamu yako.
Au sio?

Suala la mrahaba kwa wenye hakimiliki halina mjadala. Dunia ya sasa ukitaka kwenda jela basi tumia kazi ya mtu bila makubaliano ama usimpe chake.
 
Reactions: ADK
Hebu tuvute kumbukumbu ya ile issue kwa ufupi...

Suzzy baada ya kutafuta cheo kazini kwa muda mrefu bila mafanikio anadokezwa na shoga yake juu ya mganga makini Panga la Shaba(PLS) ambae ......................

Aisee asante kwa kutukumbusha. Binafsi nachokumbuka ni dada fulani kuolewa na Panga la Shaba baada ya kuwekewa dawa ya kumpumbaza, kisha baadaye PLS kukamatwa na polisi.... nilishapoteza kumbukumbu. Thanks.
 
Ukivipata 3D. holla' @ ADI......

Nimesoma comments zenu, interesting.... Really Really interesting....
 
Reactions: 3D.

Mkuu unastahili pongezi kwa namna ya pekee sana.
Umerudisha kumbukumbu za wengi hapa hasa nadhani pia 3D amekata kiu yake japo kwa 45%.
Kuna kitu umekizungumza hapo katika jibu lako kwa Bishop, "lugha ya picha"
huo ni ufanisi wa hali ya juu wa kifasihi ambacho fanani yeyote lazi awe nacho, kama ukichek wakina Musiba na Mtobwa (may their soul s RIP) walifanikiwa sana katika kuwaumba Joram Kiango na Willy Gamba,
kitu hichi kimekuwa adimu sana kwa waandishi wetu tena, japo natambua uwepo wa vipaji vingi vikubwa sana.
3D bado kuna nafasi ya kutuonyesha ambacho hatujawahi kukiona,
ntakuwa pale!
 
Reactions: 3D.
Aisee asante kwa kutukumbusha. Binafsi nachokumbuka ni dada fulani kuolewa na Panga la Shaba baada ya kuwekewa dawa ya kumpumbaza, kisha baadaye PLS kukamatwa na polisi.... nilishapoteza kumbukumbu. Thanks.

Huyo dada alikuwa anaitwa Christina na hata kitabu hicho cha michoro kilikuwa kinaitwa Christina.
Mtunzi ni marehemu Mashaka Y Mapunda na mchoraji wake ni John Kaduma.
Mchawi Panga la Shaba ndiye aliyeigwa na wakenya kwenye igizo la Tausi akiitwa Sangoma ambaye pia alimuoa mwanamke aliyekwenda kufuata tiba. huyo mama alikuwa mke wa mzee kasri
 
Reactions: 3D.

Mgalanjuka ametupa kumbukumbu nzuri. Kuna wakati Tanzania ilikuwa na waandishi waliobobea kama uliowataja. Nimesoma baadhi ya vitabu vya E. Musiba kama Njama na Kikosi cha Kisasi; Ben Mtobwa: Roho ya Paka, Tutarudi na Roho Zetu? Waandishi wengine ni John Msimbe Simon Simbamwene (JOMSSI) aliyeandika Operesheni Sukuma Namba Nane, Kivumbi Uwanjani; pia Mwandishi Faraj Hussein Hassan Katalambullah: Simu ya Kifo, Majarida ya Film Tanzania eg Kesi ya Wakenda etc.

Kwa vipimo vyangu hapajatokea tena mchoraji mahiri kama John Mathias Kaduma aka John Black aka Fogasta aka Baba Jack aka Mohammed Hussein (Mmachinga) akijinadi kutumia mfumo wa Samba Msele (4-4-2 style). Sorry kwa porojo guys!! I just loved this guy. RIP John Kaduma.

Currently najaribu kujifua ili nifikie uwezo naoutaka katika kutengenza film. Huenda ikanichukua muda mrefu kidogo, maybe mwaka na nusu hivi kutokana na majukumu ya hapa na pale, lakini ninajifunza very seriously. Ningependa kama Panga la Shaba anaruka kwa ungo basi iwe hivyo, kama atapanda fisi basi iwe hivyo pia. Tough though!!!

You better be there jouneGwalu.
 

