Kitabu cha Panga la Shaba

Halafu kuna kitabu kilikuwa kinaitwa tuanze lini? sikumbuki mwandishi je kunayeyote anakijua?
 

Aliyetaka kuandikiwa movie ndiye mwenye hakimiliki ya hicho kitabu,
ni mkurugenzi wa Wamasa Publication, wachapishaji wa Sani pamoja
na hicho kitabu. Una jingine la kusema?...
 
Enzi zile primary bush huko nilisoma na dogo mmoja ambaye kaka zake walikuwa Dar, basi kila sani likitoka wanamtumia dogo gazeti. Dogo alikuwa kusoma anakukodisha kwa sh 5 ya mapembe enzi hizo.

Kumbu kumbu zinaniambia Kaduma alikuja akafanya kazi kwenye kijarida kinaitwa Tabasamu, nilikuwa napenda stori zake za michoro ya kibabe yenye mambo ya mapenzi pia.

Kulikuwa na jamaa mwnigine anaitwa Marco Tibasima naye alikuwa mchoraji mzuri sana. Kuna stori moja ilikuwa inahusu mambo ya ujambazi na utemi Shimo La Udongo (sikumbuka vizuri jina la kitabu) nayo ilikuwa nzuri sana.
 
Mimi natafuta kitabu USHINDI WA MAHABA. Ni cha zamani sana na mwandishi sikumbuki. Msaada jamani.
 
Nadhani mwandishi alikuwa ni John Msimbe Simon Simbamwene. Kama nakumbuka vizuri.

Umenikumbusha habari za Simbamwene. Kampuni yake ilikuwa inaitwa JOMSSI Publications. Kama sijasahau sanduku la barua lilikuwa 118 Morogoro!! Alipata kuandika vitabu kama Chini Ya Ulinzi, Operesheni Sukuma Namba Nane (OSNN) na Kivumbi Uwanjani. Mmoja wa characters wake alikuwa Inspector Fog.

Habari za Panga la Shaba sina kumbukumbu nazo sana.
 
Mbona sasa imebaki kuwa stori za vitabu hivi vyote vilivyotajwa humu je hakuna jinsi ya kupata hata kama ni kufotoa.

Baba yangu alikuwanacho cha mwanamalundi ngoja nimuulize kama bado kipo.
 
Hivi hawa waandishi wanaendaga wapi? Kulikuwa na Hammie Rajab mwandishi wa SANDA YA JAMBAZI nadhani aliandika pia JOTO LA FEDHA.
 
Hivi hawa waandishi wanaendaga wapi? Kulikuwa na Hammie Rajab mwandishi wa SANDA YA JAMBAZI nadhani aliandika pia JOTO LA FEDHA.

Duniani hatukai milele!! Hammie Rajab alifariki nadhani mwaka juzi. Sikumbuki hadithi zake ila najua amepata kuandikia jarida lililokuwa linaitwa Busara ila halikuvuma kama Sani. Katuni ya John Kaduma ya Power Mbulumbundu ilianzia katika jarida hili.
 
Rukia mtoto kindakindaki
 
Halafu kuna kitabu kilikuwa kinaitwa tuanze lini? sikumbuki mwandishi je kunayeyote anakijua?

Tuanze Lini kiliandikwa na Kajubi D Mukajanga. Ni story ya wivu wa mapenzi uliosababisha jambazi John Botefo na mdogo wake Charlie kupanga mauaji ya kutisha
 
No Haha hongera mkuu
 
Kuna kitabu kilikuwa kinaitwa Pande na ukimwi hatari sana kingine kilikuwa kikiitwa Bomu la vipusa,kingine kikiitwa tamaa humo ndan kuna katuni za majini zarizari,janjinini na mengine mengi nakumbuka mbaaaaali na uhenga unazidi kunisogelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mrejesho umeshatengeneza hiyo cinema.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…