Kitabu cha Panga la Shaba

Kitabu cha Panga la Shaba

Halafu kuna kitabu kilikuwa kinaitwa tuanze lini? sikumbuki mwandishi je kunayeyote anakijua?
 
Hivi nyie watu mnaishije kama Homo-Erectus?

Hicho kitabu mnachotaka kutoa kopi ni mali ya mtunzi na huo mnaotaka kufanya ni wizi. Cha msingi ni kuwasiliana na mtunzi (mwenye haki miliki) ili awaambie namna ya kukipata au awape idhini ya kukinakili.
Na wewe unayetaka kutengeneza movie, hilo linaweza kukupa hasara, wasiliana na mwenye story yake kwanza

Aliyetaka kuandikiwa movie ndiye mwenye hakimiliki ya hicho kitabu,
ni mkurugenzi wa Wamasa Publication, wachapishaji wa Sani pamoja
na hicho kitabu. Una jingine la kusema?...
 
Enzi zile primary bush huko nilisoma na dogo mmoja ambaye kaka zake walikuwa Dar, basi kila sani likitoka wanamtumia dogo gazeti. Dogo alikuwa kusoma anakukodisha kwa sh 5 ya mapembe enzi hizo.

Kumbu kumbu zinaniambia Kaduma alikuja akafanya kazi kwenye kijarida kinaitwa Tabasamu, nilikuwa napenda stori zake za michoro ya kibabe yenye mambo ya mapenzi pia.

Kulikuwa na jamaa mwnigine anaitwa Marco Tibasima naye alikuwa mchoraji mzuri sana. Kuna stori moja ilikuwa inahusu mambo ya ujambazi na utemi Shimo La Udongo (sikumbuka vizuri jina la kitabu) nayo ilikuwa nzuri sana.
 
Mimi natafuta kitabu USHINDI WA MAHABA. Ni cha zamani sana na mwandishi sikumbuki. Msaada jamani.
 
Nadhani mwandishi alikuwa ni John Msimbe Simon Simbamwene. Kama nakumbuka vizuri.

Umenikumbusha habari za Simbamwene. Kampuni yake ilikuwa inaitwa JOMSSI Publications. Kama sijasahau sanduku la barua lilikuwa 118 Morogoro!! Alipata kuandika vitabu kama Chini Ya Ulinzi, Operesheni Sukuma Namba Nane (OSNN) na Kivumbi Uwanjani. Mmoja wa characters wake alikuwa Inspector Fog.

Habari za Panga la Shaba sina kumbukumbu nazo sana.
 
Mbona sasa imebaki kuwa stori za vitabu hivi vyote vilivyotajwa humu je hakuna jinsi ya kupata hata kama ni kufotoa.

Baba yangu alikuwanacho cha mwanamalundi ngoja nimuulize kama bado kipo.
 
Hivi hawa waandishi wanaendaga wapi? Kulikuwa na Hammie Rajab mwandishi wa SANDA YA JAMBAZI nadhani aliandika pia JOTO LA FEDHA.
 
Hivi hawa waandishi wanaendaga wapi? Kulikuwa na Hammie Rajab mwandishi wa SANDA YA JAMBAZI nadhani aliandika pia JOTO LA FEDHA.

Duniani hatukai milele!! Hammie Rajab alifariki nadhani mwaka juzi. Sikumbuki hadithi zake ila najua amepata kuandikia jarida lililokuwa linaitwa Busara ila halikuvuma kama Sani. Katuni ya John Kaduma ya Power Mbulumbundu ilianzia katika jarida hili.
 
Jina Christina nalikumbuka. Hivi hakukuwa na toleo zaidi ya moja ya vitabu vya Panga la Shaba? Nahisi kama niliona viwili tofauti. Umenikumbusha igizo la Tausi. Nadhani lilivuma kama ilivyokuwa kwa Tamthilia ya La Mujer De Mi Vida ya Barbarita. Namkumbuka mke wa Kasri, nadhani alikuwa anaitwa Zuri. Nilikuwa nawapenda Kasri, Rehema, Dama, Sitti, Mponda (wa kwanza), Kibibi , Joto na Ondieki. Nimemsahau jina binti aliyekuwa anajiita "Mtoto kindakindaki", alikuwa matata sana!! Mganga Sangoma alikuwa anapaza sauti ya "Waungwana!!! Ndiyo nawasikia waungwana!"
Rukia mtoto kindakindaki
 
Halafu kuna kitabu kilikuwa kinaitwa tuanze lini? sikumbuki mwandishi je kunayeyote anakijua?

Tuanze Lini kiliandikwa na Kajubi D Mukajanga. Ni story ya wivu wa mapenzi uliosababisha jambazi John Botefo na mdogo wake Charlie kupanga mauaji ya kutisha
 
No
Asante mkuu Bishop, nadhani pia kwa kuwa kitabu chenyewe kilikuwa kwa style ya comics inachangia kumbukumbu kutofutika kirahisi. Unakuwa na mental picture ya characters wote mpaka wale maafande wawili mmoja mfupiii na kofia yake inayofunika nusu ya uso.
Haha hongera mkuu
 
Kuna kitabu kilikuwa kinaitwa Pande na ukimwi hatari sana kingine kilikuwa kikiitwa Bomu la vipusa,kingine kikiitwa tamaa humo ndan kuna katuni za majini zarizari,janjinini na mengine mengi nakumbuka mbaaaaali na uhenga unazidi kunisogelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Actually, kusudio langu la kukitaka kitabu hicho ni kuona ikiwa kina uzito ule ule nilioupata nilipokisoma utotoni (nadhani nilisomewa maana kwa wakati huo very likely nilikuwa sijui kusoma... sina kumbukumbu nzuri). Kama stori yake itakuwa ina uzito huo nakusudia kutengenezea sinema hasa kama imagination na level nayoikusudia inaweza kutekelezeka (kutengenezeka) hapa Tanzania.

Kuna baadhi ya hadithi na simulizi za Tanzania ambazo ni excellent kwa kutengeneza sinema kuliko kuwa na themes zile zile ambazo kwa sasa zinalalamikiwa sana. Asante Bishop.
Mrejesho umeshatengeneza hiyo cinema.?
 
Back
Top Bottom