Jina Christina nalikumbuka. Hivi hakukuwa na toleo zaidi ya moja ya vitabu vya Panga la Shaba? Nahisi kama niliona viwili tofauti. Umenikumbusha igizo la Tausi. Nadhani lilivuma kama ilivyokuwa kwa Tamthilia ya La Mujer De Mi Vida ya Barbarita. Namkumbuka mke wa Kasri, nadhani alikuwa anaitwa Zuri. Nilikuwa nawapenda Kasri, Rehema, Dama, Sitti, Mponda (wa kwanza), Kibibi , Joto na Ondieki. Nimemsahau jina binti aliyekuwa anajiita "Mtoto kindakindaki", alikuwa matata sana!! Mganga Sangoma alikuwa anapaza sauti ya "Waungwana!!! Ndiyo nawasikia waungwana!"
 
Jamani kuna mwandishi wa Zanzibar Shafi Adam Shafi, ila kuna mwenzie alikuwa ana mpelelezi anaitwa Bwana Msa, kwakweli nimetafuta sana vitabu alivyotumika huyu local sleuth bwana Msa, kama kisima cha giningi..kosa la bwana Msa na vinginevyo...

Naombeni sana kwa mwenye kujua aniPM pia mimi nacollect vitabu vya zamani vya waandishi wetu mahiri, naombeni msaada,mkuki nanyota publishers wana stock ndogo na kwingineko sijapata

Tafadhalini mwenye kujua anisaidie nimetafuta sana, ila not Shigongo books please.
 
Reactions: 3D.

Nimesoma kitabu kimoja cha Shafi Adam Shafi "Kuli." Hiki ni moja ya vitabu nilivyovipenda sana. Kitabu hiki kinagusa sana maisha ya Mzanzibari katika mazingira ya utumwa na uonevu. Pia kinazungumza juu ya mapenzi ambayo binafsi nayaona kuwa mazuri sana... mapenzi ya "nakupenda hivyo hivyo ulivyo"... Nakumbuka Rashidi alihukumiwa kwenda jela huku mkewe mjamzito akishuhudia. Rashidi alimtazama mkewe akamwambia "Yana Mwisho Haya" (Na ndiyo sentensi ya mwisho ya kitabu hicho).

Nikiviona ntakushtua.
 
Hivi vitabu huyu mtu anavyo, alinionesha wakati akitafuta
moja ya hadithi ambayo alitaka nimuandikie script ya filamu
ili aangalie uwezekano wa kutengeneza movie...

Hivi nyie watu mnaishije kama Homo-Erectus?

Hicho kitabu mnachotaka kutoa kopi ni mali ya mtunzi na huo mnaotaka kufanya ni wizi. Cha msingi ni kuwasiliana na mtunzi (mwenye haki miliki) ili awaambie namna ya kukipata au awape idhini ya kukinakili.

Na wewe unayetaka kutengeneza movie, hilo linaweza kukupa hasara, wasiliana na mwenye story yake kwanza
 

Hii live tena bila ya chenga,,,,1985-95 enzi zile mambo ya heshima na adabu mashuleni
 
umenikumbusha mbali sanaaaa! niliacha mdogo wangu akaungua na pasi. niliambiwa nimuangalie mtoto, mie nipo bussy nasoma panga la shaba! mtoto akaungua na pasi, nilichapwa na mama na baba kwa kunichangia, sitasahau katika maisha yangu, kipondo kile!
 
huyo dada aliitwa suzy au christina???
 
simu ya kifo mtunzi alikuwa ni Hammie Rajab,vitabu kama operesheni vipusa,nteko vano maputo ,njama,kikosi cha kisasi,hofu,kikomo(wizi wa almasi mwadui-Elungata),hapa musiba(RIP) alikuwa ananata na uhandishi si mchezo,hasa anapomzunhumzia mpelelezi mashuhri willy gamba,na katibu muhtasi wa chief,binti muadilifu mwenye mapenzi ya kweli ,ambaye kila wakati macho yake yalikuwa yanalengalenga machozi anapoagwa na will ,marcelina,acha jombaa,jamaa alitishsha sana
 
marehemu John Kaduma namkumbuka sana kwa michoro yake ktika kitabu cha James Akeke,jambazi sugu,na mpenzi wake anna makambi,wakienedesha kundi la ujambazi la mashetani weusi wa kijiweni kulisambaratisha kundi la mashetani weusi wa minazini,humo ndani utamkuta Onnu,pispo,nk katika kambi ya kitwana James akeke,wakati kwa kambi ya shetani weusi wa minazini wakiongozwa na ben dos,utawakuta kina pilima,abbasi,gebiu,nk nk,wacha bhana,wakuu mwenye hiki kitabu tafwadhari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…