Mgalanjuka ametupa kumbukumbu nzuri. Kuna wakati Tanzania ilikuwa na waandishi waliobobea kama uliowataja. Nimesoma baadhi ya vitabu vya E. Musiba kama Njama na Kikosi cha Kisasi; Ben Mtobwa: Roho ya Paka, Tutarudi na Roho Zetu? Waandishi wengine ni John Msimbe Simon Simbamwene (JOMSSI) aliyeandika Operesheni Sukuma Namba Nane, Kivumbi Uwanjani; pia Mwandishi Faraj Hussein Hassan Katalambullah: Simu ya Kifo, Majarida ya Film Tanzania eg Kesi ya Wakenda etc.
Kwa vipimo vyangu hapajatokea tena mchoraji mahiri kama John Mathias Kaduma aka John Black aka Fogasta aka Baba Jack aka Mohammed Hussein (Mmachinga) akijinadi kutumia mfumo wa Samba Msele (4-4-2 style). Sorry kwa porojo guys!! I just loved this guy. RIP John Kaduma.
Currently najaribu kujifua ili nifikie uwezo naoutaka katika kutengenza film. Huenda ikanichukua muda mrefu kidogo, maybe mwaka na nusu hivi kutokana na majukumu ya hapa na pale, lakini ninajifunza very seriously. Ningependa kama Panga la Shaba anaruka kwa ungo basi iwe hivyo, kama atapanda fisi basi iwe hivyo pia. Tough though!!!
You better be there jouneGwalu.